CHADEMA (Odinga) vs CCM (Uhuru) siasa za nje!

CHADEMA (Odinga) vs CCM (Uhuru) siasa za nje!

John Pombe Magufuli alikwenda kuzindua kampeni za Odinga na kumpigia debe, je ndani ya CCM yuko katika nafasi gani? Je ni hatua zipi za kinidhamu anastahili kuchukuliwa na CCM?!

Nape analo jibu, huenda mwili wa magufuli upo ccm lakini moyo wake upo Chadema.
 
ni lini chadema wametangaza kumuunga mkono odinga au kenyata au ccm wametangaza lini mbona mnapenda kuzusha mambo na kujiingiza kwenye siasa za watu.....mambo ya kenya waachieni wakenya wenyewe mara huyu hivi yule vilee watanzania bana ya kwenu yamewashinda mnaanza umbea

Watanzania wanafikiri kenya ni wajinga kiasi hiki mpaka waendekeze siasa za majungu kama ambavyo wanataka kulianzisha humu.
 
Kwa Watanzania kama hawa hizi ndizo hoja za siasa za kimataifa. Kwa mawazo kama haya siyo ajabu hata za kwetu zimetushinda.
 
Hii ni porojo usitake kuchagulia watu upande na kuleta uchonganishi wa mahusiano mabaya kwa Nchi zetu za Africa Masharika kisa fikra zako za Uchadema na UCCM!

Huyu mleta mada anafikiri KENYA wana siasa za uCHADEMA CHADEMA aza kutafuta umaarufu kwa majungu
 
Mkuu usipotoshwe, Yericko Nyerere ni verified user hapa JF au unahoji integrity ya JF? Andrew Vs Yerecko Nyerere imekaa kisiasa zaidi usiingilie mambo yao na wala usisumbuliwe na mambo yao.
By the way, tunaangalia hoja zaidi kuliko mleta hoja. Ni kosa kuhusisha hoja na mleta hoja.
Asante mkuu kwakumuelewesha huyo ndugu yetu.
 
Cha kuzingatia hapa ni kuwa siasa za Kenya hazitabiliki,hasa sababu ya ukabila na udini,
mkumbuke uchaguzi ukirudiwa wagombea wengi watamuunga mkono Kenyatta kwa sababu ya ukabila"
 
CCM ni makini sana, wala hawakutamka kuhusu uungaji mkono kwa mgombea yeyote; CHADEMA kutokana na kukosa ukomavu na busara wamejiingiza kichwa kichwa kumuunga mkono ODINGA, jioni ya leo watakula jeuri yao na kupata pigo la kisiasa tukielekea uchaguzi 2014 na 2015
Hapo kwenye italic na underlined, naona hujatulia unaandika kishabiki, Mhe. John Pombe Magufuli alimtangaza Raila kwamba ndiye anayefaa kuiongoza Kenya, sijasikia, sijaona wala sijaambiwa kwamba kuna kiongozi yeyote wa CHADEMA amemuunga mkono mgombea kati ya hao wawili. Kimsingi nilifikili kama CCM wasingemuunga mkono mgombea yoyote wangemuonya Magufuli na kukanusha kwamba ule ulikuwa utashi wake na si msimamo wa Serikali ya CCM. Ingawaje mwandishi wa thread hii anaonekana kusahau baadhi ya mambo. Kinana ameenda kumsaidia Raila kuiba kura kama alimvyomsaidia Kikwete kuiba akamzawadia makontena ya pembe za ndovu na kama haitoshi akampa na ukatibu mkuu wa CCM.
 
Nikusahihishe kidogo mkuu, ccm inamuunga mkono Uhuru Kenyata, na uhuru ameizuru tz kwa siku mbili akihanikiza usaidizi huo,

Kinana yupo mikononi mwa Uhuru na si Odinga,

Sula magufuli haikutangazwa tu lakini alipewa onyo na chama chake, hivyo ccm wakaww wanacheza mchezo huo kwa umakini sana ili kuogopa kutojichanganya kwakuwa tayari wazuri wao alishajichanganya.

Hivi ninavyokwambia nikuwa macho na masikio ya ccm yapo kwa Uhuru bila kikomo.
 
