Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,298
- 3,061
Tatizo la chadema ni kuwa hawataki kuambiwa ukweli. Ukweli kwao ni usaliti
Na ndivyo inavyostahili kipindi hiki kuliko wakati wowote.Marafiki wa maadui zetu na mifumo yao hawatapata nafasi.
Majenerali wakuu hawabadilishwi katikati ya vita
Kama CCM mna uchungu sana wachukueni mnaowataka wakagombee huko kwenu.Msitupangie aina ya silaha za kuwapiga nazo ninyi.
Mtaishia kulalama tu na kupoteza muda.Hampati kitu.So, go home
Ben, pamoja na kujitahidi kujibu maswali na hoja za wadau humu ndani huku hoja nyingi ukizipinga but they have a point, kuna watu wanaongea ukweli humu but wanashindwa kuuprove ukweli wao kwa kuwa hawana ushahidi mkononi lakini wanaongea kitu ambacho kipo na ambacho jamii inakiona, pamoja na kujitahidi kukitetea chama chako humu, jitahidi pia na kuyafikisha mawazo haya kwa uongozi wako wa juu ya myafanyie kazi.
kumbuka Beni, migogoro ikitumika vizuri itawajenga lakini pia ikitumika vibaya itawabomoa!
kazi kwenu!
Chanaga united usipotetea wakula wapi utakula wewe....ukiwa mnafiki ujanani uzeeni utakuwa mchawi kabisa...sio wewe uliyemchafua ZZK hapa jamvini?? Waislam wanamssemo mmoja katika moja ya aya za Quran Isemayo SEMA UKWELI HATA KAMA UNAUMA
Wewe hupiganii taifa lako kwa namna yoyote ile bali upo humu kulinda mkate wako hasa baada ya kuchukua nafasi ya Ludovick. Pia hupiganii chama chako bali unapigania kakikundi kadogo ka viongozi wa juu ambao kwa namna moja au nyingine una nasaba nao au unanufaika kutokana na wao kuwa viongozi
Karibu vyama vyote vya siasa nchini hususani vile vikubwa vimekuwa vikitumia hoja ya VIKAO HALALI VYA CHAMA kama njia ya kubana wanachama wake kutoa maoni; au labda kwa usahihi, kuwazuia kueleza maovu ya chama. Katika hili, CHADEMA ndo sio wastahimilivu hata kidogo; heri ya CCM wanavumulia wanachama wao katika kile kinachoitwa kutoa habari za chama bila kupitia viako halali vya chama. Kwa bahati mbaya kabisa, wana-CHADEMA wa kawaida nao wameingia kwenye mtego huu, kwamba inapotokea mwana-CHADEMA ameeleza mambo yanayowachukiza viongozi nje ya utaratibu wa kawaida; wana-CHADEMA hawa wa kawaida watakuja juu na kumtuhumu mwenzao kwa kumuita majina mbalimbali ya hovyo hovyo!
Wapenzi, wanachama na mashabiki wa kawaida wa vyama vya kisiasa nadhani wanatakiwa kuamka na kugundua kwamba hiki kinachoitwa kwamba ni VIKAO HALALI VYA CHAMA ni ghiriba tu za viongozi wa vyama hivi ya kutaka yale mabaya ya vyama yasisemwe! Hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA kwa hakika kina jina la kuvutia na ndio maana hata wale wapenzi na wanachama wa kawaida nao wamekuwa wakiimba nyimbo hizi za VIKAO HALALI VYA CHAMA! Hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA ni kama kile kingine kinachoitwa UTAWALA BORA ambao Watanzania wengi tumekuwa tukiupigia upatu bila kufahamu kwamba UTAWALA BORA ni kichaka cha maovu ya viongozi na watendaji mbalimbali! Utawala Bora hauwezi kuwa na manufaaa kwa wananchi ikiwa unakuwa practiced kwenye jamii isiyo na maadili kama ya kwetu!
Sasa turudi kwenye hiki kinachoitwa kwamba VIKAO HALALI VYA CHAMA!! Hivi leo hii tuseme kuna mwanachama ana uhakika kabisa kwamba (say) Dr. Slaa au Freeman Mbowe amefanya ABC; tena jambo la fedheha kabisa! Hivi kweli mwanachama huyo anaweza kuwa na Ujasiri wa kusimama mbele ya VIKAO HALALI VYA CHAMA na kutamka waziwazi maovu hayo? Kama atakuwa na huo ujasiri, ni wanachama wangapi wanaweza kuwa na huo ujasiri wa kumchana LIVE mwenyekiti au katibu wa chama ambao tayari wamesha-prove kwamba hawana uvumilivu dhidi ya maoni hasi!
