CHADEMA na mbio za mwenge

CHADEMA na mbio za mwenge

Maboso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
5,163
Reaction score
5,765
Wakuu,
Salamu zenu na habari ya mapumziko marefu.

Napenda tushirikiane kutafakari na kujadiliana hili jambo. Wengi wetu tumeshuhudia jinsi viongozi na wabunge wa CHADEMA walivyo mstari wa mbele katika kushinikiza wananchi kutochangia na kushiriki shughuli za mwenge wa uhuru.

Binafsi napata shida sana kutambua nini huwa ni lengo la hawa viongozi wa CHADEMA. Najiuliza kama ni kweli huwa wanamaanisha wanachokisema au huwa wanaamua kuropoka tu.

Hebu tujaribu kutazama hizi picha za tukio la kuzimwa mwenge Iringa halafu tujaribu kujadiliana hasa tukizingatia huyu mwenzetu Mchungaji Msigwa naye ni mmoja wa wanaopinga na kuhamasisha wananchi kususia shughuli za mwenge.

IMG_0862.JPG IMG_0862.JPG IMG_0864.JPG IMG_0863.JPG IMG_0861.JPG IMG_0868.JPG IMG_0866.JPG i33.jpg i32.jpg i29.jpg i28.jpg IMG_0865.JPG
 
labda tujiulize Msigwa kaenda kwa sababu ya kuzima mwenge
au kaenda kwa vile mwenge huo umezimwa katika jimbo lake?
ametumia busara kuwakilisha wananchi wake mbele ya rais.
Kuna mawili hapo kuukata mwenge na kuwakilisha wananchi mbele ya rais wao.
unaweza kuingia kanisani kwa heshima hata kama wewe sio mkristo wa dhehebu lile kama lengo ni uwakilisho wa jumuia yako.Haimaniishi kuwa pale anasapoti hilo litochi.
 
Kwenye picha lakini wanapendeza, kwa maoni yangu ni vizuri kama watanzania tukajadiliana kama mwenge uendelee au la bila kujali itikadi za vyama!
 
Mwenge hauna maana yoyote ile

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Lokissa CHADEMA inakubaliana na Mwenge? Kwani kutoshiriki kwenye mbio za Mwenge ni msimamo wa watu binafsi au ni wa kichama?
 
Last edited by a moderator:
labda tujiulize Msigwa kaenda kwa sababu ya kuzima mwenge
au kaenda kwa vile mwenge huo umezimwa katika jimbo lake?
ametumia busara kuwakilisha wananchi wake mbele ya rais.
Kuna mawili hapo kuukata mwenge na kuwakilisha wananchi mbele ya rais wao.
unaweza kuingia kanisani kwa heshima hata kama wewe sio mkristo wa dhehebu lile kama lengo ni uwakilisho wa jumuia yako.Haimaniishi kuwa pale anasapoti hilo litochi.

Mkuu,
Upo sahihi kabisa kuwa Msigwa kaenda pale kama mwakilishi wa wananchi. Lakini mimi kinachonitatiza ni kuwa kama yeye haungi mkono mwenge na amekua akiwashawishi wananchi wake wa jimbo la Iringa kutounga mkono shughuli za mwenge, je pale amekwenda kumuwakilisha nani? Kama akiwa bungeni huwa anakua mstari wa mbele katika kususia bunge pale anapoona mawazo ya wananchi wake hayasikilizwi, kwa nini asifanye hivyo hivyo katika shughuli hii ya mwenge?
 
Lokissa CHADEMA inakubaliana na Mwenge? Kwani kutoshiriki kwenye mbio za Mwenge ni msimamo wa watu binafsi au ni wa kichama?

Chadema haikubaliani na mwenge na ndio maana nimeshangaa kumuona Mch. Msigwa kwenye hii shughuli.
 
Wakuu,
Salamu zenu na habari ya mapumziko marefu.
Napenda tushirikiane kutafakari na kujadiliana hili jambo. Wengi wetu tumeshuhudia jinsi viongozi na wabunge wa Chadema walivyo mstari wa mbele katika kushinikiza wananchi kutochangia na kushiriki shughuli za mwenge wa uhuru. Binafsi napata shida sana kutambua nini huwa ni lengo la hawa viongozi wa Chadema. Najiuliza kama ni kweli huwa wanamaanisha wanachokisema au huwa wanaamua kuropoka tu. Hebu tujaribu kutazama hizi picha za tukio la kuzimwa mwenge Iringa halafu tujaribu kujadiliana hasa tukizingatia huyu mwenzetu Mchungaji Msigwa naye ni mmoja wa wanaopinga na kuhamasisha wananchi kususia shughuli za mwenge.

