CHADEMA na lawama kwa Walimu

Bila shaka kwa nguvu na Muumba tu wazima na harakati za kujenga maisha yetu pamoja na taifa kwa ujumla.

Leo nikiwa kama Mwalimu kitaaluma, naomba nizungumzie madai, lawama na kuhusishwa kwa kundi hili adhimu na siasa za nchi yetu.

Kwa kuanza naomba mtambue, Walimu sio watumishi kada mali ya wanasaisa, walimu hatuhusiki na umiliki wa chama chochote cha siasa nchini, so far. Kumekuwa na lawama, chuki na maneno ya kejeri kutoka kwa makada wa vyama vya siasa hasa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenda kwa Walimu haswa linapokuja suala la uchaguzi mkuu hapa kwetu.
Ipo hivi; imeonekana mara nyingi walimu wakipewa nafasi za kusimamia uchaguzi mkuu, naomba mtofautishe, mamlaka pekee nchini zenye kusimamia hili zoezi ni NEC, POLISI na Wizara ya mambo ya ndani kwa ujumla, sio CWT wala chama chochote cha Walimu. Walimu sio wasimamizi, ni waendesha zoezi la kupiga kura, mwisho wa siku wao hufanya vile wanavyoelekezwa.

Vijana wa CHADEMA wamekuwa na kawaida ya kulaumu Walimu kuwa wanahusika na wizi wa kura ama kuisaidia CCM kuingia madarakani, jambo ambalo linashangaza, na linasikitisha ukizingatia CDM ndio chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, na mnajua ilivyo hadhi kubwa kuwa chama kikuu cha upinzani, hii ni sawa na kusema “chama mbadala wa chama tawala” kina kuja na hoja hii kwa kweli.

Walimu tunapata nafasi nyingi za kusimamia zoezi kulingana na wingi wetu katika kada, vile vile uzoefu wa kuratibu shughuli zinazohusisha watu wengi, uandishi na uzoefu katika kutoa maelekezo, mambo ambayo zoezi la upigaji kura linataka. Suala la kutumika na CCM halihusishi waalimu kaa sababu hakuna semina ya walimu kama walimu peke yake ya namna gani kura ziibiwe kituoni, ama waraka rasmi kwa Walimu kuhusu wizi wa kura. Na endapo itatokea mwalimu kama msimamizi wa kituo akafanya hivyo asihusishwe kama mwalimu kwa sababu hakutumwa kama Mwalimu, ualimu unahusiana vipi na wizi wa kura? Ni mtaala? Miiko ya kazi? Ama ni kitu gani.

NIONAVYO MIMI

CHADEMA huitumia hii hoja kwa namna mbili.
1.SABABU YA KUPATA MTAJI WATU KISIASA Kwa kuwa Walimu ni kundi kubwa, wataka wawa “provoke” kwamba wao ndio sababu ya matatizo yote nchini pamoja na matatizo yao wenyewe lengo likiwa ni kuwafanya wawe subjects wao ambapo kwa madai haya maana yake Walimu kuyakataa itabidi wafanye matakwa ya CDM, kwa neno la kimombo wanaita “Blackmailing” yaani jitihada za kuwa prove wrong watu, Walimu wawape favor CDM.

Ndugu zangu CDM, kama kweli mnataka kuwa chama tawala nchi hii, acheni siasa za namna hii, changamoto katika utawala zipo kila kona duniani, fanyeni siasa yenu kama wanasiasa mnao jielewa, kumbukeni kundi mnalojaribu ku mess up nalo ni kubwa mno, lawama zikiwa nyingi zinakuwa sehemu ya maisha yetu, tukiwazoea hamtakuwa na mtaji wa watu huenda kama mnavyojaribu kutafuta kupitia sisi, dare not comrades!

2. KISINGIZIO BAADA YA KUSHINDWA UCHAGUZI
“Hata wakishinda wao, CCM itaunda serikali” nadhani mnamfahamu aliyesema hii kauli, kwa hiyo jueni kwamba mpo kwenye chi ambayo watu wana haki ya kupiga kura ila sio kuchagua viongozi, msilalamike lalamike hovyo kuwalaumu walimu as if sisi ndo tunaunda serikali, wapo walimu wengi tu makada wa vyama vya siasa ikiwemo chama chenu, amini usiamini kwa lawama hizi! (Sina neno)

”CCM itatumia dola kubaki madaraki” vile vile mnajua aliyesema hii kauli, hakusema CCM Itatumia Walimu kubaki madaraki, mkishindwa kuelewa na hapo basi hamjaamua tu na mnachuki na sisi za bure tu.