Kwa upande wangu, sina tatizo na hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA lakini nadhani ni busara watu tukaangalia ni nani wanapaswa kuachiwa kuimba nyimbo hizo! Mwacheni Mbowe, mwacheni Dr. Slaa au watu wengine kama hao waimbe hizo nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA kwani kutofanya hivyo ni kuhatarisha nafasi zao kwenye chama! Sitaki kuamini kwamba kutahatarisha uhai wa chama unless kama tunataka kusema CHADEMA ni MBOWE au SLAA! Wakati sioni tatizo kwa akina Mbowe kuimba nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA lakini kwa mpenzi, shabiki na mwanachama wa kawaida ambae wala hajui hata viatu anavyovaa Dr. Slaa ni rangi gani au vile vya Mbowe; basi kuimba nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA ni uzuzu! Ni uzuzu kwa sababu whether you like it or not; kamwe hutaweza kufahamu ukweli mchungu unaokihusu chama chako kupitia hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA unless if you're prepared whether for bad or worse, wewe na chama chako tu kama ilivyo kwa Waislamu au Wakristo na dini zao!!
Hawa watu na wanachama wa kawaida nadhani ingekuwa ni busara zaidi kujadili contents za tuhuma kuliko kung'ang'ana na VIKAO HALALI VYA CHAMA ambavyo hata wao wenyewe hawahudhurii! Hili ambalo kwa wana-CHADEMA wanajidanganya kwamba eti ni kutowafumbia macho wasaliti ni ujinga mtupu, sana sana lina-prove ni jinsi gani UONGOZI WA CHADEMA unavyoandamwa na vivuli vya uoga! Swali la VIKAO HALALI VYA CHAMA linatumika kama njia ya kuwaziba watu midomo! Ni ajabu CCM iliyojaa ma-conservatives angalau inavumilia maoni makali ya wananchama wao yanayotolewa dhidi ya chama chao na wakati mwingine dhidi ya viongozi! Hivi ni nani asiyejua kwamba Nape na Samuel Sitta walikuwa on transit kuelekea CCJ? Hata hivyo waliwavumulia…. itakuwa ni ujinga kudhani kwamba uongozi wa juu wa chama na serikali hawakufahamu harakati hizo za akina Sitta!
Kuna Columnist mmoja kwenye gazeti la Raia Mwema anajiita MSOMAJI RAIA! Huyu jamaa huwa anaiponda wazi wazi serikali ya Kikwette! Na kwenye baadhi ya makala zake; huwa anamponda hata JK mwenyewe! Lakini what's so interesting, MSOMAJI RAIA ni wa ndani katika serikali ya Kikwete; namfahamu! Sasa ikiwa mtu wa kawaida kama mimi nafahamu who's MSOMAJI RAIA, itakuja kuwa KIkwette mwenyewe ambae amezungukwa na wana-intelejensia kadhaa kila Idara?! Hata hivyo, Kikwete anamvumilia MSOMAJI RAIA!
Huku Uswahilini kuna tabia Fulani imezoeleka kabisa! Unakuta mzazi analetewa mashitaka kwamba kijana wake amedokowa/ameiba mahali, au labda nyumba ya mtaa wa pili. Ni kawaida kukuta wazazi wanakuja juu, mithili ya moto wa kifuu kwamba mtoto wao anasingiziwa; KATU HAWEZI KUWA MWIZI. Wapo wanaofikia kusema hizo ni chuki tu utafikiri mzazi husika huwa anatembea na mwanae kila mahali! Siku wanakuja kutanabahi, anakuja kusikia kwamba Mwanao yupo Jela au kapigwa moto! Wazazi wa aina hii ndo mashabiki wengi wa CHADEMA walivyo! Wakati si Dr. Slaa wala Mbowe wana sifa za kuwa Malaika lakini wapenzi na mashabiki wa CHADEMA wanataka kufanya kama hawa watu ni MALAIKA ambao tunaambiwa huwa hawafanyi makosa!
Lililo wazi ni kwamba, mwanadamu pekee asiyefanya makosa ni MAITI! You'll never be free of mistakes unless if you're dead!
Hoja kuu ya post yangu ni kuwa Ben hayuko jukwaani kuwajibiwa viongozi wake wakuu wa chama hoja zinazoelekezwa kwao..yeye anatoa maoni yake binafsi.
