Chadema: Mwajibisheni Shibuda - A golden opportunity

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,358
6,422
Kwa matamshi yake kuwa wanaopinga Posho ni madomokaya na hiyo ikiwa ndiyo sera ya CDM, Sasa CDM wanaweza kumfukuza shibuda. Yupo nje ya bunge anapinga sera za chama chake, wanaweza kumwajibisha kama chama kwa utovu wa nidhamu kama kanuni za chama zina kipengele hicho. Hapa kinga ya bunge ilivyoainishwa kwenye katiba kifungu cha 100 hakimlindi hata kidogo. Yupo nje ya bunge na anakashifu sera za chama chake. kama kuna provision ya hivyo katika katiba/ kanuni za nidhamu za cdm. This is an opportunity to flush him out of cdm
 
CDM wamekuwa wakwanza kila mara kutaka magamba wawe wepesi kufanya maamuzi magumu ilhali wao wenyewe wanaogopana,si mara ya kwanza Shibuda kupishana na viongozi wake,alishawahi kuita sitting allowance UJIRA WA MWIHA!akipigia chepuo kuwa ni stahili halali kwa wabunge!CDM kuweni mfano kwa kuchukua maamuzi magumu,kubalini mpoteze jimbo moja kwa kumfukuza katika chama Shibuda ili sisi ambao hatujashawishika na siasa za bongo tubadilishe mawazo angalau mwaka 2015 tukasimame katika vituo vya kupigia kura kwa mara ya kwanza!Dr Slaa mbona mnakuwa mabubu katika hili?
 
kauli yake haina madhara kumbuka shibuda ni mtoto yatiima aliokotwa tu bara barani hana itakadi za cdm bado mdogo mawazo yake bado yapo kimagambamagamba hajui afanyalo,yeye ni mtaji tu kwa cdm hujui anongeza ruzuku? cdm inajuwa inachofanya
 
hakuna kitu kama hicho'atapiga kelele mpaka 2015'shibuda ni kama mke mwenye mume mwelewa'kazi kwake

Jenga hoja usiseme hakuna kitu kama hicho. mimi nimetoa hoja ya kisheria kidogo kuwa kinga ya bunge sasa haitamlinda shibuda kwa vile anatoa matamshi ya kukikashifu chama wakati yupo nje ya bunge. Sera ya chadema ni kupinga posho yeye anasema ni madomokaya, amekosa nidhamu!!! Kifungu cha 100 cha katiba ya URT hakitamsaidia. nakumbuka wakati ule alipofanya utovu wa nidhamu akiwa bungeni tulitoa maoni kuwa mkimfukuza akienda mahakamani atawashinda maana analindwa na kinga ya bunge. Sasa yupo nje ya bunge anakashifu chama. Ndio maana akina Lema wako mahakamani maana walitenda hayo wanayotuhumiwa wakiwa nje ya bunge and consequently hawana kinga ya Bunge. Toa maoni yako on those legal lines utueleweshe
 
There is a lot of logic in your statement. Nilikuwa sijui hilo ndio maana nikapost hiyo thread. kama ruzuku zinakwenda kwa number of wabunge then, you need to think twice before flushing him. Ingawa kwa maoni yangu ningekubali kupoteza hiyo ruzuku yake kulinda maamuzi ya chama.
 
Kwa matamshi yake kuwa wanaopinga Posho ni madomokaya na hiyo ikiwa ndiyo sera ya CDM, Sasa CDM wanaweza kumfukuza shibuda. Yupo nje ya bunge anapinga sera za chama chake, wanaweza kumwajibisha kama chama kwa utovu wa nidhamu kama kanuni za chama zina kipengele hicho. Hapa kinga ya bunge ilivyoainishwa kwenye katiba kifungu cha 100 hakimlindi hata kidogo. Yupo nje ya bunge na anakashifu sera za chama chake. kama kuna provision ya hivyo katika katiba/ kanuni za nidhamu za cdm. This is an opportunity to flush him out of cdm

Kwani sheria zinasemaje endapo Shibuda CDM watahamua kumfukuza? Nasikia kuna uwezekano wa serikali kumtetea mbunge aliyefukuzwa mahakamani? anayefahamu masuala ya kisheria ya kinga ya mbunge naomba atujuze wakuu?
 
