CHADEMA ni kama CCM..,ama mbaya kuliko CCM...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA ni kama CCM..,ama mbaya kuliko CCM...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TandaleOne, Nov 10, 2011.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Mwaka 2010 tulishuhudia matukio mengi yakijiri ndani ya taifa letu, ni matukio yaliyonasibishwa na siasa na kukua kwa demokrasia.,kulingana na muundo na mitindo ya utokeaji wake wengi tuliamini kuwa siasa katika Tanzania imepata muamko mpya na inashika hatamu katika kuleta mabadiliko ya kinchi katika Nyanja zote ambako siasa inagusa ama inahusika moja kwa moja, hapa nikijumuisha uchumi, tamaduni na jamii.

  Katika matukio, lipo moja lilikuwa very significant and relative to what I am writing today.,nalo ni kukua na kutanuka kwa CDM mpaka kufikia kuwa chama kikubwa cha upinzani chenye mikiki na mabavu tele tena shupavu mbele ya CCM.,kushindwa na kufanikiwa kwake.

  Kukua kwa chama hiki hakujatokea ghafla ama kwa bahati nasibu ni kwa kuwa kulikuwapo na mipango thabiti tena ya muda mrefu ya kuhakikisha chama hiki kinakua na kufikia malengo yake ya kuchukua nchi na kutawala dola. Kwa kuwa lengo langu si kuelezea historia ya kukua kwa CDM sitaingia ndani katika kulieleza hili.

  Lengo kuu la waraka huu ni kueleza kupoteza kwangu matumaini na hamu ya kuwa shabiki wa siasa za Tanzania na imani yangu kuwa Siasa na wanasiasa wetu wanao uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya jamii ya watanzania ambao wapo katika dimbwi la umasikini na dhiki kuu.

  Kutokana na propaganda zilizopenyeshwa na kukubalika katika vichwa vya wengi ni kuwa hali ngumu ya maisha ya watanzania imeletwa na uongozi mbaya wa serikali ya CCM, ambayo wizi, ujambazi, uporaji, ufisadi, rushwa, elimu isiyo na tija(hafifu), uongozi wa kupeana (unprofessionalism) njaa,magonjwa,miundombinu hafifu,na mengineyo yameonekana kutawala.

  Kwa kiasi kikubwa kama si kwa asilimia zote nilikubaliana na hili, na nikawa attentive, makini na kujiaminisha kuwa hawa wanao address matatizo haya wanakuja na mbinu mbadala na mawazo tatuzi katika kushughulikia hali hii, na si mimi pekee bali watanzania walio wengi hasa wa mijini tuliamini hivyo.

  Kushindwa kwa CDM;

  Kulingana na yanayoendelea hivi sasa ndani ya CDM kikiwa kama chama kikubwa cha upinzani kunaonyesha dhairi kushindwa kwake katika kufikiri juu ya njia sahihi na mbinu piganizi katika kuyashughulikia matatizo yanayowakabili watanzania kiuchumi, kiutawala, pamoja na kijamii.
  Na nitayazungumza machache na kwa mifano ili watu wapate kuelewa kiunaga ubaga

  1: Katika ufisadi, CDM haijaonesha mipango thabiti juu ya kulishughulikia suala la ufisadi nchini zaidi ya kuitisha maandamano ya kupinga kulipwa mafisadi ambao wanabebwa na mahakama, hili linaonyesha ni kwa kiasi gani hakuna mipango thabiti,ya muda mrefu na endelevu juu ya kuzuia miaya ya rushwa.

