CHADEMA na ulimbukeni

Tatizo la msingi la nchi hii ni watu kupenda udaku zaidi ya kufikiri,mwiba umeprove kuwa wewe ni mpenda udaku na mtu usiependa kufikiri,cdm wapo makini na wataendelea kuwa makini,,
 
Chama kinaongozwa na watu ambao hawakusoma;

M/Kiti ni DJ na katibi mkuu ni Askofu, unategemea nini kwenye chama hicho zaid ya kukurupuka ?

Haahaa! Kwa nini kila CDM ikianzisha ajenda inakuwa ya kitaifa? Ufisadi, Katiba Mpya, Matumizi mabaya ya nguvu za Polisi, etc! CCM sasa hivi wamechanganyikiwa kila mtu anaongea la kwake: Chikawe vs Mwakyembe/Sitta, UVCCM vs CCM, Kombani/Werema vs JK, Mwema vs Andengenye, Makamba vs Nahodha, etc! CCM is slowly dying, to say the least!
 
Mkuu asante maana mbavu zinauma.
 
Chama kinaongozwa na watu ambao hawakusoma;

M/Kiti ni DJ na katibi mkuu ni Askofu, unategemea nini kwenye chama hicho zaid ya kukurupuka ?

Chenu chenye wasomi kinaingiza nchi katika mikataba ya mibovu ya "shanga kwa almasi" Nafikiri utakuwa wa karne kama si ya 16 basi ya 17
 
Mimi nawahasa wanajamii mliokuwa makini huyu ni TUNTU ANAYE BEEP NA PRIVATE NUMBER!msameheni bure!kwani mbuzi mwovu akichunga na mbuzi mwema hata mwema ugeuka kuwa mwovu!!hivyo yeye hawezi kiona viongozi vilaza niwapi!ila kaona wa chadema!
 
Mwiba nimwehu uwezi kuwa na thread ndefuuu lakini chenga tupu!!mimi ninachofikiria nikwamba anatafuta wingi wa wawa changiaji! au MS????
 
chama kinaongozwa na watu ambao hawakusoma;

m/kiti ni dj na katibi mkuu ni askofu, unategemea nini kwenye chama hicho zaid ya kukurupuka ?

hivi wewe na mwiba wote ni great thinker? Nina mashaka mmeingia choo cha kike-jf siyo mahali penu, labda kwenye taarabu za mkwere kila ijumaa

mwiba -hutaweza kubadili roho na uelewa wa great thinkers ndani ya jf-labda nikupe mifano michache ya mafanikio ya chadema,

1. Vita ya ufisadi -moto umeshika kasi ni ilani ya chadema siyo ccm -mnadandia lazima mtaanguka lini -ili kuonesha hampo makini na hili mkwere na ccm waliwapigia debe mafisadi wenzio-mfano mramba

2. Vita ya kuandika katiba mpya -ipo kwenye ilani ya chadema haipo kwenye ilani ya ccm msivyokuwa makini-mnakurupuka tuu, yes madai yalianza siku nyingi lakini why now reason chadema. Unalijua hilo kawaulize werema na celina walivyokuwa wanajua

3. Vita ya malipo ya dowans na sakata zima la dowas/richmond -slaa aliwambia mkwere anamkono pale mkamjia juu kwa matusi sasa uvccm wamekuja juu -hivi hapa nani kama limbukeni inachekesha kweli slaa anawatisha.

4. Afya na elimu bure- ilani ya chadema -hii mtaiga tuuu mpende msipende

5. Kupinga uchakachuaji -huo ni msimamo wa chadema

6. Makazi bora -kamulize mkwere ameanza na kwao bagamoyo amewambia waanze kujenga nyumba bora alikuwa wapi 5years? Nani limbukeni?

7. List of shame -ni msimamo wa dr slaa na chadema miaka yote mpaka wote waachie ofisi za umma.

Haya jamaa yako anaedai chadema inaongozwa na watu ambao hawakusoma

kama unaweza na wewe ni great thinker
weka hapa profile ya
mkwere vs mbowe
makamba vs dr slaa

harafu tuone kati yao nani kasoma zaidi ya mwenzake tunakuruhusu uweke na degree za kununua udom na muhimbili baada ya kuporoka misifa.
Usikurupuke kuandika usilolijua shule ya slaa huwezi hata kidogo kulinganisha na mkwere na msanii/ mropokaji makamba.

Waulize wanaofanya tathmini ya uchaguzi aliyeanguka zaidi ya alivyotegemea ni nani -usikurupuke kuandika-chukua chako mapema imechakachua ubunge shinyanga mjini, segerea, karagwe, kibaha, sumbawanga, kigoma mjini, bukoba mjini, mbeya vijiji.

Next time usikurupuke kuandika utumbo -chadema inakua kwa kasi na inaongozwa na nguvu ya umma.
 
Alooh kama tupo Great thinkers hapa JF basi wewe utakuwa mmoja wao na sio wale wanaovamia mada na kurusha mijitusi kama makaro ya choo kikubwa ,hawa ni watu hatari hapa JF,inawezekana wamesoma lakini hawakufahamu.

Hapo umeweka muhtasari wa yale yote niliyoyaandika isipokuwa hapo ulipotaja CUF nakuchukulia kuwa umeteleza au ni jazba imekupeleka utegu.

Chadema ni lazima wajisahihishe na kuwacha kuwa kama malaghai au matapeli ,iwapo wanawaelekeza watu kufanya kitu basi washikamane na kitu hicho na sio baadae wazalendo waone wamepandishwa mkenge au wamedanganywa na Viongozi wa Chadema hawasikiki na hata wakisikika huwa wamezuka au kuzusha jingine.
 
