CHADEMA nzito zaidi ya CCM

CHADEMA nzito zaidi ya CCM

Kumbe umekurupuka kiasi hicho jaribu basi hata kusoma kidogo najua unafukuzana na muda ili buku 7 yako iingie

Unajua kuna kudonoa na macho kwa kusaka kupiku vineno fulanim. Hii inahitaji ujuzi na kujua nini kimo.. mimi kama mdau wa humu kama sivutiwi kusoma yote sijisukumi.. mleta mada angeweka ujanja wa kuvutia kuanzia juu labda ningesoma hata kama anaipa kiki upinzani..

So ndio hivyo
Kwaheri.. soma wewe jifurahieeeree na hayo ya sijui nini nini mnayopenda upinzani kusoma.. hiyo buku saba yangu kama unalipwa wewe kwa niaba yangu mbona hujaniambia kabla!!!
 
Hahahaaaaaa!!!!!usikimbie rafiki yangu hiyo dozi leo imekuingia pole sana CCM zenu zimetimia lazima muelekee kibra
 
Hahahaaaaaa!!!!!usikimbie rafiki yangu hiyo dozi leo imekuingia pole sana CCM zenu zimetimia lazima muelekee kibra

Haijaniingia tena wewe ndio unanifanya hata nisirudi kuisoma baadae nikiona uzi upo upo bado kwa new posts.. unafikiri kuniandikia kuwa niusome nilikuwa sijui unalotaka kunisukumia...

Sasa subiri nipate ile kuboreka humu.. labda kwa sasa nipo bizi na uzi zingine humu.. na huyo ameandika kichwa cha uzi tu ni ndoto kutaka kujisafisha juu ya kukimbiwa.. maneno yangu ya post ya mwanzo yanasimama sibadili.

Jifunze kudonoa hata 5 words kujua nini kimo na kuona mboreko mtu unasepa..

Jua ningeusoma ningejibu labda gazsti na zaidi.. ila kurudia rudia kuwaeleza majambo kila mara huwa napunzika kusubiria wakati mwingine... jua kuwa na matumizi mazuri ya kichwa sio kujiandikia tu
 
Rudi uisome hii nyuzi best naamini utaingiza kitu kipya kichwani nakuondoa makando kando ya Lumumba karibu sana CDM kwa maendeleo ya Tz
 
Hata Lowassa asingekatwa Ccm asingehamia Chadema, Nyarandu asingepokwa uwaziri CCm asingehamia Chadema. Yapo mengi tu hapo usijifanye huyaoni, umeeleza madhaifu ya CCM tu lakini hujatueleza uzito wa Chadema unatokana na nn

Lkn kumbuka Akina nyarandu sidhan Kama wanafuta hela cdm Zaidi ya wao kutoa hela Yao mfukoni.
 
Rudi uisome hii nyuzi best naamini utaingiza kitu kipya kichwani nakuondoa makando kando ya Lumumba karibu sana CDM kwa maendeleo ya Tz

Hivi leo vipi mbona mpo wengi mnaniambia nikaribie Chadema.. huko mtajiju maana ningekuwemo nanyi na tabia zenu ningewacharaza wote kwa jinsi mnavyoboa... ha ha ha haaaaaaaaa

Cocochanel hadi raha jamani.. endelea ulipo siku ukiwa tayari njio twende pamoja kuchukua kadi ya uanachama wa kwa Magufuli.
 
Lakini Nyalandu ni tofauti maonana ameuacha ubunge aliokuwa nao.
 
Hivi leo vipi mbona mpo wengi mnaniambia nikaribie Chadema.. huko mtajiju maana ningekuwemo nanyi na tabia zenu ningewacharaza wote kwa jinsi mnavyoboa... ha ha ha haaaaaaaaa

Cocochanel hadi raha jamani.. endelea ulipo siku ukiwa tayari njio twende pamoja kuchukua kadi ya uanachama wa kwa Magufuli.
Ukija kwetu tunakutoa huo undondocha wa Lumumba akili zikikurudia tunakuacha huru
 
Ili tupime kiwango cha ujinga wako

Ha haaaaa ningekuwa hivyo usingeninukuuu hadi sasa.. acha wivu sema nikufmdishe kuwa supa upstairs.. ila jua hutanipita.