  Hali zinazopelekea rushwa na hata kutoa direction ya adhabu na kanuni zinazosimamia utekelezaji wa mikakati hiyo ya kupambana na rushwa bali tumeona kuwa wapo viongozi katika CDM ambao wanapropagate ufisadi katika nafasi zao ndogo walizonazo hali inayotoa ishara ni kwa kiasi gani wanaweza kuwa pindi wakipata nafasi kubwa, kumbuka ya Mshahara wa Dk Slaa, kumbuka Magari ya Mbowe, kumbuka ukwepaji wa kodi wa chama, yale ya diwani kule Mara, n.k

  2: Katika nchi ambayo demokrasia ni msingi na daraja la kuendea utawala wa sheria, wananchi (wapiga kura) lazima wawe na ufahamu wa kutosha juu ya maamuzi wanayotakiwa kuyachukua pindi wanapotumia fursa yao ya kupiga kura, Katika hili CDM wamekuwa mbele kulalamika na kupinga matokeo bila kufanya study yakinifu juu ya uhalisia wa wapiga kura Tanzania, wakiwa wanatumia sample space ambayo ni irrelevant kwa wakazi wa mijini na watumiaji wa mitandao katika kufanya tathmini zao za ushindi ama kushindwa.

  Katika uchaguzi mkuu uliopita na zingine ndogondogo tathmini za kwenye mitandao zilionyesha kuwa CDM itashinda kwa kishindo na matokeo yamekuja tofauti mara zote katika chaguzi zote, na ni baada ya matokeo ndipo CDM hukakamaa na kunadi kuibiwa kura baada ya kutulia na kujifanyia tathmini yakinifu. UKWELI NI KUWA..

  Wapiga kura walio wengi ni watu wa vijijini ambao wengi katika wao ni masikini wa kutupwa , kulingana na ripoti ya benki ya dunia iliyotolewa October mwaka huu ni kuwa asilimia 83 ya masikini huishi vijijini,ambao katika hao milioni 6.4 wanaishi katika mstari wa umasikini wa kukosa chakula, milioni 10 wanakabiliwa na kukosa chakula kwa msimu-kwa maana wanakuwa nacho kipindi cha mavuno na kabla ya kipindi cha masika kinawaishia.

  Wengine milioni 12.7 hawapati mahitaji yao ya msingi, hii ikimaanisha kuwa zaidi ya watanzania milioni 30 wanaishi katika umasikini wa kutupwa idadi ambayo ni kubwa maradufu ukulinganisha na hapo nyuma na ni idadi inaonyesha kukua kwa umasikini na kufilisika kwa serikali inayotakiwa kuwahudumia watu hawa.

  Katika hali kama hiyo watu hawa lazima watadanganyika kwa kupikiwa wali, kupewa t-shirt na kofia lakini pia watanunulika kwa bei rahisi sana, hali inayowawezesha viongozi wasio na nia ya kweli ya kuwaletea maendeleo kujipenyeza kwa urahisi na kupata uongozi, wakati hali iko hiovi huko vijijini CDM wao wako busy ARUSHA wakiandamana na kulala nje, mambo ambayo hayana mashiko yeyote wala sababu za msingi.

  Lakini kama hayo hayatoshi, ni kuwa wakati serikali ikishindwa kusimamia fedha na miradi inayoelekezwa katika maeneo ya vijijini CDM inashindwa kuweka mkakati wa ufuatiliaji na taasisi ya kuhoji matumizi na utekelezaji ( hili linawezekana kisheria) ambapo kupitia taasisi hiyo usimamizi utaimarika lakini pia wapiga kura watapata mrejesho na kushuhudia nia ya kweli ya wanasiasa wao ya kuwaletea maendeleo.

  3:Kulingana na mfumo wa sasa wa kiuchumi wa soko holela ambapo wenye nacho hupata fursa ya kujitajirisha zaidi kwa kupitia migongo ya walalahoi, CDM inayofursa ya kutoa muelekeo wa uchumi na mfumo unaojali na kugusa pande zote kwa kushauriana na wachumi walionao na kuandaa proposal ya sera zenye kulenga mabadiliko chanya kwenye sekta ya fedha,kodi, biashara, mishahara,na miamala mbalimbali katika sekta tofauti za kiuchumi hususani kilimo, ambapo watanzania walio wengi wamejiajiri huko. Na hili lazima lifanyike chini ya wataalamu wa uchumi na fedha.

