CHADEMA ni washindi katika hili

Mbogo nyeusi

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
233
540
Nimesikia Mwanza viongozi wa chadema wakiongozwa na freeman Mbowe wamekamatwa saa nane za usiku na jeshi la police,

Ukweli ni kwamba jeshi la police na serikali wanashindwa kujua kwa kufanya vile lawama zinaenda kwa mama kuonekana anaendeleza yale tuliyo zoea kwa mwenda zake hivyo kutojitenga na huo udhalimu kwa sababu ccm wao wanazunguka nchi nzima wakisema wanakagua utekelezaji wa ilani na wanafanya mikutano ya hadhara,huu ni mwendelezo wa ukandamizaji wa demokrasia mama nakuomba ujitenge washauri wako wanakudanganya Kama hilo la miamala ya ccm.

Mama hiyo ni hofu tu,unakumbuka maneno ya baba wa taifa kwa mrema mwaka 1995 kuhusu ghari kusukumwa na kubebwa? Police walikuwa wanfanya haya haya ya unyanyasaji bila kujua wanampaisha mrema na Mwl alivyo ona mbali alipiga stop jeshi la police kuingilia kazi za kisiasa za Mrema ghafla graph ya mrema ikashuka ule ufalme ukayeyuka.

Lipo kongamano lilifanyika majuzi segerea ukweli ni kwamba watu wasio wa mtandaoni hawakujua kinacho endelea na mpaka sasa watu hawajui na hawakumbuki kilicho jadiliwa tupo busy na maisha yetu,

Unajua hawa chadema wangeruhusiwa kufanya hako kakongamano kao jumamosi iliyopita jeshi la police lisingekuwa linahangaika na hii kamata kamata yao ya usiku wa manane kwa watu ambao wamelala
Na isitoshi sisi wananchi tunaufahamu juu ya ukweli wa katiba japo mnatufanya Kama mabwege flani hivi tusio na akili

Nauliza viongozi waliokamatwa usiku wa manane na kupelekwa lockup,ivi wakipelekwa mahakamani watafunguliwa mashtaka gani?

Kwamba wanegomea agizo la mkuu wa mkuoa au wamefanya mkusanyiko bila kibali?ikiwa wamekatwa usiku wa manane wakiwa wamelala?

Mama ushauri mwingine siyo mzuri rejea tozo za simu ulivyo kuchafua akili za kuambiwa changanya na zako
 
Wingi wetu na umoja wetu ndiyo iliyo silaha na ngao yetu ya matangamwizi.

Hata wabadili stadiums zote kuwa magereza watachemsha.

Harakati na ziendelee!
 
Hii ni nin? Tunaelekea wap?serikali umeamua kuvunja Sheria ambazo ndizo mwongozo wetu? Kiukweli hatuko salama Tena.
 
Ulichoongea ni sahihi kabisa. Hawa watu wangeachwa wazunguke wanavyotaka, waongee wanavyotaka mwisho wasingepata attention yoyote!

Mbowe baada ya msiba wa Magufuri amezunguka karibu kanda zote! Ameyasema yote ya moyoni yaliyokuwa yanamsibu, leo si maisha yanasonga tu! Wa kwanza kuchoka ni hao hao wafuasi wake

CHADEMA wanashindwa sehemu ndogo sana! Hawana subira! Wahenga walisema subira ya vuta heri na mvumilivu hula mbivu

Rais ameapishwa tu kushika madaraka huku Taifa likiwa kwenye maombolezo, wao kesho yake washaandika barua ya kuomba mwaliko! Sio kwa haraka zile

Mpaka Sasa ni miezi minne tu tangu achukue madaraka lakini wao lawama zimeshakuwa nyingi

Ndani ya miezi hii minne walitaka wawe wameshaonana na Rais, katiba mpya iwe imeshapatikana, nk.....Kukaa na wapinzani ni jambo jema kabisa lakini mtu mzima halazimishwi kutekeleza jambo

Kwa hali ilivyo Sasa, hata mwaliko walioomba ulishakosa umaalumu tena maana ni Kama imekuwa lazima
 
DC mmoja mjinga mjinga.

wakati mwingine neno linaweza mtoka mtu mzima ukabaki unawaza, anatafufa kick au shida yake ni kitu gani???
 
Rais ameapishwa tu kushika madaraka huku Taifa likiwa kwenye maombolezo, wao kesho yake washaandika barua ya kuomba mwaliko! Sio kwa haraka zile
Rais huyu ana dharau Sana. Yaani anaenda Burundi anaacha kukutana na wanasiasa wenzie?? Tena wamemuandikia barua ya kuomba wakutane naye. Anaenda sokoni Kariakoo kuingilia Mambo ya uongozi anaacha kukutana na chadema??
 
Rais ameapishwa tu kushika madaraka huku Taifa likiwa kwenye maombolezo, wao kesho yake washaandika barua ya kuomba mwaliko! Sio kwa haraka zile
Rais huyu ana dharau Sana. Yaani anaenda Burundi anaacha kukutana na wanasiasa wenzie? Tena wamemuandikia barua ya kuomba wakutane naye.

Anaenda sokoni Kariakoo kuingilia Mambo ya uongozi anaacha kukutana na chadema??
 
Back
Top Bottom