Mwisho kabisa naomba niwasihi muweke hadharani sera zenu kwa mtindo wa kuzidisha kutoa elimu zaidi hasa maeneo ya vijijini ambapo kuna ngoma kubwa sana ya chama tawala. Msiishie kutukana walimu, mbaya zaidi hamtulipi mnazidisha hasira tu.

Nawasilisha.
Wewe ni toleo la ngapi la Walimu?
 
Tatizo la walimu wengi ni kutokujielewa, wanazidiwa na kada zingine zote.
Kwamba walimu wasipohusishwa kwenye Mambo ya upigaji kura bac chadema itashinda uchaguzi? Elimu elimu elimu Ni tatizo kwa nchi yetu yaan mpaka saiz walio wengi hawajui sabab Ni ipi inafanya upinzan wasipate haki yao hata wakishinda kihalali,hivi kweli kundi la ualimu ndilo limegeuka tume ya uchaguz? Kuna clip zilionekana makamba ,kinana wakiwa masaki Wana edit matokeo je walimu walikwepo pale ndani?
 
Wanatishwa sababu kura zinaletwa kwenye masanduku
Jaman acheni ujinga anyefinalize matokeo sio mwalimu Bali ni tume ya uchaguz ,Ni vile tu mmepata pakujifichia Mambo yanapokuwa tofaut kwa upande wenu ,mtaan humu tuna walimu wengi Sana Ni wafia wa chadema na hawaitak ccm kabisa na wengine washatishwa Sana Lakin msimamo wao Ni ule ule .

Hoja hapa Ni Nan mwenye kuamua idad za kura ziende chama gan walimu mnawaonea tu
 
Swali la kijiuliza kwa nini kila siku nyie tu walimu mbona siyo kada nyingine ??
Walimu pekee wanafika laki tatu na uchafu Kama sijakosea na ndio kada yenye watumishi wengi Sana nadhan shida ipo hapo ,mkubwa jalala
 
Bora hata ueleweshe; kibarua kigumu hiki
 
Kinachotokea kipindi Cha uchaguzi Kati ya chadema na ccm ndicho hicho hicho kilichotokea kwa wagombea wengi wa ccm ngazi ya ubunge ,mtakubaliana na mm kuwa wabunge wengi walioshinda kura zamaoni sio hao waliopewa nafas ya kupeperusha ticket ya Jimbo ,Zaid kilichofanyika Ni maamuz ya mtu mmoja mwanaume haswa na kuamua kuwa mtu wa tatu au wa nne anapewa kijiti Sasa mnashindwa nn kuelewa hoja ndogo hii kuwa kura haziamui chochote linapokuja swala la kushika madaraka?.

Upeo mdogo ndio unawalaumu walimu Ila wenye akili wanaujua ukweli kuwa mwalimu hawez kuwa sabab ya chadema kutoshika madaraka.
 
Safi kabisaaa, wasipokuelewa wewe basi tenaa, tupo kwenye nchi ambayo watu wake wana uhuru wa kupiga kura, sio kuchagua viongozi
 
Jaman acheni ujinga anyefinalize matokeo sio mwalimu Bali ni tume ya uchaguz ,Ni vile tu mmepata pakujifichia Mambo yanapokuwa tofaut kwa upande wenu ,mtaan humu tuna walimu wengi Sana Ni wafia wa chadema na hawaitak ccm kabisa na wengine washatishwa Sana Lakin msimamo wao Ni ule ule .

Hoja hapa Ni Nan mwenye kuamua idad za kura ziende chama gan walimu mnawaonea tu
Matokeo hubandikwa ukutani kwenye kituo cha kupigia kura
 
nyie walimu ndiyo maana bashite alisema atawatia viboko vya kwenye makalio.
Baada ya kusema yuko wapi saiz? Hii kada huwez kuidharau ukabak salama ,Leo hii unajua kutype uharo kisa hii hii kada ,jipige kifuani alafu sema Mimi Ni zwazwa natukana walionifanya nijue hata kuandika hapa jf.
Wote wanaowabeza walimu hawana tofaut na wasalit ,yaan unamsaidia mtu akishafanikiwa anakuona takataka, uzur hii kada ndio imebeba kada zote unazoona ndio za maana ,coz bila mawalimu hizo kada zingine zisingekwepo Leo hii ,iwe kada ya Sheria ,doctor,uhamiaji,jwtz,askar,sijui kada gani haijapita mikonon mwa mwalimu mkubwa jalala acha wajinga muendele kumponda mwalimu na kumshusha thamani Ila ndio hivyo ashakuwa mzaz wako na Hana budi kukubali kuwa jalala.