Wewe una matatizo si kidogo.
By the way, uchaguzi wa Kenya ni very sensitive matter kutokana na historia ya uchaguzi uliopita. Vithread vya kipumbavu kama hivi vinaweza kuwa sababu ya kukosekana msuluhishi just in case jambo baya likitokea.
Utu uzima haupigi hodi, UMESHAKUWA mkubwa behave kama mkubwa...
Msuluhishi siku zote ni Marekani. hawa akina JK wanatumwa tu.
 
Maghufuli ni CCM na alienda kuhudhuria mkutano wa kumuidhinisha Odinga kugombea uraisi wa Kenya
 
Wewe Yeriko, hukusikia ndugu Pombe Makufuli alienda kumpigia kampeni odinga?, naomba ufafanuzi.
Ni ukweli usiotiliwa shaka kuwa CCM inainjinia uchaguzi wa Kenya, na ipo upande wa Uhuru mmoja wa waogombe urais wa Kenya,

Vivyo hivyo chama kikuu cha upinzani nchini chadema, kimejikita katika siasa za kimataifa kwa hapo Kenya huku karata yake kikiitupa miguuni mwa Raila Odinga mmoja wa wagombea anaepewa nafasi kubw ya kushinda kupitia muungano wa vyam ndugu.

Vita hii tunaiangaza kama ni yamapambano ya chadema na ccm kuelekea 2015 hasa kila mmoja akisafisha njia ya kuungwa mkono kumataifa,

Ikiwa ni hivyo tayari ccm na chadema kila mmoja ashashinda kete moja moja, kwanza ni Chadema Zambia kwa bwana Satta, na CCM Congo kwa kijana Kabila ambako dhahiri utawala unakula huku umeshikilia sahani mkononi kwani hakuna tumaini la kuweka mezani chakula chini ya M23.

Je ni chadema (Odinga) ama CCM (Uhuru)

Karata yangu naitua kwa Chadema.
 
Nimekutana uso kwa uso na Mzee wa Tembo aka mjuzi wa kupika matokeo Mzee Kinana yupo hapa Nairobi kama msimamizi wa kimataifa!!! Sijui kama atamsaidia Uhuru mbinu za wizi wa kura, lakini ukweli mambo ni magumu na si rahisi kusema nani ataibuka mshindi kati ya Uhuru na Laila. Misururu mirefu imeanza kupungua sasa, hii ikiashiria kwamba wengi tayari wamepiga kura mpaka sasa!!!

Tiba
 
Same here mkuu, ila si kwa ajili ya kabila lake
Inawezekana si kwa kabila lake, lakini Jumamosi nilishtuka sana nilipoona wanapeperusha mabendera ya Marekani uwanjani Nyayo kwenye hitimisho la kampeni zao. Sijui kama waliihusisha na ujaluo wa rais wa Marekani au walikuwa na maana gani. Nimeishi na hawa jamaa, wana ubaguzi wa kikabila kupindukia. I hate them for this.
 
Nimekutana uso kwa uso na Mzee wa Tembo aka mjuzi wa kupika matokeo Mzee Kinana yupo hapa Nairobi kama msimamizi wa kimataifa!!! Sijui kama atamsaidia Uhuru mbinu za wizi wa kura, lakini ukweli mambo ni magumu na si rahisi kusema nani ataibuka mshindi kati ya Uhuru na Laila. Misururu mirefu imeanza kupungua sasa, hii ikiashiria kwamba wengi tayari wamepiga kura mpaka sasa!!!

Tiba
Hapa nipo naangalia live coverage ya citizen tv. Nairobi bado kuna msururu wa kutisha. Sidhani kama wapigakura wa Bongo wangevumilia hali hii na jua kali.
 
Huyo Uhuru si ndio anakesi The hegue? Alafu Uingereza tayari imeshasema haitafanya kazi nae kutokana na mashtaka anayokabiliwa nayo.

Mimi naona Raila atashinda kwa kishindo. Ccm kwa jini wao kila sehemu ni poor analysis?
Mwendesha Mashitaka alikuwa kwetu Tz majuzi!!! Uhuru inaungwa mkono na magamba!! Draw the line!!
 
Back
Top Bottom