CHADEMA ndani ya Songea mjini

Makamba anapong'atuliwa alishamwandaa mwanae na ameshika sehemu nyeti ya secretarieti, Mwinyi mwanae ni waziri, Nape baba yake alikuwa kiongozi mwandamizi, Kikwete mwanae kiongozi umoja wa vijana nk. huu ndio uongozi wa ukoo anaotakiwa Nape auongelee na una mizizi miaka mingi kulilko kuhangaikia chama ambacho hata hakijashika dola.
 
ni kweli kabisa ufasadi ni tatizo kubwa, mkuu wa kaya hawezi kufanya kitu hapa maana anausika moja kwa moja

 
timing bom
 


Kijana Nape ndiye msiri mkubwa ambaye CCM hawakumjua alivyowasaliti alipokuwa mmoja wa waanzilishi wa CCJ na kuiba Katiba ya ANC kwa mzee Madiba, Mpendazone mwanzilishi mwenza katoboa siri hiyo kwanye mwendelezo wa mikutano ya Chadema - Ruvuma -Mbambabay. Nape anaubavu bado?
 
peoples power itawaondoa ccm miaka si mingi, kila kona imeshachoshwa, wakulima wamechoka, walimu wamechoka, wanafunzi wamechoka, wawekezaji wa ndani wamechoka, ila hawa watu wa usalama, polisi na wanajeshi wachini chini ambao hawanufaiki na serikari ya kirafiki tupo pamoja, hao wengine wanalinda maslahi yao binafsi.
 

Haya ndo matokeo ya songea?
 
safiiiiiiiiiiiiiii ijumaa itakua wapi nije na kamera kabisa
 
hapa cdm ninawashangaa, kushangaa pinda kushindwa kuwawekea umeme majirani zake. Sasa kwanini cdm isiamue genereta hili kusambazia umeme kwa baadhi ya wananchi wa madaba?? Kumbe ubinafsi upo katika kila chama!


Nadhani iq yako inaweza kuwa na matatizo. Hili gari ni maalum kwa ajili ya kampeni na shughuli nyingine za mikutano mbalimbali. kumbuka hili gari lina sehem ya jukwaa, na jenerator kwa ajili ya kuwezesha system nzima ya sound. Kwa hiyo tukiwapa hili generator Madaba halafu shughuli za mikutano ziindeshweje? Si unajua TANESCO walvyo na hila kwenye mikutano ya CHADEMA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…