CHADEMA na unafiki uliotukuka

Hoja mufilisi kabisa, kwa kususa kunasaidia nini? Chaguzi karibia zote za marudio walikua wanasusa kutokana na mazingira mabaya ya hizo chaguzi, kipi kiliwafanya washiriki huu uchaguzi kama sio unafiki...
Sikubaliani na wewe, guy ulikuwa uwanja moana wakupambana na kujua mbivu na mbichi,ila kwasababu refa aliamua kutoa ushindi mezani Bila kuchezesha mechi,hivyo ushindi ukawa upande wa refa. Kwa ukatili wa kiwango kilicho shuhudiwa.
 
"Kwa sababu viongozi wakuu wamekosa.....wanataka wakose wote" hivi waliokosa ni viongozi wakuu tu??? Woteeeee wamekosa I mean wamenyimwa ubunge. Hadi wagombea wasio viongozi, acha kupotosha.
 
Lakini kumbuka uchaguzi huu ni tofauti kabisa na chaguzi zote zilizopita. Na pia kumbuka mwaka jana tumeona kioja kingine: Uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo nchi nzima ccm wamebeba. Tulishuhudia maafisa wahusika wakifunga ofisi hata wiki nzima ili tu wagombea wa upinzani wasipate fomu, au kurejesha fomu kwa wakati.

Miaka ya nyuma kulikuwa na uporaji for sure, lakini mwaka huu, hii ni kitu ingine kabisa. Inashangaza waleta mada kama hii, wala hawayaoni haya. Pengine ni makusudi?

Maana katika serikali ya Magufuli , kuwa mpinzani tu ni kosa la jinai.

Lakini ukiangalia vizuri, hao waliotangazwa kushinda, sio hasa wapinzani wenye misimamo mikali. Ni kama Magufuli "kagawa" ushindi wake kuwapa ambao hawatamsumbua Bungeni. Kule ambako unashangaa ccm wamepitapitaje, mfano Tunduma na Mbeya mjini, ndio unaambiwa ccm imeshinda.

CHADEMA bado wana muda wa kutosha kufanya maamuzi. Ni hekima kutoa muda kwanza, maana sheria inatoa muda wa vikao 3 vya Bunge. Ni mapema mno kuwahukumu
 
Mnatusumbua kwa kujifanya wapenda Democracy kumbe wahuni na wezi kama wale wengine tu.
Kwa hiyo mwizi ni CHADEMA ? Unachekesha sana. Lakini wakati watu kama wewe mnasherehekea "ushindi wa kishindo" katika mazingira ambayo mnajua kabisa bila polisi na Tume ya Uchaguzi inayopendelea ccm, wala msingetoboa, hamuangalii athari za ujambazi huu kwa taifa letu.

Kama alivyosema rais mstaafu Obama, matendo ya rais Trump na Republican wake yanaharibu taasisi nzima ya Demokrasia katika taifa hilo, na akasema kwamba hiyo ni "dangerous" path.

Nafikiria hivyo kwa nchi yetu pia. Akina Mwinyi, Mkapa na Kikwete walifikiria mbali zaidi ya ccm. Lakini Magufuli wala si kwamba anaifikiria ccm, bali yeye mwenyewe . Na hiyo ni habari mbaya kwa taifa la Tanzania
 
Mengi tuu...
Kuna clip ya jiwe anasema kwny mkutano wa hadhara kuwa Bunda hakuna taa za barabarani sabb tu wana mbunge wa upinzani!!!
Kwa hiyo kwa elimu yako mataa ya barabarani Bunda ni maendeleo? Mikoa au wilaya ngapi zenye wabunge wa CCM hazina hizo taa za barabarani?
 
We kijana wa zamani acha kuwa mjinga kwa kushabikia chama zee.
 
Hoja mufilisi kabisa, kwa kususa kunasaidia nini? Chaguzi karibia zote za marudio walikua wanasusa kutokana na mazingira mabaya ya hizo chaguzi, kipi kiliwafanya washiriki huu uchaguzi kama sio unafiki...
Kwa hiyo wewe kwa maono yako na uwezo wako woote bado hujaiona faida ya wao kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu??? Haya baki masikini hivoivo! Lakini usilazmishe na wengine wafikiri kwa kimo kidogo kama chako!
 
Kwa hiyo wewe kwa maono yako na uwezo wako woote bado hujaiona faida ya wao kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu??? Haya baki masikini hivoivo! Lakini usilazmishe na wengine wafikiri kwa kimo kidogo kama chako!
Sasa kama kulikua na faida unafiki wa kususa unatoka wapi?
 
Hivi nani alitengeneza ile orodha ya viti Maalum Chadema..bila ya Mnyika kuikana ilikuwa inapita...Chadema kuna Vichwa sana na yule mbunge wa Nkasi hafukuzwi uwanachama ila anakuwa labelled kibaraka
 
Kwani **** amekamatwa ? Au wenge la kukosa ubunge
Kwa hiyo Kama mwizi alikamatwa mwaka juzi akapigwa mawe, miaka yote wakamataji watumie adhabu ile ile?!

Mwaka huu adhabu kwa mwizi yule yule ni tofauti. Tulia tulii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…