Chadema nao wanakula bila kunawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema nao wanakula bila kunawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jenifa, Apr 19, 2011.

 1. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  chadema nao kumbe wanatafuna mapesa yetu bila kuwajibika mbowe anazitafuna tu hizo na kusingizia anajilipa madeni.
  Vita ya ufisadi yageukia vyama vya siasa


  [​IMG]
  Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovic Etouh

  Ramadhan Semtawa

  VYAMA sita vya siasa vyenye wawakilishi bungeni, vinadaiwa kuwa vimeshindwa kuwasilisha taarifa za hesabu kuhusu matumizi ya ruzuku ya jumla ya Sh17.14bilioni kwa mujibu wa sheria. Vyama hivyo ambavyo vinapata ruzuku inayotolewa na Serikali ni pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Tanzania Labour (TLP), NCCR-Mageuzi na UDP.

  Tuhuma hizo zimo kwenye Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inayoishia Juni 30, 2010.

  CAG ametoa ripoti hiyo baada ya sheria, kwa mara ya kwanza kumpa mamlaka ya kuvikagua vyama vya siasa ambavyo mahesabu yao, yanapaswa kuwasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania.


  "Taarifa za fedha kwa malipo ya ruzuku ya Sh17,146,819,904 kwa vyama vya siasa mbalimbali hazikuwasilishwa na vyama husika katika Ofisi ya Msajili," ilisema Ripoti ya CAG katika fungu la 27 kuhusu Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na matumizi ya ruzuku.


  Takwimu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa zinaonyesha kuwa CCM kinapata ruzuku ya asilimia 70, CUF asilimia 20, Chadema asilimia nane na NCCR-Mageuzi, UDP na TLP vinagawana asilimia mbili.


  Katika mahesabu ya kawaida, kati ya fedha hizo Sh 17.14 bilioni, CCM itakuwa imepata mgawo wa Sh12bilioni, CUF Sh 3.43bilioni, Chadema Sh1.37bilioni na vyama hivyo vitatu kwa asilimia mbili yao vikipata Sh343milioni.


  Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alipoulizwa na gazeti dada la The Citizen kwa simu alisema asingeweza kuzungumzia jambo hilo nyeti kwa mawasiliano ya simu kwani anahitaji kukaa na kulifanyia kazi kwa kina.


  Hata hivyo, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovic Utouh katika ripoti hiyo alisema kitendo hicho ni kinyume cha kifungu 14 (1) na (3) cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992.


  Sehemu ya kifungu hicho inasema, "Chama chochote cha siasa ambacho kina usajili wa kudumu, kinapaswa kutunza hesabu zake vizuri za ruzuku na kuwasilisha kwa Msajili."


  Kifungu hicho kinaendelea: "Kwa kutumia taarifa ya mwaka ya ukaguzi wa hesabu uliofanywa na mkaguzi anayetambulika kwa mujibu wa Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu, huku ikiwa na tamko la mali zote zinazomilikiwa na chama hicho."


  Utouh alisema pia kwamba Sh56.9milioni zilitumika na msajili huyo wakati hazikuhusiana na shughuli za vyama vya siasa.


  "Jumla ya Sh56,180.44milioni zilitumika na Msajili wa Vyama vya Siasa wakati hazikuhusiana na shughuli za vyama vya siasa," alisema Utouh katika taarifa hiyo.


  Mbali na tuhuma hizo, Utouh alisema kwamba kiasi cha Sh272.8milioni zilitumika kulipa deni la miaka ya nyuma la Bodi ya Udhamini ya chama cha UDP bila kuonyeshwa katika taarifa za fedha na kusema: "Malipo haya yanaathiri utendaji wa ofisi kwa mwaka wa sasa wa fedha."


  UDP kinaongozwa na John Cheyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).


  Alipoulizwa kuhusu fedha hizo, Cheyo alisema hajaisoma vyema ripoti hiyo na kuongeza kwamba atakuwa kwenye nafasi nzuri kuzungumzia hilo baada ya kuipitia kwa kina.


  "Kwa sasa hivi itakuwa ni vigumu kuzungumzia ripoti hiyo wakati sijaisoma vizuri. Nitakuwa siko sahihi kama nitazungumza bila kuisoma. Nipe muda nisome kisha nitaweza kuizungumza," alisema.
   
 2. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Simple minded. nimesoma habari yote sijaona anapotajwa Mbowe au Slaa kutumia kwa Mke au Mbowe kulipa madeni. Maoni yako yapo too biased kwa sababu tatizo sio kufuja bali kutowasilisha hesabu kitu ambacho hakitoi conclusion ya moja kwa moja kuwa vyama husika vimetumia vibaya fedha hizo.
   
 3. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Achana na wajivua gamba hao wala wasikuumize kichwa..
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Uhasibu na taratibu zake kwenye vyama vya siasa haupo. Vyama hivi vinapewa ruzuku ya nini? Mbona taasisi kama za dini zinajiendesha bila ruzuku. Tunaigharamia sana SIASA huku huduma za jamii zikizidi kudorora. Tukiondoa ruzuku za vyama, kesho yake CCM haitakuwepo.
   