  4: katika mambo yanayopigiwa kelele katika uongozi chini ya serikali ya CCM ni undugunization katika ajira na mgawanyo wa vyeo na madaraka, katika hili CDM tuliamini watakuja na mbinu tofauti ya kuhakikisha kuwa vyeo na madaraja ya kazi yanagawanywa kulingana na uwezo, elimu na nafasi ya mtu,lakini tofauti na matarajio ya wengi bado ipo system ya kulimbikiziana vyeo ndani ya CDM, watu kama mnyika na wengineo wanavyo vyeo zaidi ya vitatu wakati mmoja kana kwamba hakuna vijana wengine katika CDM walio na uwezo na elimu ya kushika nafasi hizo.

  5: kupoteza umaarufu na kushindwa ushawishi kwa jamii. Hivi sasa kwa mtu aliye makini na siasa za ndani ya nchi, anaweza kugundua kwa urahisi kuwa CDM wamepoteza umaarufu na ushawishi kwa watanzania, umaarufu ambao ulipatikana kwa gharama kubwa na akili nyingi, hii inatokana na kupoteza uelekeo kwa media outlet zinazotumiwa na chadema, mfano wa magazeti kama mwanahalisi, mtanzania.

  Tanzania daima,mwananchi, the citizen na social medias kama jamii forums ambazo kwa mara ya kwanza zilikuwa na mvuto mkubwa kwa watanzania wapenda habari lakini kutokana na kuandika kwa mlengwa mmoja na kwa muda mrefu bila kubadilika zimepoteza ladha na thamani yake kwa watanzania.

  6: Migogoro ndani ya chama.,CDM kikiwa chama kilichojitokeza mbele ya watanzania kama chama cha wapenda mabadiliko, wapenda vijana na wanaharakati wa kweli wenye kutaka Tanzania yenye neema ipatikane, bahati mbaya CDM kimekuwa kikijiingiza ndani ya migogoro ya mara kwa mara tena kwa viongozi wake wa ngazi za juu.

  Ili linatokana na ukweli kuwa wapo wapenda madaraka wasiotaka kupisha wenzi wao na hasa vijana katika nafasi nafasi za kiutawala ndani ya chama, wenye kutaka kutoa kauli za mwisho zisizopingwa wala kukosolewa.,hali hii inatia mashaka kwa watanzania walio wengi hivyo kupoteza ari na hamasa katika kukipenda na kukiamini CDM.,wengi wakiamini kuwa tofauti pekee ya CDM na CCM ni herufi "D" tu na si vinginevyo.

  Kwa kuhofia kuwachosha wasomaji, nitasitisha hapo na mengine naweza nikayazungumza kama sehemu ya comments, ila kwa kumaliza nitasema kuwa MTANZANIA TAMBUA WAZI KUWA MABADILIKO YANAANZA NA WEWE NA NI JUKUMU LAKO WALA SI LA YULE.,ACHA KULALAMIKA, ACHA KULALA NJE, ACHA KUPIGA MAYOWE.

  CHUKUA HATUA ZA KWELI ZA KULETA MABADILIKO YA KWELI BILA KUFUNGWA KATIKA ITIKADI AMA IMANI. BALI KWA MSUKUMO WA UTANZANIA WAKO NA UTAIFA WAKO.

  MAANDAMANO NI NJIA YA KUFIKISHA UJUMBE LAKINI SI NJIA PEKEE YA KUFIKISHA UJUMBE.,MAANDAMANO PEKEE HAYATUTOI KATIKA UMASIKINI NA KUTUTAJIRISHA BALI UZIDISHA UMASIKINI NI NJIA ILIYOSHINDWA, INAYOSHINDWA NA ITAKAYOSHINDWA TANZANIA…!
   
 2. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Hatuchoki ila nahisi hujafikiri au umefikiri sana ukapitiliza ndo maana unalinganisha mafuta machafu na maji safi.
   
