CHADEMA ndani ya vita ya kuamua heshima au maslahi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,399
Katiba ya Tanzania ibara ya 66 (1), inaelekeza kuwa lazima kuwepo wabunge wanawake asilimia 30 ya wabunge wote wa makundi mengine. Makundi mengine ni wabunge wa kuchaguliwa (ambao mwaka huu jumla ni 264), wabunge 10 wa kuteuliwa na Rais, wabunge watano wa kutoka Baraza la Wawakilishi, pia wanne ni Spika wa Bunge kama si mbunge.

Katiba ibara ya 78, inatoa mwongozo wa mgawanyo wa asilimia 30 za viti maalumu kuwa kila chama kitakachofikisha asilimia 5 na kuendelea ya kura za ubunge, kitapata mgawanyo wa viti maalumu.

Hata hivyo, katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni, Chadema kilifikisha asilimia zaidi ya 18, wakati CCM wana zaidi ya asilimia 70.

Kwa kifupi, ni CCM na Chadema pekee wenye hadhi ya kutoa wabunge wa viti maalumu katika Bunge hili la 12. Sasa, kwa masharti yaliyopo kwenye Katiba, Chadema si kwamba wanapewa viti maalum, bali ni mali yao.

Walipewa na wananchi kupitia kura. Ni vizuri kulieleza hili kinagaubaga ili watu wafahamu. Kuna watu wanadhani ni viti vya huruma kutoka serikalini, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wala CCM.

Hivyo, wakati mjadala huu wa viti maalum ukiendelea, inapaswa ifahamike hivyo kuwa vile viti 19 maalumu ambavyo ndiyo mgao wao kama ilivyokokotolewa na NEC, ni haki yao. Walipewa na wananchi. Si vya msaada wala mgawo wa huruma. Chadema watambue hivyo, kadhalika CCM na watu wengine wote.

Hili lipo mpaka Zanzibar. Chama cha ACT-Wazalendo kina hadhi ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kupendekeza jina la Makamu wa Kwanza wa Rais. Ni haki yao kwa sababu ya kura walizopata. Wazanzibari waliamua kutokana na mgawanyo wa kura kwamba CCM na ACT-Wazalendo waingie ubia wa kuendesha serikali yao kwa mwaka 2020-2020.

Kwa mujibu wa Ibara ya 39 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, uteuzi wa Makamu wa Kwanza wa Rais kutoka chama kilichoshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa Rais, si hiari kwa Rais aliyeshinda, bali ni lazima pale mshindi wa pili anapopata kura za urais asilimia 10 au zaidi.

Katika matokeo ya urais Zanzibar yaliyotangazwa Oktoba 29, mwaka huu, Maalim Seif Sharif Hamad, aliyegombea urais kupitia ACT-Wazalendo, alipata asilimia 19.87, ambayo ni karibu mara mbili ya asilimia zinazohitajika ili chama kilicho nafasi ya pili kitoe Makamu wa Kwanza wa Rais na kushiriki kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Ibara hiyo, inaeleza bila kutaja idadi kuwa kama mshindi wa kiti cha urais hakuwa na mpinzani, basi Makamu wa Kwanza wa Rais atapatikana kupitia chama kitachoshika nafasi ya pili kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Hadi sasa, kabla ya kupitisha majina ya viti maalum, CCM wana viti 49 na ACT-Wazalendo kimoja.

Kwa ufafanuzi huo wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010, mantiki yake ni kuwa ACT-Wazalendo ndio wenye kutakiwa kutoa majibu ya mtihani wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, kama wakubali au wakatae. Na kwa mujibu wa Katibu, wanapaswa kuwa na majibu ndani ya siku saba kutoka siku ambayo Dk Hussein Mwinyi alipoapishwa kuwa Rais wa Zanzibar.

Kwa mantiki hiyo, Chadema wanaposusa viti maalum si kwamba wanakataa zawadi, bali wanagomea haki yao ambayo wanaamini imepunjwa. Ni sawa na ACT kugomea Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Hawakatai zawadi, bali wanaona hiyo haki ni ndogo baada ya kuona wamedhulumiwa.

Hoja ni hii; wakiendelea kususa watapata kipi na wakikubali kujiunga watakosa nini? Kati ya mwaka 2015-2020 Cuf walisusa Zanzibar, walipata nini? Tukumbuke, Cuf walimgoma mwaka 2000, na wabunge wao wa Zanzibar walikaa nje ya Bunge kwa takriban mwaka mzima mpaka maridhiano yalipofanyika.

