CHADEMA yamtaka Rais Magufuli azingatie sheria kwenye utumbuaji majipu

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Vicent Mashinji, wakati alipokuwa akifungua kongamano la Baraza la Vijana CHADEMA (Bavicha) na Umoja wa wanachadema Vyuo vikuu (Chaso) mjini hapa.

Dk. Mashinji alisema kuwa tangu aingie madarakani Rais Magufuli amekuwa na utaratibu ambao umepewa jina la utumbuaji majipu ambao amekuwa akiuendesha bila kufuata sheria za nchi.

Alisema kuwa pamoja na kuwa CHADEMA wanaunga mkono kitendo cha kuwashughulikia mafisadi pamoja na watumishi wasio timiza majukumu yao ipasavyo lakini hawakotayari kuendelea kushuhudia ambavyo amekua akivunja sheria za nchi.

“Watumishi wengi wamedhalilishwa na serikali hii ambayo imekuwa ikitumia mabavu kuwawajibisha watu bila kufuata sheria za nchi,” alisema Dk, Mashinji.

“Suala la rushwa katika nchi ni jambo la kimfumo ambapo kila unapoona kunamtu katumbuliwa kwaajili ya rushwa basi kuna idadi kubwa ya watu ambao wanashiriki katika rushwa hiyo,” aliongeza Dk Mashinji.

Aidha, alisema kuwa utaratibu wa Rais kuwatumbua watumishi kwenye mikutano ya hadhara kwa kutumia ushabiki wa wananchi hauwezi kulisaidia taifa kufanikiwa katika kuwaletea mabadiliko ya kweli wananchi wake.

“Magufuli ametumbua watumishi wengi sana tangu aingie madarakani lakini niwaulize sukari imeshuka bei au mchele umeshuka bei lakini kila siku tunasikia watu wametumbuliwa bila kuwa na tija kwa taifa,” alisema.

Aliwataka vijana wa vyuo vikuu nchini kuungana na CHADEMA katika kuhakikisha serikali inaruhusu kuonyeshwa kwa vipindi vya Bunge moja kwa mpja kama ilivyo kuwa hapo awali.

“Bunge maana yake ni mkutano wa hadhara ambao wote tunatakiwa kushiriki lakini kutokana na udogo wa eneo wanakwenda wawakilishi wetu lakini na sisi tunatakiwa tufuatilie kupitia runinga zetu moja kwa moja ili tuweze kujua kinachofanywa bungeni na wawakilishi wetu,”alisema.

Pia aliwataka vijana kuacha ushabiki wa kushabikia siasa bali waikosoe serikali ili iweze kufanya kazi ambayo ni kuwaletea maendeleo wananchi wake kwakua huo ndio wajibu wake.

Akizungumza na wenyeviti wa CCM wa Mikoa na Wilaya Ikulu, Rais Magufuli alisema wanaotetea watu wanaotumbuliwa na wao ni majipu hivyo ataanza kuwachunguza.

Alisema inasikitisha kuona watu wanatetea watumishi ambao wamekuwa wakiwaibia watanzania miaka mingi lakini wanapofukuzwa kazi wanalalamika.

“Kama wamekuwa wakiwaibia wananchi hadharani nasisi tutawafukuza na kuwatangaza hadharani, inasikitisha kuona baadhi yetu tunatetea watu wanaofukuzwa kazi,” alisema Rais Magufuli

CHANZO: Nipashe
 
CHADEMA imeanza kurudi tena kwenye siasa za uanaharakati baada ya mafanikio ya kisiasa chini ya Dk. Slaa.

Moja ya msingi wa uanaharakati ni kupinga kila jambo na kulalamika sana bila kutoa majawabu. Ni sawa na mtoto anaelalamika sana au kulilia chakula wakati hafahamu hata changamoto za upatikanaji wake.

Dk. Slaa alikuwa ameishakivusha katika hizi siasa za uanaharakati na kuanza kujipanga kama chama kinachosubiri kuaminiwa na wananchi wengi ili kupewa nchi.

Lazima wajitathmini kisiasa au watajikuta wanaendelea kudharaurika kwenye kundi la watu wenye fikra pana ambao ndiyo wapiga kura wengi.

US President, Abraham Lincoln once said, ‘’Better to remain silent and be thought a fool than to speak out and remove all doubt’’.
 
