Tendwa: Vurugu na mauaji ya Arusha Chadema hawawezi kukwepa lawama Send to a friend Tuesday, 11 January 2011 20:22
Na Joyce Mmasi
KILA chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na maandamano kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, hii ni sehemu tu ya haki za vyama vya siasa iliyoelezwa katika sheria namba tano ya mwaka 1992 ya vyama vya siasa.
Sheria hii pia katika sehemu ya tatu kifungu 1 (e) imeeleza wajibu wa vyama vya siasa na kueleza moja ya wajibu huo ni kufanya mkutano wa kisiasa na maandamano bila kufanya vurugu kwa mujibu wa sheria.
Sehemu ya nne katika sheria hii ya vyama vya siasa pia inaeleza wajibu wa msajili wa vyama vya siasa ambapo katika kifungu 1 (c) kinaeleza wajibu wa msajili wa vyama vya siasa, ni kuzuia kitendo cha uvunjifu wa kanuni za maadili kisiendelee na kukitaka chama au kiongozi wa chama kujirekebisha.
Inakuwaje vyama vya siasa vinazuiwa kutimiza wajibu na haki zao kwa mujibu wa sheria hiyo. Imekuwa ni kawaida kwa jeshi la polisi kuzuia kufanyika kwa maandamano na mikutano ya hadhara vinavyoandaliwa na vyama vya siasa, je, hatua hii ya polisi ni halali?
Msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa anasema serikali inapaswa kusikilizwa na kwamba endapo kutakuwa na zuio au ushauri katika utekelezaji wa haki au wajibu, chama kinachohusika kinapaswa kusikiliza na kutii.
Kauli ya Tendwa inafuatiwa na vurugu zilizosababishwa na maandamano ya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wakitekeleza vipengele hivyo vya sheria ya vyama vya siasa licha ya kuzuiwa na serikali kupitia jeshi la polisi.
Tendwa anasema endapo Chadema wangesikiliza amri ya jeshi la polisi na kuitii, kusingekuwa na vurugu wala matukio ya umwagaji wa damu yaliyofanyika mkoani Arusha.
Anasema jeshi la polisi kwa kutilia mashaka maandamano yao, walizuia maandamano hayo licha ya kuyaruhusu awali na kuruhusu mkutano pekee ambao walifanya hivyo kutokana na kujiandaa kulinda amani katika mkutano huo na maandamano.
Anasema kwa mujibu wa maelezo ya polisi, kulikuwa na kila dalili ya maandalizi ya vurugu yaliyoandaliwa na wafuasi wa chama hicho na hivyo kuruhusiwa kwa maandamano hayo kungepelekea vurugu, uvunjifu wa amani nap engine vifo vingi zaidi.
Nini chanzo cha vurugu hizo
Chanzo cha vurugu za Arusha ni kupinga uchaguzi wa Meya wa jiji hilo ambapo madiwani wa CCM pamoja na mmoja kutoka TLP walishiriki uchaguzi na kumchagua kiongozi wa jiji hilo, baada ya wale wa Chadema kugoma kutokana na kutokukubaliana na ushiriki wa mjumbe mmoja wa CCM aliyejulikana kama Mary Chatanda ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia mkoa wa Tanga.
Msajili anasemaje juu ya utata wa mbunge huyu wa viti maalum na malalamiko ya Chadema? Nadhani Chadema hawako wazi katika hili, kwani uhalali wa Mary Chatanda lilishatolewa ufafanuzi na katibu wa Bunge. Sheria iko wazi na ilifafanuliwa na katibu wa bunge baada ya madiwani wa pande zote mbili kuonyesha utata walipokuwa katika kikao cha kwanza cha uchaguzi wa Meya, ambapo vyama vyote viwili vilikuwa vikilalamikia ushiriki wa mjumbe mmoja mmoja kutoka kila chama.
Anasema ufafanuzi walioupata juu ya uhalali wa wabunge hao wa viti maalum waliokuwa wakilalamikiwa na vyama vyote viwili ni kwamba, sheria inawatambua wabunge kama madiwani wa sehemu wanazotoka na inaendelea kufafanua chama kinachowakilishwa na mbunge wa viti maalum, kitakuwa na haki ya kumpangia kazi sehemu yoyote isipokuwa hataruhusiwa kufanya kazi katika eneo lingine.
Anasema baada ya ufafanuzi huo utata wa suala la uwakilishi wa mbunge huyo wa viti maalum ukawa umemalizika na kwamba haelewi sababu za Chadema kususa kuendelea na uchaguzi wa Meya na kushangazwa na chama hicho kukwepa kueleza wafuasi wake suala hilo huku ikiendelea kushikilia msimamo wa kutomtambua mbunge huyo wa viti maalum wa CCM.
Uhalali wa uchaguzi wa Meya
Msajili anasema, baada ya kususia uchaguzi uliofanywa bila Chadema kushiriki vyama hivyo viwili vinavyohusika katika suala hilo vilipaswa kuzungumza ili kupatikana kwa suluhu na kwamba yeye alikubali kuwa msuluhishi, lakini anasema hajui sababu ya chadema kuamua kuitisha maandamano kabla ya kumalizika kwa mazungumzo ambayo anasema anaamini yangeweza kuleta suluhu na kujenga amani miongoni mwao.
Anasema jambo moja ambalo haliko wazi na ambalo angependa Chadema wakaliweka bayana ni kueleza wazi agenda yao, na nini wanachokitaka au wanachokusudia badala ya kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuhatarisha amani na kupunguza imani ya wananchi dhidi ya chama hicho.
Haijulikani hasa wanataka nini, maana kama ni kweli ilikuwa uhalali wa Mary Chatanda walishasomewa sheria na wakaelewa. Awali walizungumzia suala la kutaka katiba, kila mtu aliunga mimi nimeunga mkono nimetoa maoni yangu, Waziri mkuu naye kasema, na mwisho rais ameridhia, sasa waeleze wanataka nini ili madai yao yawe wazi na yaeleweke, anasema.
Msajili anasema inavyoonekana, ndani ya chama hicho, wapo baadhi ya viongozi wanataka kudanganya wananchi na kuficha kuwaeleza ukweli na akasema ni vyema kwa vyama vya siasa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.
Ushauri wa Tendwa kwa Polisi, CCM na Chadema
Tendwa anasema pamoja na huzuni iliyotawala kufuatia vurugu zilivyosababisha mauaji, ni vyema kwa jeshi la polisi kuangalia uwezekano wa kuepuka vurugu na badala yake kutumia nguvu zinazoweza kuhatarisha maisha ya watu.
Wananchi nao wasikubali kutumika na vyama vya siasa au baadhi ya watu, waepuke vurugu na watii maagizo wanayopewa, kama polisi ambaye ni mlinzi wa amani amezuia maandamano, wananchi wanapaswa kutii amri halali ya polisi, na vyama vya siasa kupitia viongozi wao vifuate taratibu ili kuimarisha amani na kuepuka vurugu zinazoweza kuleta maafa.
Anasema vyama vya siasa hususani Chadema kinapaswa kuepuka kutoa shutuma za mara kwa mara dhidi ya chama tawala huku akitolea mfano katika mikutano yake mingi na vyama vya siasa, vimekuwa vikitumia muda mwingi kushutumu chama tawala badala ya kutoa hoja ya kujenga nchi.
Kwa upande wa CCM, msajili anasema kama chama kiongozi kinapaswa kuwa makini na kushirikiana na vyama vingine katika kutatua migogoro ili kuepuka matukio yanayoweza kuhatarisha amani ya nchi.
Source : Mwananchi