Eeeeh nije niwasaidie.. sema hilo.. eeeeh... endelea kuota.. mimi mbona hata humu siandikagi kufikia uwezo wa kiwango nachojua ninacho.. kwa sababu sitaki pia nyie upinzani kuwafunzia humu majambo.. maana mngekuwa mnaringa sana kwa kiki ambayo ningewapatia.. na sababu mnaboa bora nishangilie tu lori la Magufuli.
 
Yaani CCM yangu imefikia mahali pa kununua wanachama? Yaani CCM yangu inakufa hivihivi. Halafu siioni mikutano ya kampeni ya CCM yangu jamani. Iko wapi? Yaani kila kona ni CHADEMA inajaza watu hata kama mgombea wao yuko jela duh!!! Jamani CHADEMA wabaya nyiyeeee!!!!
 
KWASASA CHADEMA NI CHAMA KIKUBWA KULIKO CCM!

Kwanza hongera sana Mbowe na Jopo zima lililopo ndani ya CHADEMA kwa kujenga chama kikubwa kuliko CCM kwa wakati huu na kuendelea.

Kuna watu hawawezi kuniamini kirahisi lakini napenda kuwaambia kuwa siku si nyingi CCM itakuwa chama cha UPINZANI na hapa ndipo nchi hii itakuwa kwenye mstari wa maendeleo.

KWALEO NISISEME MENGI NGOJA NIJIKITE KWENYE MSINGI WA HOJA YA MSINGI!

Katika historia ya Tanzania haijawahi kutokea wakati ambapo ccm ikawa na haja ya wanachama kama wakati huu, huu ni wakati ambao ccm wanafanya kukutafuta na kukubembeleza ili uhamie kwao, hata kama ulikuwa diwani tu watakutangaza kwenye vyombo vya habari na hata Rais atakushika mkono huku akikusifia.

Huu ni wakati ambao hata fedha inatumika kuwanunua wapinzani ili wahamie ccm kwani kimsingi hakuna sababu ya kimsingi ya kumtoa mtu upinzani aende ccm na ndio maana wakishakubali kuhamia utaratibu wa media coverage kuwatangaza lazima ufanyike.
Hii ni kwasababu kuna uhaba mkubwa wa watu huko ccm.

CCM inapitia kipindi kigumu sana, inapitia kipindi ambacho watu wamekosa imani na chama hicho huku pia ikionekana kwenye jamii kwamba kuwa mwanaccm ni ushamba.
Katika uwepo wake madarakani kwa miaka tangu UHURU ccm haina tena cha kuwadanganyia wananchi kwani bado Tanzania ni kati ya nchi masikini sana duniani Na hata Afrika, ni nchi ambayo ina kiwango kikubwa cha ujinga, ni nchi ambayo ina kiwango kikubwa cha maradhi kiasi kwamba Meli ya wachina ikija kutoa huduma za afya watu maelfu wanagombania huduma utadhani hakuna serikali kwenye hili taifa.
Katika hali kama hii ccm itawaambia nini tena wananchi, yote waliyoahidi hawajatekeleza na bado hali ya masiha ni ngumu mno!

Kilichopo kwa sasa ni kwamba wanajitahidi sana kuhakikisha wanaendelea kubaki madarakani ndio maana wanatumia nguvu nyingi mno za haki na zisizo za haki.

Katika awamu hii nguvu kubwa mno ya vyombo vya dola inatumika kuangamiza upinzani. Kama CHADEMA isingekuwa kuliko CCM yanini kutumia nguvu hizo?

Wakati mwingine hata hatari za kiuhai zipo na ishara zinaonekana ili madaraka yaendelee kushikwa.

Katika hali kama hii hata sheria zinapindishwa ili ikiwezekana wapinzani(CHADEMA) Wasiwasiliane kabisa na wananchi.

Hapa hata kama wewe ni mbishi kiasi gani lazima ukubaliane na mimi kwamba aliyeko madarakani ana hofu mno ya kuondoka kwani anaujua huu ukweli ambao wewe unataka kuupinga.

Nataka nieleweke kwamba ingelikuwa kuna uwanja sawia wa kufanya siasa kwa sasa kati ya CCM na UPINZANI hapo ndipo ungeamini kwa asilimia 100 hiki ninachokisema.

Hebu fikiria kidogo kwamba katika wakati ambao CCM imekimbiwa na mawaziri wake wakuu wawili, MZEE KINGUNGE NGOMBALE MWIRU, mawaziri, wabunge na wengi wengineo lazima wawe waoga kwani uzani kwasasa umelalia kwenye UPINZANI.