 3. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Kuna jambo moja kubwa ninaloendelea kuliona na kujifunza zaidi kwenye maisha

  "Wanaoongea na kulalamika matatizo bila suluhisho ni wengi kuliko wanaoongea na kuchukua hatua za suluhisho kwa matatizo/mapungufu yaliyopo"

  Atleast 20% ya post yako ndefu ingekuwa imebeba solutions kwa haya unayoainisha kama matatizo ingekuwa na msaada zaidi kuliko ilivyo sasa (simaanishi haina msaada, do not quote me wrong)
   
 4. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Katiba mpya tu jamani na tupate uongozi unaofata sheria baaaaaaaas!!!
   
 5. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hazizuii ng'ombe kunywa maji..tetehhh
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Umesema vema sana, kama vile ulikuwa kwenye kichwa changu. Tatizo la chadema ni kwamba viongozi wanaficha madhambi yao kupitia mwamvuli wa NGUVU YA UMMA. Viongozi wa CDMA wengi wao walikuwa siyo watu wazuri katika jamii, na hili liko wazi, sasa wanaamua kusafisha tabia zao mbaya ambazo watu walizoea kuziona wakiwa nazo.

  Chama hiki kina viongozi ambao wana mali nyingi ambazo zinatokana na kukwepa kulipa kodi, wengine wanajulikana kwa tabia za wizi na tabia nyingine nyingi. Naungana na wewe kwa silimia mia moja kuwa CDM ni chama kibaya sana hasa ukizingatia asili ya maisha ya viongozi wake.
   
 7. m

  mtz flani Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo kuna vijana wanalipwa (haijaishi na nani) kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kutumia muda wao mwingi kuwasifia mabwana zao. hivi kweli dume zima na korodani zako unamsifia mwanaume mwenzio kuwa ndiye atakayemaliza matatizo ya familia yako una akili timamu wewe?

  Jamani nchi iko kwenye matatizo, hebu tuache kutaja watu tutambue matatizo yetu then kwa umoja wetu tutafute suluhisho la kudumu la hayo matatizo. hii akili ya kulala nje kwa ajili ya kumtetea mtu ambaye kwa akili yake timamu ameamua mwenyewe kwenda gerezani sijui kama inaondoa umasikini wetu kama Watanzania. Mbowe, Slaa, Sitta, Lema n.k hao ni wanasiasa wanaotafuta madaraka tusiwaamini sana.

  Najua kuna watu wanalipwa na utawaona wakitukana tu wenzio ambao wana maoni tofauti na wao but anyway, time will tell.
   
 8. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Soma tena kwa makini herufi baada ya herufi, nadhani utagundua kuwa kuna solutions na mapendekezo ya msingi kama yakifanyiwa kazi...!
   
 9. Nani Kasema

  Nani Kasema Senior Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanafiki na propagandist wa Chama cha Mafisadi, Kama Huyu, wanavyo-pretend kuwa ni Wanamageuzi wanaoitakia chadema mema, basi ujue kuwa kiyama kimekaribia
   
 10. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  [h=6]
  "ACHA UKWELI UONGELEWE"
  wakati hali iko namna hii maeneo ya vijijini na kwenye vitongoji ambako maelfu ya watanzania na wapiga kura wanapatikana, ambako huduma za jamii hazifiki, ambako watu wamepoteza matumaini, ambako umasikini umeshamiri bado sisi tupo tukilala nje Arusha tukiamini hilo ndilo suluhisho la watu hawa walioko huku. Ofisi ikiwa katika hali hii inatoa picha kuwa wanachama wako wangapi na wanaari na hamasa kiasi gani, inajulisha ni kwa namna gani watu hawa hawafikiwi na hawathaminiki.


  [/h]
  chadema.jpg
   
 11. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Labda wapumbavu ndio wataona solution kwenye habari yako lakini werevu watasoma na kushangaa..
   