View attachment 116699View attachment 116699View attachment 116708View attachment 116707View attachment 116706View attachment 116705View attachment 116704View attachment 116703View attachment 116702View attachment 116701View attachment 116700View attachment 116709

Una akili ndogo kama ya Nape na Lukosi .Huyu ni kiongozi wa eneo hilo ana awajibu kuwepo nyumbani kwake na si zaidi .Kwani katangaza watu wachangie mwenge au kaenda shughuli inaishia ? Poor you
 
Nao wengine waliovaa sare za CHADEMA wote hao ni wabunge wa Iringa Mjini hivyo walipaswa kuwepo uwanjani? Kwani wabunge wanapotoka nje ya bunge huwa hawahusiki na kikao cha bunge kinachokuwa kinaendelea?
 
Wakuu,
Salamu zenu na habari ya mapumziko marefu.
Napenda tushirikiane kutafakari na kujadiliana hili jambo. Wengi wetu tumeshuhudia jinsi viongozi na wabunge wa Chadema walivyo mstari wa mbele katika kushinikiza wananchi kutochangia na kushiriki shughuli za mwenge wa uhuru. Binafsi napata shida sana kutambua nini huwa ni lengo la hawa viongozi wa Chadema. Najiuliza kama ni kweli huwa wanamaanisha wanachokisema au huwa wanaamua kuropoka tu. Hebu tujaribu kutazama hizi picha za tukio la kuzimwa mwenge Iringa halafu tujaribu kujadiliana hasa tukizingatia huyu mwenzetu Mchungaji Msigwa naye ni mmoja wa wanaopinga na kuhamasisha wananchi kususia shughuli za mwenge.

View attachment 116699View attachment 116699View attachment 116708View attachment 116707View attachment 116706View attachment 116705View attachment 116704View attachment 116703View attachment 116702View attachment 116701View attachment 116700View attachment 116709

Kwani Nani aliekwambia amenda kwa shughuli hizo za Mwenge? Yeye alikuepo Kumuenzi baba wa taifa. You Got a problem with that?
 
Una akili ndogo kama ya Nape na Lukosi .Huyu ni kiongozi wa eneo hilo ana awajibu kuwepo nyumbani kwake na si zaidi .Kwani katangaza watu wachangie mwenge au kaenda shughuli inaishia ? Poor you

Usapanic mkuu. Tulia leta hoja tujadiliane. Ulichoandika hapo hata sijakuelewa ulitaka kumaanisha nini.
 
Kuna watu hapa wanajitahidi kutenganisha maji na tope... Mantiki inapopotea majadiliano hugeuka mabishano!
 
Vijana wa Chadema watakujibu mimi sina chama
ninaujua msimamo wa Msigwa na pia ni mtu anaejua umuhimu wa uwakilishi.
Kumsusia rais sio jambo jema akiwa jimboni mwake
yeye hana ugomvi na JK ana ugomvi na mwenge.
labda nikuulize kama huli kitomoto kisha nkakualika kwangu kwa mazungumzo hutakuja kwa vile nakula kitimoto??
utakuja tutaongea lakini kitimoto changu hutakigusa na hakitakuathiri ukiwepo...
Kama tungemuona Msigwa akiunyanyua mwenge huo ndio tungehoji uhalali wa kauli zake kama anasimamia anachosema

Lokissa CHADEMA inakubaliana na Mwenge? Kwani kutoshiriki kwenye mbio za Mwenge ni msimamo wa watu binafsi au ni wa kichama?
 
Chadema haikubaliani na mwenge na ndio maana nimeshangaa kumuona Mch. Msigwa kwenye hii shughuli.

kwani siasa ni vita?kaenda kusikiliza mwenge una sera gani katika jimbo lake ili akisema neno msije kusema hakuwepo ameambiwa
 
Hayo maguo waliyovaa ndio lile vazi la taifa lilioundiwa tume na Nchimbi wakati huo akiwa Waziri wa Vijana, Utamaduni, na Michezo au ndio CCM wameamua kutoka kivingine kujaribu ku-compete na gwanda na M4C kimavazi? Ha ha ha!

CCM wanadhani mapenzi ya wananchi yako kwenye mavazi! Mnakosea sana wajameni!
 
Vijana wa Chadema watakujibu mimi sina chama
ninaujua msimamo wa Msigwa na pia ni mtu anaejua umuhimu wa uwakilishi.
Kumsusia rais sio jambo jema akiwa jimboni mwake
yeye hana ugomvi na JK ana ugomvi na mwenge.
labda nikuulize kama huli kitomoto kisha nkakualika kwangu kwa mazungumzo hutakuja kwa vile nakula kitimoto??
utakuja tutaongea lakini kitimoto changu hutakigusa na hakitakuathiri ukiwepo...
Kama tungemuona Msigwa akiunyanyua mwenge huo ndio tungehoji uhalali wa kauli zake kama anasimamia anachosema
Vipi ukisikia kuna Sheikh anauza Kitimoto ingawa hali, wewe utamuelewaje? Jibu lake likiwa ni kwamba wanaouza ni watu wengine yeye anachukua hela tu, utamuonaje? self denial ni kitu kibaya sana. Leo kwenye Ratiba kulikuwa kunaonyesha kwamba Msigwa ataubeba Mwenge halafu yeye akakataa?
 
Back
Top Bottom