Mimi nawahasa wanajamii mliokuwa makini huyu ni TUNTU ANAYE BEEP NA PRIVATE NUMBER!msameheni bure!kwani mbuzi mwovu akichunga na mbuzi mwema hata mwema ugeuka kuwa mwovu!!hivyo yeye hawezi kiona viongozi vilaza niwapi!ila kaona wa chadema!

Hahahahahahaaa kweli huyu ni tuntu.
Ana beep na private number halafu anaomba kupigiwa!! kazi kweli kweli.
 
hapo umesema mkuu...
 
Hahahahahahaaa kweli huyu ni tuntu.
Ana beep na private number halafu anaomba kupigiwa!! kazi kweli kweli.

Mwita, jamaa anasahau akishatuma tafadhali nipigie namba inaonekana? Hapo ndipo utapima ulimbukeni! Na si unajua namba zimesajiliwa? Sasa hata ukiwa na private namba unajifichaje? Kazi ipo
 
Hii hoja ilikuwa kwenye tamko la waislamu pale diamond jubilee au? mbona unakurupuka sana nini maoni yako au ushauri wako kwa CHADEMA?
 
UCHAGUZI WA MEYA MANISPAA YA ARUSHA

Kwa kuzingatia kwamba umekuwepo upotoshaji mkubwa kuhusu uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha, na hata kusababisha malalamiko mengi na vurugu, Kamati Kuu inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:-

Kwanza:

· Matokeo ya Udiwani Manispaa ya Arusha yalikuwa ifuatavyo: Madiwani wa Kata: CCM 10, CHADEMA 8 na TLP 1 – Jumla viti 19.
· Madiwani Viti Maalum: CCM 3, CHADEMA 3.
· Wabunge Viti Maalum: CCM 3, CHADEMA 3.

Matokeo ya jumla: CCM – Viti 16, CHADEMA 14 na TLP 1. Jumla Viti 31.

Siku ya kupiga kura (tarehe 18/12/2010) Mkutano ulipoanza wajumbe 14 wa CHADEMA hawakuwepo. Waliofika ni wajumbe 16 wa CCM na 1 wa TLP, jumla wajumbe 17 ambao ni zaidi ya nusu ya wajumbe wanaotakiwa ili mkutano uwe halali kwa mujibu wa sheria.

Katika mazingira haya Msimamizi wa Uchaguzi aliendesha uchaguzi ambapo Ndugu Gaudence Vicent Lyimo wa CCM alipata kura 17, hivyo kutangazwa mshindi halali wa kiti cha Umeya na Ndugu Michael Kivuyo wa TLP alipata kura 17 na kutangazwa mshindi halali wa kiti cha Naibu Meya.

Kwa hiyo wanaosema uchaguzi huo haukuwa halali ama hawajui sheria au wanajiingiza tu katika ushabiki wa kisiasa.

CHADEMA wanadai katika wale wajumbe 16 wa CCM, mmoja wao (Mhe. Mary Chatanda) hakuwa mjumbe halali kwa kuwa katika kugombea Ubunge wa Viti Maalum aligombea kupitia Mkoa wa Tanga.

CHADEMA, kupitia Msimamizi wa Uchaguzi waliomba ufafanuzi wa kisheria kutoka Tume ya Uchaguzi, Katibu wa Bunge na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Ofisi zote hizo tatu zilitoa jibu kwamba Mhe. Mary Chatanda alikuwa mjumbe halali wa kikao hicho, na kwamba Wabunge Viti Maalum ni Wabunge wa Kitaifa na vyama vyao ndivyo vinawapangia Halmashauri za kufanyia kazi. Mhe. Mary Chatanda anaishi Arusha akifanyakazi kama Katibu wa CCM wa Mkoa huo hivyo CCM ilimpangia hapo hapo Arusha ndipo afanyie kazi za Halmashauri kama Diwani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa iliarifiwa kuhusu uamuzi huu kama sheria inavyotaka.

Ni ufafanuzi huo huo ndio CHADEMA waliutumia kushinda kiti cha Halmashauri ya Hai baada ya kuwapangia kufanyakazi katika Halmashauri hiyo Wabunge 2 wa Viti Maalum na ambao si wakaazi wa Wilaya hiyo. Kura hizo mbili ndizo ziliwapa CHADEMA ushindi; na CCM tumekubali matokeo kwa kuwa kwa kufanya hivyo CHADEMA hawakuvunja sheria.

Uhalali wa Mhe. Mary Chatanda kupiga kura Manispaa ya Arusha ni sawa sawa na uhalali wa Wabunge wawili wa Viti Maalum wa CHADEMA walivyopiga kura Hai.

Jambo hili CHADEMA wanalijua vizuri lakini wanapotosha umma kwa makusudi wakitumia vyombo vya habari ambavyo bila kufanya utafiti navyo vimekuwa vinashabikia suala hili.

Kwa kifupi Kamati Kuu inasisitiza kwamba Uchaguzi wa Meya wa Arusha ulifuata sheria kwa ukamilifu, na washindi walishinda kihalali na hakuna sababu ya kurudia kufanya uchaguzi mwingine. Iwapo kuna watu hawaridhiki na mchakato wa uchaguzi huo wanayo nafasi ya kupinga katika vyombo vya sheria bila ya kufanya fujo wala kuleta uvunjifu wa amani kama ule uliotokea tarehe 5/1/2011 kule Arusha.
 
Bila shaka huyu anatumia tumbo na kwato badala ya kichwa kufikiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…