Nanyaro Ephata
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 1,221
- 1,788
Nimeandika mara kadhaa kuwa ccm ni marehemu,kuwa chama kinachoitwa ccm ni mfu kilikufa ikazikwa,hakipo.Tunajua kuwa chama cha siasa ni imani(itikadi) leo wanaccm hawajui imani yao maana haipo na haipo kwa kuwa chama kimekufa!
Bahati mbaya ccm wanafikiri watafufuka kwa kuiua CHADEMA,yaani kipaumbele cha wanaccm ni kuiua CHADEMA,wakati Taifa letu linakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi,kisiasa na kijamii,wakati tunapata uhuru Mwl Nyerere alitangaza maadui wa Taifa kuwa ni Ujinga,maradhi na Umaskini,maadui hawa wangalipo miaka zaidi ya 50 ya uhuru! Kilichokufa hakiwezi kamwe kuua kilicho hai
Nguvu kubwa ambayo inatumiwa na serikali kupambana na CHADEMA ingetumiwa hata robo yake tu kupambana na ujinga,maradhi na umasikini hakika nchi yetu ingepiga hatua kubwa mbele! Na kama CHADEMA ni dhaifu kwa nini nguvu kubwa inatumika kupambana na chama dhaifu?pamoja na masahibu makubwa wanayopitia viongozi wa chama na wanachama wetu nchi nzima bado fikra za mabadiliko zimeendelea kukua!hii mbegu ya mabadiliko ndani ya Watanzania haiwezi kufutwa au kuuwawa na yeyote yule
*Mabadiliko ni lazima na chadema ndio njia ya mabadiliko*
Ni aibu kubwa kwa watawala kuwa wanapoteza rasilimali kubwa,wameshindwa kusoma alama za nyakati,wanajidanganya kuwa wataweza kuzuia nguvu ya mabadiliko,bahati mbaya wanaamka kipindi ambacho tayari mbegu imeshaota,mbegu imeenea nchini kote,kuanzia mijini na vijijini kamwe hakuna awezaye kuzuia!
Hata sasa watashindwa kama walivoshindwa huko nyuma,propaganda kuwa CHADEMA ni chama cha Kaskazini ilishindwa..Propaganda kuwa ni chama cha Kikanda ilishindwa vibaya sana,na nyingine nyingi hata sasa watashindwa tena kwa kuwa CHADEMA tulianza na Mungu,tunaendelea na Mungu na Tutamaliza na Mungu.Mungu wetu ni mkuu asiyefananishwa na lolote,Mungu mwenye wivu mwingi! Kwamba mgombea wa CHADEMA hatotangazwa tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1994 huko Kigoma hadi leo hakuna mgombea wa upinzani aliyetangazwa kwa hisani ya ccm na mawakala wao!tumeshinda kwa kuwa tulitumia peoples power ambayo ndio falsafa yetu kuu
Wakati Goliati akimtazama kijana mdogo Daudi kwa dharau kubwa,kwa upande wa Daud aliona ukubwa wa Goliati kama fursa kubwa ya urahisi wa kulenga shabaha!
We have God we have the power
Nanyaro EJ
Mwenyekiti-Arusha Mjini