tunduruboy
JF-Expert Member
- Mar 16, 2013
- 423
- 218
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeilalamikiaTume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwamba ina mikakati ya kuvuruga uchaguzi mdogowa madiwani na ubunge unaotarajiwa kufanyika Juni 16, mwaka huu. Uchaguzi huoutahusisha kata 26.
Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, MsafiriMtemelwa, aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake kwamba Wakurugenziwa baadhi ya Halmashauri ambao ndiyo wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya NEC,hawajatoa ratiba ya uchaguzi huo kiofisi.
Alisema fomu za kuomba kuwania nafasi hizo zimefichwa nakatika maeneo mengine zinatolewa kwa siri katika baadhi ya Halmashauri hususaniya Babati na Singida, jambo linaloashiria mchezo mbaya unaofanywa na NEC.
Alitoa mfano kwamba, Singida fomu zimeanza kutolewa mwishonimwa wiki siku ambayo siyo ya kazi kiserikali hivyo kuathiri utaratibu mwingineambao mgombea anapaswa kuufuata ikiwamo kuapa mahakamani.
"Hali si nzuri katika uchaguzi, kuna kiwingu cha kutakakuuvuruga, kuna rafu na hila, tumewasilisha malalamiko haya NEC hivyo tunaiombaiyafanyie kazi ili kuondoa hii hali," alisema.
Akijibu tuhuma hizo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, JuliusMalaba, alieleza kutofahamu taarifa hizo kwa kuwa alikuwa kwenye kikao nakumtaka mwandishi wa gazeti hili kufika ofisini kwake leo kwa ufafanuzi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Babati,Dominick Kweka, alikataa kuzungumzia malalamiko hayo kwa madai kwamba hawezikuzungumza na mwandishi wa habari asiyemfahamu kwenye simu, wakati Mkurugenziwa Halmashauri ya Singida, E. Mwenda, simuyake haikuwa inapatikana.
Wakati huo huo, Mtemelwa amesema CHADEMA inajipanga kwaajili ya kunyakua jimbo la Sumbawanga Mjini mwaka 2015, baada ya Mahakama yaRufani kumtangaza mbunge wa jimbo hilo(CCM), Hilaly Aeshi, kuwa mbunge halali.
source: chademablog