Vuta picha kipindi unatokwa na kamasi Ni huyu huyu mwalimu alikupa namna ya kupenga kamasi namna ya kuanza na a, e,i, o,u had Leo hii na wewe upo jf unajimwaga ,sikumbuki Kama Kuna mwanasheria au doctor aliekufundisha kuandika na kuyajua yaliojificha ndani ya vitabu vingine ,ambapo baada ya kujua yalio kwenye vitabu vingine Leo unaona aliekupa huo ujanja Ni mjinga.
This is pathetic indeed.
 
Matokeo hubandikwa ukutani kwenye kituo cha kupigia kura

Na mawakala wa chama wakiwemo? Hata hivo Walimu hawajaanza kuendesha zoezi leo, wakati upinzani wapo bungeni walipitishwa na walimu ama wana sheria?
 
Matokeo hubandikwa ukutani kwenye kituo cha kupigia kura
dah kweli wewe ni kilaza wa kutupwa Tena Zaid ya Sana .
Haya ngoja nikupe mfano hai ,Mimi natokea mkoa wa mbeya wilaya ya Rungwe ,uchaguzi wa mwaka Jana nilibahatika kuwepo huko nyumbani Jimbo la Busokelo .
Matokeo ya kila kata za Hilo Jimbo Ni karibia mgombea wa upinzan some body Wakili Msomi Boniface Mwabukusi alikuwa ameshinda kwa kata nyingi kulinganisha na mgombea wa ccm some body Atupele na kila mtu alijua Mwabukusi ndie mshindi ,na waliosimamia kwa idadi kubwa Ni hao hao Walimu ,Ajabu Sasa Mkurugenzi akawa hataki kutangaza ukweli Hadi kupelekea matokeo ya mbeya jiji kutoka mapema wakat matokeo ya kajimbo kadogo kaliko megwa toka Rungwe kushindwa kutangaza matokeo kwa wakat had kuepelekea Mkurugenzi kutangaza matokeo usiku wa saa sita na mshinda akatangazwa yule wa ccm ,nadhan hata yeye hakuamin kilichotokea huyo wa ccm , Sasa kwa hapo mwalimu unamlaumu kwa lipi?

Acheni kuwaonea Walimu ,maana walimu hawana nguvu hiyo mnayoimba kila leo ,nadhan mmeona ndio sehemu ya kumalizia hasira zenu wakat ukweli mnaujua kabisa kuwa tatizo Ni tume na vyombo vya Dora vikishirikiana na serikali.

Hata walimu wakiamua wakae pemben bado chadema hawawez shinda Kama mnavyofikiria ,mkitaka uhalal wa yote haya pambaneni na katiba mpya hasa Ile ya walioba ,nadhan kidogo inaweza leta haki Ila sio hii ambayo rais anateua watu wa tume ,anateua jaji mkuu anateua kila aina ya watu ambao Ni lazima wawe upande wa mteuaji.
 
Wanataka kutobolea na katiba hii, wanaumwa
 
Bila shaka kwa nguvu na Muumba tu wazima na harakati za kujenga maisha yetu pamoja na taifa kwa ujumla.

Leo nikiwa kama Mwalimu kitaaluma, naomba nizungumzie madai, lawama na kuhusishwa kwa kundi hili adhimu na siasa za nchi yetu.

Kwa kuanza naomba mtambue, Walimu sio watumishi kada mali ya wanasaisa, walimu hatuhusiki na umiliki wa chama chochote cha siasa nchini, so far. Kumekuwa na lawama, chuki na maneno ya kejeri kutoka kwa makada wa vyama vya siasa hasa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenda kwa Walimu haswa linapokuja suala la uchaguzi mkuu hapa kwetu.
Ipo hivi; imeonekana mara nyingi walimu wakipewa nafasi za kusimamia uchaguzi mkuu, naomba mtofautishe, mamlaka pekee nchini zenye kusimamia hili zoezi ni NEC, POLISI na Wizara ya mambo ya ndani kwa ujumla, sio CWT wala chama chochote cha Walimu. Walimu sio wasimamizi, ni waendesha zoezi la kupiga kura, mwisho wa siku wao hufanya vile wanavyoelekezwa.