Hivi nyie watu mnalipwa mini na ccm kiasi cha kujitoa akili kiasi hicho au ndo izo 700 kwa siku yani kweli bora mavi kuliko ccm kwasababu mavi unaweza kufanya mbolea na kuishabikia ccm inahitaji digrii nying za ujinga yan mpaka kizazi bado kuna watu wanaiunga mkono ccm hama maboya hayaishi!!
 
Wewe ni bonge la mnafiki na mzushi, hufai kuigwa katika jamii. Kila thread yako ni ya kipuuzi nafuu ya wanafki wenzio wa gazeti ya raia Tanzania na ya udaku
Inashangaza unasoma kila mara thread za mnafiki na mzushi. Hudhani kama wewe ndiyo una matatizo makubwa kwa sababu watu wenye fikra pana wanafahamu wazushi na wanafiki hupuuzwa. Ulitakiwa uachane na hizi thread za mzushi na mnafiki.
 
Mkuu niliwahi kumuona mama mmoja kavaa kanga imeandikwa " SHAKUBIMBI MUOGOPE" nikawa sielewi maana yake.
Lakini baada yakumsoma sana huyu jamaa ndio nimeelewa
Ninashukuru kwa kunisoma sana!

Kwa kunisoma sana unatimiza malengo yangu ya kuhabarisha na kuelimisha jamii ya wanaJamiiforums.

Keep it up, dude!
 
Hivi nyie watu mnalipwa mini na ccm kiasi cha kujitoa akili kiasi hicho au ndo izo 700 kwa siku yani kweli bora mavi kuliko ccm kwasababu mavi unaweza kufanya mbolea na kuishabikia ccm inahitaji digrii nying za ujinga yan mpaka kizazi bado kuna watu wanaiunga mkono ccm hama maboya hayaishi!!
Umesoma kichwa cha thread na kuanza kumwaga maneno katika msingi wa jazba.

Soma kwanza habari yote ili uelewe chanzo cha habari.

Don't shoot the messanger!
 
Wewe ni bonge la mnafiki na mzushi, hufai kuigwa katika jamii. Kila thread yako ni ya kipuuzi nafuu ya wanafki wenzio wa gazeti ya raia Tanzania na ya udaku
Unalialia nini kijanga,hayo sio ya mleta mada ni kwa mujibu wa gazeti la nipashe lililomnukuu Mashinji,kwa kweli najuwa hujafurahishwa na maudhui,Mashinji anaunga mkono ufisadi hadharani.Pole dogo hizi ndizo siasabiashara za mbowe.
 
Hivi nyie watu mnalipwa mini na ccm kiasi cha kujitoa akili kiasi hicho au ndo izo 700 kwa siku yani kweli bora mavi kuliko ccm kwasababu mavi unaweza kufanya mbolea na kuishabikia ccm inahitaji digrii nying za ujinga yan mpaka kizazi bado kuna watu wanaiunga mkono ccm hama maboya hayaishi!!
Jikite kwenye hoja wacha kuyumbayumba kama mlevi,ni sahihi mashinji kutetea mafisadi?
 
Kwani toka utumbuaji umeanza faida yake ni nn imeleta impact gani kwa mwananchi wa hali ya chini?
 
Mkuu niliwahi kumuona mama mmoja kavaa kanga imeandikwa " SHAKUBIMBI MUOGOPE" nikawa sielewi maana yake.
Lakini baada yakumsoma sana huyu jamaa ndio nimeelewa
Umechakazwa tena,mashinji anatetea mafisadi,dah chadema ni genge hatari sana.Badala ya kujibu hoja unamkumbatia bavicha mwenzio kujiliwaza.Jikite kwenye mada dogo...je mashinji kutetea mafisadi ni sawa?
 
Kwani toka utumbuaji umeanza faida yake ni nn imeleta impact gani kwa mwananchi wa hali ya chini?
Kama wewe au ndugu yako katumbuliwa utafurahi?...lakini tumeona barabara zikijengwa,dawa zikiwekwa,madawati yakitengenezwa na uwajibikaji ukiongezeka...wewe cheza pool tu.
 
sioni uhusiano wa kichwa na content,hapo ndio dhana kamili ya lengo la mleta mada linapotimia.
 
Ukiwa Muongo usiwe msahaulifu nimeweka full hutuba yote ya katibu mkuu kupotosha umma si jambo jema kabisa
 
Back
Top Bottom