Je, mgomo wa Chadema viti maalum na ACT Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, utapuuzwa kama Cuf walivyopuuzwa bila kupata chochote 2015-2020 au itakaribisha maridhiano kama ya Cuf na CCM mwaka 2001? Chadema kwa kura za ubunge walizopata wanastahili ruzuku. Vipi wakigoma na Serikali ikaamua kusitisha ruzuku kwa sababu wabunge wake hawatumikii Bunge? Kwa siasa zilizopo za kukomoana hili halishindikani. Wakiendelea kugomea viti maalum, haitakuwa na maana na haimaanishi kuwa wakipokea viti hivyo itapunguza uzani wa hoja yao kuwa walidhulumiwa, isipokuwa ni kulinda tu heshima. Ila wakiendelea kugoma yapo masilahi watapoteza.

Mwananchi
 
Hahaha CHADEMA na ACT wameamua kutokutoa viti maalum wapelekeni mahakamani kwa kukiuka takwa la katiba.
 
Kwa kuwa mikutano ya hadhara imepigwa pini, wapinzani wakisusia hizo nafasi watakosa platform ya kuongelea maswala mbalimbali ya chama na ya kitaifa! Nawashauri waende bungeni ili wapate platform ya kuairout dhulma zote walizofanyiwa huko bungeni.
 
I always believe, I should first take what I got, then start a bigger battler in getting your rightful share or beyond.

Hiiya kugoma goma ndo ilitunyina tume huru kwenye katiba mpya. Ingawa tungepata kidogo that time ila kwa kukataa kile kidogo then hatukupati kikubwa tulichokiwaza kukipata wala kidogo tulichostahili kupata.

Negotiation is a skill, the parties should get a hood negotiator/advisor on negotiation.
 
Watu wanaiba kura halafu wanataka wizi ubarikiwe uwe kana kwamba kila kitu kilikuwa sawa tu. Kama kweli mnataka kanuni na sheria zifuate, futeni matokeo ya uchaguzi, serikali ya muda iundwe, na uchaguzi ufanyike upya chini ya tume huru. Vinginevyo ni sawa tu kuliyumbisha taifa na dish kuyumba kila sehemu huko mbeleni.
 
Kwa kuwa mikutano ya hadhara imepigwa pini, wapinzani wakisusia hizo nafasi watakosa platform ya kuongelea maswala mbalimbali ya chama na ya kitaifa! Nawashauri waende bungeni ili wapate platform ya kuairout dhulma zote walizofanyiwa huko bungeni.

Walikuwepo bunge lililopita, ni hoja gani walijadili huko ndani, maana kila siku hotuba zao zilikuwa zinazuiwa au kuhaririwa. Kama wanaenda kufuata hela hapo sawa, lakini sio kwenda na hoja mbadala maana hizo rais hataki, na rais ndio kiongozi wa bunge, na ndio chanzo cha yote haya kwa sasa kwenye siasa zetu. Siku Magufuli akitoka madarakani ndio mifumo itarudi kufanya kazi, ila kwa sasa utashi wake ndio muongozo wa mifumo. Hivyo acheni kuwadanganya cdm kwenda kushiriki bunge la wamwaga damu na wezi wa kura. Hakuna kwenda kushiriki kwenye bunge kibogoyo fullstop.
 
Ukitaka uchaguz wa haki dunia hii utasubir sana mkuu

Id ya 2020, wenzako wanasema uchaguzi ulikuwa wa haki na ccm imeshinda kihalali, ww unajichanganya kwa kukiri ukweli kuwa hakuna uchaguzi wa haki dunia hii!
 
I always believe, I should first take what I got, then start a bigger battler in getting your rightful share or beyond.

Hiiya kugoma goma ndo ilitunyina tume huru kwenye katiba mpya. Ingawa tungepata kidogo that time ila kwa kukataa kile kidogo then hatukupati kikubwa tulichokiwaza kukipata wala kidogo tulichostahili kupata.

Negotiation is a skill, the parties should get a hood negotiator/advisor on negotiation.

Kuliko kupata kwa jinsi unavyotaka ww, acha tukose vyote, iko siku kwa kuwa ni madai halali yatapatikana kama ipasavyo.
 
Chadema wanavyopenda ruzuku,hawana ubavu wa kususa
Kinachofanyika sasa no kuwatafuna waombaji ,halafu waweke milioni 20 kwa mwalimu ndipo jina liende tume
 
Back
Top Bottom