CHADEMA na Lowassa wao, wawaponza Wamiliki wa Hotel ya Bahari beach na Mwanza Hotel?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Heshima kwenu wakuu,

Nmeshitushwa na habari ya Hotel ya Bahari beach kurudishwa Serikalini kwa Kigezo kwamba haitimizi Matakwa ya Mkataba.

Waziri mpya wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla, ametoa siku 60 ili kurejeshwa serikalini kwa hoteli 10 ambazo Serikali ilizibinafsisha miaka ya nyuma. Hoteli nyingi zilibinafsishwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

Akizungumza mara baada ya kutoa tamko la kuzirejesha serikalini hoteli 10 kati ya 16 zilizobinafsishwa, Dk Kigwangalla alisema wamiliki wa hoteli hizo wameshindwa kutimiza matakwa ya mikataba.

Baadhi ya Hoteli ambazo zilibinafsishwa na zimetajwa kuwa haziendani na mkataba ni Moshi Hotel, Mwanza Hotel, Savoi Hotel, Mikumi Wildlife, Embassy Hotel na Bahari Beach.

Je hili zengwe halihusiani na Siasa? CHADEMA mara nyingi imekuwa ikifanyia Vikao vyake kwenye Hotel ya Bahari Beach. Hata Vikao vya Siri. Vikao vya kumpokea Lowassa vilifanyikia hapa. Je hii inaweza kuwa sababu? Angalieni Wamiliki wa hizo hotel na Ushiriki wao katika Siasa.

Kutoka Bahari Beach Hotel: Yaliyojiri katika Mapokezi ya Edward Lowassa kujiunga CHADEMA
Siku ya Kwanza Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA Kilichoketi Bahari Beach Hotel (Habari Picha)
Wabunge wateule CHADEMA wakutana hoteli ya Bahari Beach kupanga mikakati

Mwanza Hotel inamilikiwa na na Mwanaccm tena Mnec Christopher M Gachuma.

Gachuma, Sofia simba, Kimbisa, Nchimbi, nk, Walikuwa Team Lowassa na ndio waliopinga jina la Lowassa kukatwa hadi wakatoka nje ya Ukumbi. Walivyorudi wakaanza kuimba “tuna imani na Lowassa, oyaa, oyaa, oyaa. Lowassa kweli? kweli kweli kweli Lowassa...”

Wimbo huo uliongozwa na kundi lililokuwa nyuma ukumbini likijumuisha mfanyabiashara maarufu nchini, Christopher Gachuma, mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Christopher Sanya, aliyekuwa mbunge wa Musoma Mjini, Vedastus Mathayo na mjumbe mwingine aliyetambulika kwa jina la Joseph Marwa ambaye anatoka Mara. Wajumbe hao na baadhi wengine waliendelea kuimba wimbo huo kwa takriban dakika mbili kabla ya kunyamaza kumruhusu Kikwete afungue kikao.

Juzi Kati Rais Magufuli alisema angekuwa yeye ndo Kikwete, angewatoa nje wote waliokuwa wakiimba.

"Nasema kwa dhati kabisa, Mheshimiwa mwenyekiti mstaafu, kuwa huo moyo wa uvumilivu ulio nao, sidhani kama mimi ninao.

Nakumbuka siku ile wanaimba eti wana imani na mtu fulani, ningekuwa mimi ndio mwenyekiti, robo au nusu wangepotea_.

Nawaomba sana ndugu wajumbe, mniombee nipate angalau nusu ya moyo wa uvumilivu alionao bwana Kikwete."


Sofia simba amenyang'anywa ubunge na kufukuzwa kwenye chama. Kimbisa kapewa onyo nasikia hata Ubunge wa Afrika Mashariki ulienda na Maji.

Gachuma ulitegemea wampe adhabu gani?

Je huu Usaliti waliouonesha kipindi cha Uchaguzi 2015 inaweza ikawa ndo sababu ya kufanyiwa Zengwe?

Naomba maoni hasa kwa watu wanaowaza nje ya Box.

Magufuli: Ningefukuza nusu ya wote ndani ya siku moja kama wangeniimbia eti wana imani na mtu fulani
 
Mimi nitakuwa na maswali haya:
  1. Serikali ina pesa ya kulipa market value ya hizo hoteli?
  2. Serikali itakuwa na uwezo wa kuziendesha kwa faida hotel hizo au ndo itawapa wengine ambao nao hatuna uhakika kama wataziendesha kwa ufanisi?
Kigwa anapenda makamera, hii yaweza kutugharimu hasa ikizingatiwa kwamba sekta ya utalii ni muhimu kwa uchumi. Badala ya kuzinunua hizo hoteli, serikali iwape salary increment watumishi wake.
 
Yohana 15:15 Siwaiti tena watumwa kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake......
Watz mnajua anachafanya bwana wenu? Kama hamjui nyie ni nani basi? Mbona mnadai haki wakati jina lenu halistahili?
 
Sijui kuhusu hizo zingine ila Mwanza hotel, Moshi hotel, mikumi hotel na Mbeya hotel ni hovyo kabisa hata bure mtu halali pale let alone kwa kulipia. Hizi hotel zilikufa zamani sana na gov imechelewa sana kuzichukua.
 
Mimi nitakuwa na maswali haya:
  1. Serikali ina pesa ya kulipa market value ya hizo hoteli?
  2. Serikali itakuwa na uwezo wa kuziendesha kwa faida hotel hizo au ndo itawapa wengine ambao nao hatuna uhakika kama wataziendesha kwa ufanisi?
Kigwa anapenda makamera, hii yaweza kutugharimu hasa ikizingatiwa kwamba sekta ya utalii ni muhimu kwa uchumi. Badala ya kuzinunua hizo hoteli, serikali iwape salary increment watumishi wake.
Hivi Vito vya utalii vinafanya nini hapa Tanzania? Hoteli nyingi zenye standards wafanyakazi wake ni wa-Kenya.
 
Back
Top Bottom