 12. L

  Lua JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  yaani full upupu bora hata ungekaa kimya au hoja hii ungeipeleka kwenye vikao vya ndani vya magamba. Chadema wameshatoa njia mbadala nyingi sana, yaani ndani ya bunge (bajeti mbadala).

  Nje ya bunge kama dr. slaa aliwataja mafisadi (list of shame) wamefanya nini au ulitaka dr. akawa kamate yeye wakati hana dola wala mahakama na mwisho wanakuja kumkamata yeye.

  Ilani ya chadema imetoa njia mbadala ya kupunguza mzigo wa ukali wa maisha kwa wananchi. kupunguza kodi ya vifaa vya ujenzi, kusimamia rasimali za nchi, kuanzisha mamlaka ya kusimamia pension ya wazee na hata wazee kulipwa kila mwezi, kuwa tume huru, kuunda katiba mpya nk.

  So ulikua unataka solution gani, kama viongozi wenyewe wanapewa njia na hawataki kuitumia. (vichwa maji).
   
 13. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ama kweli CCM puppets are now on air. Ngoja tukutoe tongotongo machoni na threads zako zisizo fanyiwa utafiti pamoja na nduguyo maralia sugu.

  1. Dhamira ya dhati ya kupambana na rushwa na ufisadi sio nyimbo za majukwaani, ama machozi bungeni bali ni kwa vitendo. Rushwa ni kosa la jinai ambalo kwa mujibu wa sheria mtuhumiwa hushitakiwa mahakamani na mwendesha mashtaka wa jamii (Public Prosecutor).

  Huyu ni mteule wa Rais aliye madarakani, ingawa anapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa katiba. Katiba haijatoa uhuru kwa mtu mwingine kuendesha kesi za jinai. Tueleze ni kwa namna gani CDM watamwagiza DPP awakamate mafisadi na kuwafungulia mashtaka?

  Kazi ya kushughulikia rushwa, kuanzia kupeleleza, kukamata na kufikisha mtuhumiwa kwa DPP ni ya TAKUKURU na POLISI (Mkurugenzi wa PCCB na IGP ni wateule wa rais na wanawajibika kwa rais), CDM watatumia njia gani na kwa sheria ipi kumwagiza Hosea au Mwema kutafuta ushahidi kuhusu ufisadi, kuwakamata na kuwafungulia mashtaka mafisadi?

  Haiyumkini mahakama zetu pamoja na kuzionesha kama ni vyombo huru, lakini si huru abadani. Jaji Mkuu, Jaji kiongozi na majaji wengine wote ni wateule wa Rais (CCM), mishahara yao na marupurupu inapangwa na serikali, bajeti yao inapangwa na serikali (Celina Kombani), hata kiutendaji ni sehemu ya serikali (Rejea semina elekezi Dodoma na Hotuba toka kwa Jaji mkuu).

  Unategemea CDM wataweza vipi kupambana na ufisadi kwa njia mbadala zaidi ya kushitaki kwa wananchi? Katika mfumo ambao Serikali, Bunge na Mahakama zinafanya kazi kama kitu kimoja (Mapacha watatu, baba mmoja CCM), unategemea kundi la wananchi na asasi nyingine watapata wapi haki zao wanazoamini zimenyang'anywa?

  2. CDM haijapinga matokeo bila kufanya study kama unavyotaka Dunia iamini. Wana ushahidi wa wazi na waliutoa, lakini CDM ni chama cha wapenda amani kupita kiasi, ndio sababu hawakutaka kuingia barabarani kuandamani kupinga kuporwa ushindi wao. Na kwa kukupa ushahidi dhahiri si tume ya uchaguzi wala CCM ama JK waliokanusha madai ya CDM. Na mpaka leo tume ya uchaguzi haijatoa matokeo kamili ya kura za urais (Tembelea tovuti yao uone).

