Mada hii haujaitendea haki kabisa kwa sababu inajulikana kabisa kwamba CDM, ndicho chama mbadala kwa CCM, Na kinakubalika sana kwa sasa kuliko vyama vyote vya upinzani. Mambo mengi yako wazi kwa mfano unaweza kuangalia matokeo ya kura za uchaguzi wa Uraisi Mgombea wa CUF Aliachwa mbali sana na Dr Slaa wa CDM. Mbili CDM ni chama chenye Madiwani wengi Tanzania kuliko chama chochote cha Upinzani. Tatu CDM ni chama chenye wabunge wengi Tanzania kuliko chama chochote cha upinzani. Nne Cdm Ni chama kinachokubalika kwa sehemu kubwa ya Tanzania kuliko vyama vingine vya upinzani. CUF, ni chama chenye msomi mzuri sana Ndugu Prof Lipumba lakini kinakubalika sana PEMBA,LINDI,MTWARA, Na Katika baadhi ya maeneo fulani fulani.Unaweza kujiuliza Maeneo kama Kigoma ni CHADEMA NA NCCR Mageuzi.Na nafikili CUF wanahaja ya kujiuza zaidi ili waeleweke kwa jamii kubwa ya Tanzania. Hata Tabora CDM wako juu. Hata Dar Es Salaam, CDM wako juu ya CUF. Enzi za CUF kutamba zilikwisha ile miaka ya 2000, hadi 2005. Kuanzia 2010 ni CDM. CDM kwa taarifa yenu wana wabunge wengi zaidi mkoa wa Shinyanga kuliko hata Kilimanjaro. Kilimanjaro ina wabunge watatu wa CDM sawa na Mwanza. Kusema kwamba CDM inaishia Himo ni mzaa, utani,upuuzi,propaganda,ukipofu, ghiliba na ujinga uliopitiliza. Na nafikili watu wenye timamu hawawezi kusema hili, ni wale hamnazo tu. Kwa sababu vielelezo vyote vipo wazi. Na kama unabisha CDM NA CUF wapambanishwe katika majiji haya manne ya Tz kimikutano uone.