The Giantist
JF-Expert Member
- Dec 12, 2018
- 214
- 86
Habarini tena ndugu zangu wanabodi... Baada ya kuwaeleza kuwa TANZANIA KAMA ULAYA INAWEZEKANA leo asubuhi hapa hapa kwenye jukwaa letu hili pendwa. Nimerudi tena kuja kuwaeleza mambo mengine mawili matatu yanayotuhusu sisi sote moja kwa moja.
Ninayeandika sasa, ni mimi Sauti ya Mdodomia Giantist, ni mwanachama wa Chama Cha siasa Cha Mapinduzi (CCM). Wajibu wangu ni kwa nchi yangu, vilevile nitakuwa mzalendo kwa ajili ya nchi yangu. Kwa hiyo, sitakaa kimya kuzungumza yale mazuri ambayo serikali yetu chini ya usimamizi wa ilani ya CCM na uongozi madhubuti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli, ambayo yamekuwa yakitekelezwa kwa ajili ya kukuza maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi pamoja na nchi yetu kwa ujumla. Kwa kuwa nimekuwa na haki ya kuipongeza serikali yangu kwa upande mmoja, hivyo basi ninayohaki hiyo hiyo ya kukemea utovu wo wote au mpango wo wote ambao una nia ya kuwadhohofisha watanzania na kuidhohofisha Tanzania.
Leo nimekuja mbele yenu kwa kusudi maalum la kuwakemea watu wachache ambao kwa hakika kabisa wanaongozwa na nia ovu kwa ustawi wa nchi yetu. Lakini pia ni waongo waongo, ukipata kuzisikiliza sera zao baadhi walizozieleza kwa ufupi ni dhahiri kuwa haziwezi kutekelezeka katika uhalisia. Si wengine ni jamaa hawa wa mtaa wa UFIPA. Tumewasikia jana wakitupigia kelele kwenye mitandao ya kijamii humu, mara Dodoma kutafurika... Mara on my way to Dodoma kumsindikiza Muujiza.... Mara tumekodi mausafiri ya kutosha n.k n.k kwa kweli zilikuwa ni kilele tena si kidogo.
Hata hivyo mambo yameenda tofauti sana, mji wa Dodoma umetulia sana siku hii ya leo, mara baada ya kutikiswa siku ya juzi wakati wa uchukuaji wa fomu pale Njedengwa ofisi za NEC alipokuwa ameenda mhe. Rais Magufuli na makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu. Wanadodoma wanaendelea na kazi zao za uzalishaji mali kama kawaida, hakuna cha kelele za Lisu wale ni yeye wala cha pipozi! Hakika ni shwari, na kwa kweli muujiza wao ulienda fofofo kuchukua fomu yake ya kushiriki uchaguzi.
Lakini pia, katika kuyaeleza mambo hayo. Swali langu la msingi linaenda kwa VIFIPA. Wanawezaje kukubali kufanywa kondoo wa sadaka kwa kutumika kuwatajilisha mabwana zao wakuu wa Chama?! Huo ulimbukeni wameutoa wapi. Maana hao mabwana zenu wanapokea pesa za ruzuku, na ni ukweli usiopingika katika vyama vya siasa nje ya CCM, Chama chenye kupata walau ruzuku ya kuridhisha ni Chama chenu CHADEMA. Lakini kwa hakika hatuoni kama hizo ruzuku zinakifaa Chama na wanachama. Mnaangaika kukipigania Chama kwa mateso huku viongozi mabwana zenu wanawang'on'ga visogo vyenu kwa kuwaita makamanda! Ni aibu kwa kweli na ni fedheha.
Muda umefika sasa wa kuacha kutumika kama misukule ya kisiasa ndani ya Chama chenu. Muamke muache ujinga huo. Na huyo jamaa yenu, ameshanuia kuwatoa kafara wakati wa uchaguzi kwa kuwachochea mfanye vurugu, ili mvunje sheria muwajibishwe na kisha yeye awaache mataa, na atafanya hivyo ili atimize matakwa yake binafsi na ya mabwana zenu wa CHADEMA wakina Mbowe. Nasema haya katika ukweli mchungu ambao hamutaki kuusikia abadani.
Leo nimeliona gari la CHADEMA lilojifanya linaeneza sera za CHADEMA, hapa Dodoma Mjini. Gari lile no bovu kabisa kabisa. Nikawa najiuliza pesa za ruzuku ambazo ni Kodi ya wananchi CHADEMA wanazipeleka wapi, wanakosa kuwa na magari safi na ya uhakika! Nikazidi kupata hofu, kama wanashindwa kujisimamia wenyewe na mapato yao ya ruzuku wataweza kusimamia pesa za wananchi wakishachukua serikali?! Au kama wanakosa mipango mikakati katika kuratibu mambo yao wenyewe, wataweza kweli kuweka mipango yenye tija katika kuratibu mambo ya nchi?! Sijui walikuwa wanaenda wapi.... Lakini kutoka na ukosefu wa mipango ni dhahiri walishachelewa huko aalipokuwa wanaenda. Maana walitumia zaidi ya dakika 30 wakitengeneza kimeo Chao, maeneo ya Posta Dodoma, Arusha road.
Kwa tabia ya uroho wa fedha wa viongozi wa CHADEMA, kujilimbikizia mamlaka kwa watu fulani fulani, tabia ya kupenda kuwafanya wanachama wao kama misukule, tabia ya kukosa mipango madhubuti ili kuhakikisha hakuna muda unaopotea ili kufikia malengo, tabia ya viongozi wao kupenda kuwatoa wanachama wao kafara ili wapate heshima na umaarufu n.k ndio tabia mbaya ambayo wananchi wameshaifahamu na wameigundua ipo ndani ya CHADEMA na viongozi wake. Na kwa sababu hiyo, CHADEMA hawatakaa kuja kuongoza katika matokeo ya kura hata kuongoza dola na serikali. Maana ni dhahiri kuwa ikiwa wakashika mamlaka na madaraka ya nchi, hawatashindwa kujimilikisha hazina ya serikali, kuwalaghai wananchi kama ambavyo wamekuwa wanawalaghai wanachama wao, hawashindwi kutuuza hawa kama nchi kwa ajili ya maslahi yao binafsi. CHADEMA ni waroho tu, chini ya viongozi waroho!
CHADEMA ni Sumu kwa nchi, ambayo wananchi wasithubutu kuionja hata, inaua. Ni ya kutupilia mbali na kuifukia chini kabisa, isionekane tena katika siasa za nchi hii. Muda umefika sasa, wa wananchi kwenda kuikataa waziwazi kwenye sanduku la kura.
Karibuni Dodoma, tusherehekee siku kuu ya nananane hapa viwanja vya nanenane Nzuguni. Hakuna watu wa ufipa wala magari ya ufipa. Magari yao yameenda gereji huko, vingi vimeo!
Sauti ya Mdodomia
08/08/2020