Vijana wa CHADEMA wamekuwa na kawaida ya kulaumu Walimu kuwa wanahusika na wizi wa kura ama kuisaidia CCM kuingia madarakani, jambo ambalo linashangaza, na linasikitisha ukizingatia CDM ndio chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, na mnajua ilivyo hadhi kubwa kuwa chama kikuu cha upinzani, hii ni sawa na kusema “chama mbadala wa chama tawala” kina kuja na hoja hii kwa kweli.

Walimu tunapata nafasi nyingi za kusimamia zoezi kulingana na wingi wetu katika kada, vile vile uzoefu wa kuratibu shughuli zinazohusisha watu wengi, uandishi na uzoefu katika kutoa maelekezo, mambo ambayo zoezi la upigaji kura linataka. Suala la kutumika na CCM halihusishi waalimu kaa sababu hakuna semina ya walimu kama walimu peke yake ya namna gani kura ziibiwe kituoni, ama waraka rasmi kwa Walimu kuhusu wizi wa kura. Na endapo itatokea mwalimu kama msimamizi wa kituo akafanya hivyo asihusishwe kama mwalimu kwa sababu hakutumwa kama Mwalimu, ualimu unahusiana vipi na wizi wa kura? Ni mtaala? Miiko ya kazi? Ama ni kitu gani.

NIONAVYO MIMI

CHADEMA huitumia hii hoja kwa namna mbili.
1.SABABU YA KUPATA MTAJI WATU KISIASA Kwa kuwa Walimu ni kundi kubwa, wataka wawa “provoke” kwamba wao ndio sababu ya matatizo yote nchini pamoja na matatizo yao wenyewe lengo likiwa ni kuwafanya wawe subjects wao ambapo kwa madai haya maana yake Walimu kuyakataa itabidi wafanye matakwa ya CDM, kwa neno la kimombo wanaita “Blackmailing” yaani jitihada za kuwa prove wrong watu, Walimu wawape favor CDM.

Ndugu zangu CDM, kama kweli mnataka kuwa chama tawala nchi hii, acheni siasa za namna hii, changamoto katika utawala zipo kila kona duniani, fanyeni siasa yenu kama wanasiasa mnao jielewa, kumbukeni kundi mnalojaribu ku mess up nalo ni kubwa mno, lawama zikiwa nyingi zinakuwa sehemu ya maisha yetu, tukiwazoea hamtakuwa na mtaji wa watu huenda kama mnavyojaribu kutafuta kupitia sisi, dare not comrades!

2. KISINGIZIO BAADA YA KUSHINDWA UCHAGUZI
“Hata wakishinda wao, CCM itaunda serikali” nadhani mnamfahamu aliyesema hii kauli, kwa hiyo jueni kwamba mpo kwenye chi ambayo watu wana haki ya kupiga kura ila sio kuchagua viongozi, msilalamike lalamike hovyo kuwalaumu walimu as if sisi ndo tunaunda serikali, wapo walimu wengi tu makada wa vyama vya siasa ikiwemo chama chenu, amini usiamini kwa lawama hizi! (Sina neno)

”CCM itatumia dola kubaki madaraki” vile vile mnajua aliyesema hii kauli, hakusema CCM Itatumia Walimu kubaki madaraki, mkishindwa kuelewa na hapo basi hamjaamua tu na mnachuki na sisi za bure tu.

Mwisho kabisa naomba niwasihi muweke hadharani sera zenu kwa mtindo wa kuzidisha kutoa elimu zaidi hasa maeneo ya vijijini ambapo kuna ngoma kubwa sana ya chama tawala. Msiishie kutukana walimu, mbaya zaidi hamtulipi mnazidisha hasira tu.

Nawasilisha.
Mimi ni mwl nikwambie tuu Sisi walimu tunahusika kuiba na kuchachua kura, na nimeshiriki chaguzi zote za 2010, 2015 na 2020 uchaguzi tulioiba kura wazi wazi ni uchaguzi wa meko, watumishi wa tume wamepiga kura zaidi ya tano kwenye vituo wanampigia meko, wanafunzi wasioandikishwa waliwapigia kura watu wengine walioandikishwa. Kwa ufupi tunasitahili lawama.
 
Back
Top Bottom