 5. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  wasafi hao chadema wanatafuna mabilioni bila kuwajibika ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

  watanzania hatuna vyama tuna majambazi yanapigana kutuibia na kujaza matumbo.

  wanalipwa ngapi bungeni wanagoma kabla ya kwenda huko walituambiaga kila kitu kitakuwa wazi.
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Apr 19, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sijaona ufisadi uko wapi wandugu!
   
 7. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Hujui usemacho ww ni bora unyamaze, kila siku makanisa yanapata ruzuku za mashule yao na zahanati zao , halafu unasema nini? Tshs 600 bn kwa mwaka wanapata
   
 8. Y

  Yetuwote Senior Member

  #8
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ume-post bila kusoma? Au ni ushabiki ndo unaokusumbua? Mbona iko wazi kuwa tatizo ni la office ya msajiri wa vyama vya siasa. Hakuna chama kilichokaguliwa. Soma vizuri na kwa makini.
   
 9. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mi jitu mingine sijui hizi post wanaziandikia Chooni wakati wana kata gogo!!! Sasa kwenye huu upuu**z* wako ni wapi panapo wagusa walengwa kama watuhumiwa au ...............acha wenge kijana .
   
 10. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi serikali inapochelewa matokeo ya uchaguzi hua wako bizz wanachakachua, vivyo hivyo kwa mahesabu haya.Kama kila kitu kilikuwa kinaenda ipasavyo kwanini ucheleweshe kupeleka, yani kuchukua makabrasha nayo ngumu?

  Harafu unapoongelea swala la utawala wa sheria lazima wewe uwe wa kwanza kuutekeleza. Unachohubiri lazima ukiamini, sio unahubiri hivi wakati unaamini vile.
   
 11. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Anatafuta visingizio kwa sababu Chama chake kimeshindwa kujivua gamba gumu. Wanapapasa hapa na pale ili kutafuta roho za watu. Kama unapenda Mil 15 za Slaa omba uwe Bi. Mdogo si unaitwa Jenifa?
   
 12. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,617
  Likes Received: 2,998
  Trophy Points: 280
  Huyu aliyeleta hili alikuwa na nia fulani lakini bahati mbaya nadhani upeo wake umepelea. Uwongo au hila inayofanywa na mwenye akili (bright person) inakuwa ni vigumu sana hata kugundua kuwa ni uwongo au ni hila. Ila huu ni uwongo na hila ya mtu ambaye siyo tu ana nia ovu lakini hata akili ya kufanya huo uovu haijatimia.
   
 13. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Naamini siku GAG wakija kuwaambia fedha zililiwa lazima mtasema GAG wametumwa.
   
 14. koo

  koo JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kijana acha kukurupuka ukiambiwa hawajawasilisha haimaanishi hawaja tunza kumbukumbu au wametumia vibaya pesa kumbukumbu zipo na zitawasilishwa kwa msajiri kitu kilicho tatiza chama niujinga wa sheria yenyewe kukitaka cham kiwasilishe kumbukumbu za mahesabu kwa msajiri wakati msajiri hana utaalam na maswala yoyote yahusuyo pesa kikubwa cag mwenyewe alipaswa kufika kinondoni akagulie palepale
   
 15. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  halmshauri nao hawajala pesa ila hawajawasilisha tu matumizi.

  nyie bovu bovu kabisa miwani yenu ina rangi za chama haioni ukweli.

  mbowe anatafuna hizo pesa na mgogoro utafumuka muda sio mrefu.
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Wewe Mkaza Mjomba hebu tumia akili kidogo........nanukuu

  ''Takwimu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa zinaonyesha kuwa CCM kinapata ruzuku ya asilimia 70, CUF asilimia 20, Chadema asilimia nane na NCCR-Mageuzi, UDP na TLP vinagawana asilimia mbili. ''

   
 17. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wewe mbona hueleweki??? Umeleta mada jibu km m2 mwenye akili timamu, uneng'ang'ania MKE WA MTU KACHANGANYIKIWA, tukueleweje ndugu???? Unadhani kama wewe pesa zinakuchanganya wanawake wote ndo wako hivyo???? Kwanza unaelewa maana ya kuchanganyikiwa??? Mbona hapa inaonekana wewe ndo umechanganyikiwa??? Maisha ya watu binafsi hayakuhusu fuatilia maisha yako.
   
 18. A

  Awo JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 793
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Jenifa huwa ni wa kike sio? Au ni wivu tu?
   
 19. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwa vile wewe umezowea KULIWA baada ya mlaji kunawa basi ishakuwa shida.Ni hatari inapofikia hatua ya mafisadi kutumia nyumba ndogo zao kuwatetea.Extension ya ufisadi kwa njia ya ukahaba
   
 20. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hujapona vidonda vya kujivua gamba? Njoo nkusafishe kidonda cha gamba upone haraka.
   
Loading...