Chadema Pokeeni Mafisadi, hata Wasafi, uamuzi ni wenu, kazi mmeifanya

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,162
3,162
Mimi nashangaa sana kuona Baadhi ya Watanzania wanailaumu Chadema eti kwanini inapokea watu wanaotuhumiwa na Ufisadi mfano Lowasa. Chadema imewapigia ngoma Watanzania kuhusu ufisadi lakini bado Watanzania walio wengi hawaoneshwi na kuchukizwa na Ufisadi. Utaona hivi siku za karibuni kwenye mchakato wa kutangaza nia ndani ya CCM Watuhumiwa wa Ufisadi walionekana kuwa na wafuasi wengi. Hivyo, kama Watanania hawachukizwi na ufisadi, kuna tatio gani Chadema ikiwapokea mafisadi ili kuwafurahisha Watanzania?. Mimi nasema CHADEMA pokeeni mafisadi ili siku moja Watanzania wajue Umuhimu wenu wa wakati ule mlipokuwa mkipinga Mafisadi.
 
Katika Kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu tumeweka siasa za uanaharakati chini. Tunaangalia kura tu. Hata kama mfungwa gerezani kajiandikisha na kama tu atatupa kura yake tunampokea. Kama Mramba na Yona watatupa kura yao tunawakaribisha sana. Tunachojali sasa ni kura tu. Ninyi mwawaita mafisadi kwetu sisi ni wapiga kura wetu. Njoo kwetu ninyi nyoote mnaitwa mafisadi na ccm , nasi tutawapokea!!
 
wewe ungesema mnaanza kujiandaa kisaikolojia kuhusu hoja zenu za majukwaani juu ya ufisadi. hoja ya ufisadi mmeiua wenyewe baada ya kuanza kupokea na hata kuwafanya wateule wale mliokuwa mkiwananga kwa ufisadi. ni jukumu lenu kuwaambia watanzania kinyume chake.
 
Back
Top Bottom