Wakati wa JK ilifika hatua watu wakihamia ccm sio ishu kabisa kwani CCM ilikuwa imejaa na hata unaweza ukaenda ccm ukakosa cheo kabisa kwani kumejaa. Hali ni tofauti sana kwa sasa kwani unaweza ukahama upinzani leo na kesho ukawa MKUU wa MKOA, DC,MKURUGENZI n.k Hii ni ili kuwavutia watu waje na maana yake ni kwamba MPINZANI KWENDA CCM KWASASA NI HADI AAHIDIWE AU APEWE FEDHA, MADARAKA, OPPRTUNITY n.k bila hivyo hakuna sababu nyingine.

Hebu fikiria hoja kama za KATAMBI na KAFULILA, yani hazina mashiko kabisa, eti Kafulila anasema amehama upinzani kwasababu ufisadi sio agenda tena ya upinzani… hivi kweli tatizo la TANZANIA linaloleta mkwamo ni UFISADI PEKEE? Jiulize.

Nawaambia ukweli na naomba mniamini kuwa endapo PATROBAS KATAMBI, KAFULILA, MASHA na wengineo wangekuwa na vyeo ambavyo dau lake ni kubwa kuliko hilo wanaloenda kupewa na ccm kamwe wasingehama.

Pamoja na hoja hizo lakini pia haya yanafanyika katika wakati huu ambapo CCM inaogopa kupoteza kata zote katika huu uchaguzi mdogo wa madiwani.
Dalili zinazoonekana huko katika msimu huu wa kampeni ni kwamba wataznania kwa sasa hawaitaki ccm kabisa na hali hii ni tishio mno ndio maana sasa kodi za watanzania inabidi zitumike kuwanunua wapinzani.

Nataka nikwambie jambo moja ambalo ni endapo Upinzani nao wangekuwa na Fedha ama vyeo vya kuwagawia wanachama wake walahi CCM isingewapata mpinzani anayehamia kwao!

HATARI KUBWA ILIYOPO KWA CCM NI HII!
Ipo siku fedha zitaisha kwani fedha hazioti kama majani. Mtapataje wanachama?
Ipo siku hao mnaowachukua watachoka kwani roho zao hazipo nanyi wamekuja huko kimwili.
Ipo siku mtashindwa kuhudumia wananchi kwani hela za kodi mmefanyia manunuzi, watawang’oa kwa mapanga na marungu.
Ipo siku mtachukua mashushushu na watawadhalilisha kama hamuamini ulizeni kule ARUMERU.

USHAURI WANGU KWENU CCM
Pambaneni na maisha na hali za watanzania hiyo ndio dawa ya kuuua upinzani! Japo hauwezi kufa kabisa kwani hata ulaya pamoja na maendeleo makubwa waliyo nayo bado upinzani una nguvu.
Tambueni kuwa watanzania wasasa wana uelewa mkubwa mno, hawana imani kabisa na jinsi mnavyochukua wapinzani, wengi wanaamini ni mchezo mchafu mnacheza kwani hawaoni sababu ya nyinyi kupendwa kiasi hicho.

MWISHO KABISA
WAPINZANI msirudi nyuma kwani hizi ni dalili kuwa mnawaumiza kiasi cha kutosha kuwafanya wasichague jema wala baya, hapa ndio pa kukazia uzi hata kama msikie viongozi wengi kiasi gani wanafika bei! CHADEMA na UPINZANI ni itikadi ambayo kamwe haitoondoka kwenye mioyo ya watanzania katika wakati ambao CCM BADO IKO MADARAKANI!

BADO WENGINE WATAHAMA!

si kwa kujifariji huku, duh!! unaandika risala zile za chipukizi enzi za nyerere!!

imeuma, unatulia, unaangalia mbele, na kuwa wapi umekosea! sasa huo uzito wa chadema kama wote wataenda CCM chadema itabakiwa na nini? kama wote wanaenda kwa sababu wanapewa hela, ccm ndio wenye serikali ndio wenye dola, ndio wenye hela!! unasema kwa tusitegemee mabadiliko kwa hivi vyama??
 
Soma vizuri, ha yo unayouliza majibu yake yapo ndani ya Uzi tayari
 
Back
Top Bottom