  3. Nadhani hujui unachokiongea unakurupuka tuu. Mwelekeo wa uchumi wa nchi hautolewi na vyama vya siasa ama asasi za kiraia. Mwelekeo wa uchumi wa nchi hutolewa na serikali iliyo madarakani kupitia tume za mipango, wizara ya fedha, Benki kuu na vyombo vingine vya kifedha kama TRA. Hivi ni chombo gani kati ya hivi CDM wanaweza kuvitumia kutoa mwelekeo wa uchumi?

  Dunia nzima kushindwa kwa uchumi wa nchi ni kushindwa kwa serikali iliyo madarakani. Jamani, muwe mnaangalia hata TV, fuatilia yanayoendelea sasa Ugiriki, Uturuki japo ufunguke akili kidogo. Na kudorora kwa uchumi wa Tanzania ni matokeo ya kushindwa kwa serikali ya JK na si visingizio vingine.

  4. Suala la undugunisation fanya utafiti usikurupuke.

  5. Thread yako haijafanyiwa utafiti, kwa wakati huu CDM ndicho chama kinachoungwa mkono na watanzania wengi zaidi kuliko chama chochote cha siasa. Tafiti za sasa zinaonyesha wazi, na matokeo ya Igunga ni sehemu ya ushahidi tosha. Licha ya CCM kununua shahada, kugawa pesa, kupeleka viongozi wake wote wanaoungwa mkono na watanzania wengi, wamerudisha jimbo kwa tofauti ya kura 3000, CDM imenyang'anya kura za CUF 9000, CCM 9000 na kupata nyingine 4000.

  Na hii ni tishio kwa CCM ndio maana hawaishi kutisha watu na kubambikiza kesi viongozi wa CDM. Ikiwemo hii ya kizushi kabisa ya Mh. Lema.

  6. Siasa ni propaganda, lakini hii yako ni unafiki uliokithiri. CDM wana mgogoro gani? Vipi dhana ya kuvuana magamba na kukatazana kutangaza nia ya kugombea urais? Vipi makundi yanayotafunana ndani ya CCM?

  Umesahau mkutano wa wenyeviti na makatibu wa mikoa ulivyoisha kwa kuwa na misimamo inayosigana (Kundi la Makongoro na la Mwenyekiti wa mkoa wa DSM?), kauli ya Sita kuhusu kuenguliwa uspika kwamba ni njama za mafisadi? Je, uamuzi wa chama chenu ulitoka kwa mafisadi?

  Vipi kuhusu CCJ vs Magamba? Mgogoro ndani ya CCM ni wa maangamizi, CDM hawana mgogoro wowote ila CCM wanajaribu kuipandikiza bila mafanikio. Wanaweza kufanikiwa kuisambaratisha NCCR na si chama makini CDM.

  PUNGUZA UNAZI JADILI HOJA ZA KWELI NDUGU.[/
   
 14. p

  politiki JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  KATIKA MAKALA YAKO NZIMA UMESHINDWA KUELEZEA HOW CHADEMA IS WORSE THAN CCM. CDM ni chama kichanga ukifafanisha na ccm ambayo imekuwa miaka mingi na pamoja na kuwa na serikali na polisi bado imeshindwa kupambana na ufisadi?

  CHADEMA haina serikali wanachoweza kukifanya ni ku point out ufisadi ulipo kitu ambacho wamekuwa wakifanya kila kukicha. kuhusu kuwwafikia wananchi vijijini hilo ni suala la economics zaidi kuliko mikakati kwani hata kama una mipango lakini kama huna means ya kuweza kuitekeleza ni sawa na bure.

  CDM hakuna mgogoro, ni watu wanatofautiana hoja na hiyo ni lazima kwenye demokrsia lazima iwepo misuguano kwani watu wote hamuwezi kuwa na mawazo sawa.

  HITIMISHO.
  CDM ni chama kinachokua kwahiyo kufanya makosa ni kitu cha kawaida cha msingi ni kujifunza kutokana na makosa yako.
   
