BOB LUSE
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 3,738
- 3,198
Kwa kiongozi makini kipindi hiki cha utawala wa Magufuli ni vizuri ukawa mwangalifu kabla hujatoa kauli yoyote dhidi ya Magufuli. Ameweza kukongo mioyo ya watanzania wengi na kufanya mengi yaliyokinyume na chama chake na mtangulizi wake Kikwete.
Pia ana mapungufu kadhaa katika utendaji wake wa kazi mfano hujuma za chaguzi za mameya,kushughulikia waliosaidia upinzani na kukwepa kushughulikia swala la Zanzibar.Haya mambo wananchi wanaona na kuyasikia lakini mwangwi wake ni mdogo ukilinganisha na mema anayoendelea kuyafanya Magufuli.
Hivyo viongozi kutoa kauli za jumlajumla kuwa wanaotumbuliwa majipu wanaonewa na sheria hazifuatwi hazipaswi kuongewa na upinzani/CDM badala yake waongelee kupata katiba nzuri yenye sheria/kanuni zitakazo wabana zaidi wahujumu uchumi na kumpa madaraka Raisi kuendelea kuwafuta kazi hawa wahujumu raslimali zetu.
Mbowe na wenzio someni alama za nyakati kwa sasa mwanasiasa/mtu yeyote atakaye mlaumu Magufuli hatafanikiwa,bali atakaye ungana naye atafanikiwa.Mabadiliko mliyokuwa mnayahubili ndio wananchi wanataka wayaone na Magufuli anawapa kwa vitendo,japo anakanyaga baadhi ya watu/vyama vya siasa mkiendelea na lawama wananchi mnawapa taswira kuwa hata mngekabidhiwa nchi mngeleta mambo ya kujuana msingewezi kumudu anayofanya Magufuli.
Ni hayo tu kwa leo.