Suala la kusema Ritz na wenzake kuwa si wanachama wakawaida ndani ya chama chao...haihalalishi hoja wanazojibu hapa jukwaani zikiwalenga viongozi wa chama chao kuwa kauli za viongozi wa chama tawala.
Vinginevyo uueleze ulimwengu kupitia JF kuwa Ritz na wenzake ndiyo viongozi wakuu wa Chama cha CCM....
Kwamba kila nyumba na utawala wake ni jambo lisilo na shaka hata punje, na labda kwa nyongeza tu, hata kwamba kila utawala una sheria na taratibu zake si jambo linalohitaji mjadala; kwavile hivyo ndivyo hasa ilivyo! Kwa bahati mbaya mkuu wangu, naona nawe ni kama umejikita kwenye suala la Mwigamba; anyway, wengi akili zao wameelekeza huko ingawaje nilichosema mimi ni ghiriba ya viongozi wetu kutumia kile kinachoitwa vikao halali vya chama kama njia ya kuwafunga watu midomo! Lakini kwa upande mwingine, sina shida sana na hao viongozi wanaojificha kwenye kichaka cha Vikao Halali Vya Chama pamoja na Katiba; shida niliyonayo mimi ni hawa watu wa kawaida kushabikia nyimbo hizi bila kufahamu nini hasa malengo yake! Wengine ni vijana wadogo lakini huku wakikazana kujifunika gubi gubi kwa koti la Conservative Thinking!Kila nyumba na utawala wake.Hebu,nieleze katika jamii yetu nani alimvumilia Mfanyakazi wa nyumbani/Housegirl ambaye anatoa siri za nyumbani kwake kwa majirani zake,wafanyakazi wenzake,wakristo wenzake,waislam wenzake,wanasimba wenzake au wanayanga wenzake???
CHADEMA si chama cha siasa bali ni saccos ya Mbowe na DR Slaa
na ndicho nafikiri alichomaanisha bwana ben saanane , tukiendelea tukisikiliza hizi porojo za humu hawa watu wanalo jambo, nalo ni kutusambaratisha kwa mambo madogo madogo , tujipange na tusonge mbele. bwana ben saanane ni kweli usiopingika kuwa huwezi ukabadili makomandoo katikati ya uwanja wa mapigano , mtashindwa tu na mtarudishwa nyuma kwa hili tutawajua chadema wa kweli na fake , mungu saidia chadema , saidia ukombozi huu tunaoutafuta katika kuikomboa tanzaniaMkuu hapo kwenye number nne wala hawataki kupaongelea....shida ya ccm kwa sasa ni chadema .. Hawashughuliki na chama chao...na ukiangalia kelele nyingi zisizo na maana kuhusu uendeshwaji wa chadema ni za wana ccm au washabiki wa ccm.... Cuf wala hakuna anayewaongelea wakati lipumba.na seif sijui mwaka wa ngapi huu wako kwenye hizo nafasi za kudumu
Hapa kuna jambo la ajabu kidogo kutoka kwa miongoni mwa wana-CHADEMA! Inaelekea wengi wao wanaishabikia hali hiyo, kwamba uchaguzi wa ndani usifanyike hadi general election ipite! Kama kawaida yao, wanaipaka mafutaka kauli yao ili mradi tu kuihalalisha; kwamba eti makamanda hawabadilishwi wakati wa vita! Lakini cha kushangaza, hao ni wale wale ambao walimtaka Mwigamba atumie vikao halali vya chama; bila shaka vikao halali kwa mujibu wa katiba huku wakisahau kwamba kutofanya uchaguzi 2014 itakuwa ni kuibananga katiba hiyo hiyo ambayo wanamtuhumu Mwigamba kuivunja! VERY CONTRADICTING!Chama ni chama,na viongozi wake ni binadamu wana mapungufu kwa hiyo kukosolewa sio kitu cha ajabu,kama chadema haitafanya uchaguzi hadi uchaguzi mkuu upite 2015 je endapo ikipewa inchi na watanzania wakati haijajipanga hapo ndio mwanzo wa mgogoro mkubwa zaidi.hivi sasa tu hali iko hivyo je baadae? Kama sasa mwanachama akitoa maoni mambo yanakua hivyo baadae ikipewa ikulu mwanachama akitoa maoni nadhani atakuja wekwa ndani kwa muda usiojulikana kabisa.