 15. C

  CUFv2.0 New Member

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CDM mmekwisha. Mshaharibu sana, sasa hivi mnatumia desperate Measures. You are done!
   
 16. C

  CUFv2.0 New Member

  #16
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah! Maskini wee! Mtizameni mwenzenu huyu, kabaki kujustify makosa sasa. Kakubali yote, ila katoa sababu, kwamba Chama bado kichanga. Baasi waambie viongozi wenu, kuongoza matawi ya chama hali ndo hio, jee kuongoza mikoa! Haya komaeni!
   
 17. m

  mtolewa Senior Member

  #17
  Nov 10, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuwa na maoni totauti ndo demokrasia yenyewe,lakini kudai watu wasikilize maoni ya kijinga kama yako na hata wewe mwenyewe ukijua kuwa maoni hayo ni ama ya kijinga ama yana nia mbaya na kupotosha makusudi kama wewe na tandale mfanyavyo, huo utakuwa UPUMBAVU.

  MWL alituasa kuwa mtu akikushauri jambo la kijinga na wewe ujaua ni la kijinga halafu ukakubali,mtu huyo atakuona zuzu. Mimi najua kuwa nafsi zenu zinawasuta na ndio maana watu kama nyinyi na mafisadi wenzenu hamuwezi kusimama kifua mbele mbele ya vyombo vya haki kama vile mahakama huru,au mjadala wa wazi na hadhara na mkatetea hoja zenu hizi. uzuri watanzania wote na hata wasio watanzania wanajua ni akina nani wanatetea maslahi ya watanzania.

  Na ukitaka kuwajua utawaona wakisakamwana kunyanyaswa na vyombo vya ukandamizaji kama vile polisi na mahakama kwa uchache.aidha hii si kwa nchi yetu tubali huwapata wale wote wanaodai mabadiliko yaani majina yao ni kama panya,wasaliti,wenye uchu na madaraka,wavunja amani na utulivu n.k.mara nyingi hulala mahabusu na magerezani na mahakamani kwao huwa kama vile nyumba za ibadayaaani angalau mara moja kwa wiki.

  kwa taarifa yako kila mahali bendera ya CDM inapopea hutoa utulivu wa moyo na matumaini kuwa Ishallah siku moja tutajikomboa,kila mara watu wanaponyoasha alama ya vidole viwili hupata mori wa kuendeleza mapambano na huburudika mioyoni mwao kuwa FREEDOM IS COMING TOMORROW! NA Hivyo kupata ujasiri wa kuvumilia mateso yoyote yale.

  Kila mara majina na sura za watu kama kamanda MBOWE,SLAA, LISSU, BAREGU, LEMA, MNYIKA, MDEE, WENJE, ZITTO, SILINDE NA Wapambanaji wote wale hata nje ya CDM wanapoonwa au kutajwa huleta msisimko na shukrani kwa Mungu kwamba tunao watu wa kututangulia katika vita hivi na kwamba kwa mapenzi ya Maulana.

  TUTASHINDA.
   
 18. Lawkeys

  Lawkeys JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 1,110
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwa heshima zote, kwa moyo wangu wote na akili zangu zote, naunga mkono hoja zako.

  Mimi pia ni mmoja ya watu waliokuwa disappointed na CDM, CDM are turning out to be traitors of innocent men and women of Tanzania tuliokuwa tumetoa trust yetu kwa CDM.

  Kama CDM watazingatia ulichokiandika watalinda heshima ya chama na kujirejeshea imani ya watanzania. Wakipuuza wana options mbili:

  1. Kufa
  2. Au kusababisha kumwagika damu ya watanzania wasiokuwa na hatia. Au kumissuse trust ya watu waliotoa mioyo yao kwa CDM


   
 19. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Nani kasema..???
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nadhani ni wewe na wale wa aina yako ambao wanadhani/unadhani mko kati ya great thinkers kumbe mnashusha hadhi ya JF
   
Loading...