Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,112
Mbegu za fikra za kidini mnazopandikiza kwa watu na kuzirithisha kwa watoto wenu iko siku mtalia na kumwaga damu yenu au ya watoto wenu huku mkikumbuka maneno Mwl.Nyerere kwamba sisi ni Watanzania na tunatakiwa kujivunia hilo kuliko Ukristo au Uislamu.Michezo ya kisiasa kwa kuhusisha suala la imani ni kupandikiza mbegu za vita,ubaguzi,dharau,kutengana na kutokuaminiana.Enyi wanachama wa ccm,cuf na CHADEMA badilikeni kwani aina ya propaganda hizi ni hatari kwa ustawi wa jamii.Wala msijione wajanja kwa kujenga hoja za kuhoji udini au kujibiwa kidini kwani ni kuhatarisha amani kwa miaka ijayo.