CHADEMA ondoeni aibu

buy_dustbin.jpg
 
Chama ambacho kinashika namba 2 kwa kupata ruzuku, kimeshindwa kupata ofisi yenye hadhi katika manispaa ya Temeke. Ofisi ya wilaya ni fedheha tupu ipo mkabala na Kisuma Bar Mwenbe Yanga hivyo inakuwa ni kero kwa wanachama kutembelea ofisi.
CHADEMA badilikeni!! Ruzuku mnapata, mnamalizia katika maandamano??

Jk anakaa ikulu ni nini ameshakifanya kwa wananchi wake ktk ahadi alizowahi kuzitoa?Nimekusoma hapo juu kuwa unasema ofisi yenye hadhi ni yenye viti na meza sasa hao watendaji Wa Chadema ktk hiyo ofisi wanakaa chini?Magamba a.k.a. MAFILILi @ work
 
Chukua hiyo ruzuku then ugawanye kwa shughuli zote chama uone kama hivyo viti vya kuzunguka unavyovitaka kama itawezekana.Ofisi ina fanicha ambazo ni zawakaida kulinganisha na maisha ya Mtanzania.
 
Mimi nafikiri, wewe uliyeandika uzi huu ni wale wale amboa hamna la kusema zaidi ya kuiandama Chadema, mimi nimepita sehemu nyingi za nchi hii, na nimeona office nyingi za Chadema zinazokizi haja ya kuwa office ya Chama, Chama bado kinakuwa na wala sisi wananchi hatuhitaji viyoyozi kwenye office za chama, tunahitaji sehemu ambayo tutamkuta mwenyekiti ama katibu na kueleza shida zetu na kutekelezewa, kama ni kununua kadi ziwepo, kama ni kulipia kadi mihuri na risti viwepo. Kama untaka viyoyozi baki huko huko ccm office za magamba, ila ipo siku tutwauliza walizijenga kwa jasho la akina nani.
 
Huu ni udaku tu! Tungekuwa na hiyo unayo hiita ya hadhi unge anza kusema cdm mmepata pesa wapi kujenga ofisi kama hile.

Kila siku maneno maneno ,binadamu bana.
 
Chama ambacho kinashika namba 2 kwa kupata ruzuku, kimeshindwa kupata ofisi yenye hadhi katika manispaa ya Temeke. Ofisi ya wilaya ni fedheha tupu ipo mkabala na Kisuma Bar Mwenbe Yanga hivyo inakuwa ni kero kwa wanachama kutembelea ofisi.
CHADEMA badilikeni!! Ruzuku mnapata, mnamalizia katika maandamano??
wazo suri sana,

nina imani haumaanishi ofisi expensive bali unamaanisha ofisi itakayowawezesha hata wanachama kuwa comfortable zaidi
 
CCM WANAGHOROFA pale mtendeni street,
Wanaukumbi mkubwa unaojengwa maeneo ya image kama unakwenda kilimani club ambao utatumiwa na uvccm.

Je uwajibikaji wa chama chenye majengo mazuri na utendaji wa chama ambacho hakina majengo au ofisi nzuri unatofautiana?nakama unatofautiana utendaji wa chama kipi kati ya chama cha jumba zuri (ccm),na chama cha jumba bovu (cdm) niwakupendeza na wahaki?
 
Kipi kilicho bora kati ya kuwa na Ofisi nzuri na zenye hadhi (kama CCM) bila huduma NA kuwa na Ofisi za aibu(kama CHADEMA) zinazotoa huduma bora na kwa wakati!!??

MAFILILI nadhani utupe msimamo wako juu ya hili ili tupate pa kuanzia na msingi wa hoja yako!!

I'LL BE BACK!!
 
ugomvi mkubwa wa Mbowe na Chacha Wangwe ulikuwa ni Mbowe kukataa kupeleka sh. laki moja kila Wilaya kwa mwezi. Sasa kama laki moja kwa mwezi kwa Wilaya mnashindwa mnafikiri shughuli za chama zitafanyika vipi? Ndio maana presence ya chama katika maeneo mengi inakuwa felt wakati wa maandamano tu!
 
Nawe usisahau kumjengea Babu yako kibanda kwa posho unazopokea kwa Nepi, unatia aibu sana, unapata posho kibao, posho ya umbea, uzabinazabina, uongo, uzushi, ufitini n.k n.k
 
Chama ambacho kinashika namba 2 kwa kupata ruzuku, kimeshindwa kupata ofisi yenye hadhi katika manispaa ya Temeke. Ofisi ya wilaya ni fedheha tupu ipo mkabala na Kisuma Bar Mwenbe Yanga hivyo inakuwa ni kero kwa wanachama kutembelea ofisi.
CHADEMA badilikeni!! Ruzuku mnapata, mnamalizia katika maandamano??

Mkuu, mimi nadhani wako sahihi.
Ofisi nzuri haimkomboi mwananchi maskini anayeishi kwa dola moja ya kimarekani sawa na kiasi cha Tsh. 1,500/= kwa siku.
Waache waitumie hela hiyo kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili wajitambue.
Ujue mkuu, wapo wabunge wa CCM wameingia bungeni kwa kuwaongopea wapigakura kwamba wakichaguliwa wanauwezo wa kuwapata wahisani ili kuwaletea maendeleo katika sehemu zao!!!???
Kwa kukosa elimu ya uraia na kujitambua watu wanashindwa kuelewa kwamba maendeleo yao yataletwa na wao wenyewe kupitia viongozi wao waliowachagua.
Hivyo elimu wanayoitoa sasa itawawezesha kuwadharau waomba kura wa aina hiyo na kupata viongozi bora watakaonusuru maisha yao na vizazi vyao.
 
roho iliniuma sana nikafikiri ofisi haina kadi wala viongozi kumbe viti na meza,hiyo haina shida kwani hakuna mlo unaotakiwa uliwe hapo mezani kwa starehe hivyo.............gamba mkubwa
 
Chadema kimejaa ukiritimba wa hali ya juu. Ruzuku inaishia kugawana posho za maandamano.
 
Back
Top Bottom