Shibuda inabidi achunguzwe history ya ukoo wake upande wa baba yake.Huyu jamaa inawezekana kabisa 75% akawa siyo mtanzania.Anaonekana kama ni mamluki aliyetumwa na nchi yake kuja kudumaza maendeleo ya TANZANIA.Huyu cyo mwenzetu haaaata kidogo.
 
Jenga hoja usiseme hakuna kitu kama hicho. mimi nimetoa hoja ya kisheria kidogo kuwa kinga ya bunge sasa haitamlinda shibuda kwa vile anatoa matamshi ya kukikashifu chama wakati yupo nje ya bunge. Sera ya chadema ni kupinga posho yeye anasema ni madomokaya, amekosa nidhamu!!! Kifungu cha 100 cha katiba ya URT hakitamsaidia. nakumbuka wakati ule alipofanya utovu wa nidhamu akiwa bungeni tulitoa maoni kuwa mkimfukuza akienda mahakamani atawashinda maana analindwa na kinga ya bunge. Sasa yupo nje ya bunge anakashifu chama. Ndio maana akina Lema wako mahakamani maana walitenda hayo wanayotuhumiwa wakiwa nje ya bunge and consequently hawana kinga ya Bunge. Toa maoni yako on those legal lines utueleweshe

hoja gani tena mkuu?hapo nimemaliza yote!
 
Guys it seems you have a point but you can not analyse it logically......

hivi nani m'baya kati ya hawa? anayechukua posho na kukaa kimya, yaana anazipenda na hasemi kuwa anazipenda, huku sera za chama kiko -kinyume na hilo..

au m'baya huyu shibuda ambaye anachukua, anasema kuwa anazipenda na aliye-kinyume chake anatukana!

ukimfukuza shibuda anayesema, shart ufukuze na wengine wanaopokea posho na wako kimya!

au hao wabunge wa CDM wanaozipokea posho hawapingi sera za CDM??

usijibu swali hili...just skip!
 
CHADEMA lazima kidhihirishe ukomavu wa kuvumiliana!!!! Lazima kimvumilie Huyo Kibuda wao mpaka mwaka 2015! Ninachokijua ni kuwa amewaharibia wanaCCM wenzake ambao wangetaka kukimbilia CHADEMA baada ya kushindana na sera za Magamba wakati wa uchaguzi!!!!. Muacheni akae,aliropoke atakacho ila nyinyi andaeni Kamanda wa kushika jimbo hilo uchaguzi ajao halafu muone atakimbilia wapi! Shibuda anafanya hayo yote ili afukuzwe arudi CCM na kupokelewa kwa mikono miwili, lakini mwaka 2015 baada ya kura za maoni, CCM hawatampokea maana watakuwa wameisha mtengeneza mgombea mwingine!

Huyu adhabu yake siyo kumfukuza kwenye chama, bali ni kumtenga kwa kila jambo ndani ya chama hata vikao vya wabunge wa CHADEMA asiruhusiwe kuhudhuria! anatakiwa kuteswa kisaikolojia mpaka atakapoamua yeye mwenyewe kubwaga manyanga.
 
Kwa matamshi yake kuwa wanaopinga Posho ni madomokaya na hiyo ikiwa ndiyo sera ya CDM, Sasa CDM wanaweza kumfukuza shibuda. Yupo nje ya bunge anapinga sera za chama chake, wanaweza kumwajibisha kama chama kwa utovu wa nidhamu kama kanuni za chama zina kipengele hicho. Hapa kinga ya bunge ilivyoainishwa kwenye katiba kifungu cha 100 hakimlindi hata kidogo. Yupo nje ya bunge na anakashifu sera za chama chake. kama kuna provision ya hivyo katika katiba/ kanuni za nidhamu za cdm. This is an opportunity to flush him out of cdm

Hii post inaonesha wishful thinking ya maadui wa CDM na jinsi gani mbinu za kuingiza mifarakano ndani ya CDM zilivyowaishia. Tofauti kati ya CDM na CCM inapatikana kwenye mfano kama huu wa Shibuda, Japo Shibuda yupo responsible kwa chama chake ila the most ni kwamba yupo responsible kwke mwenyewe na waliompigia kura. Kama CCM iliamua kumuacha Shibuda 2010 kwa sababu alitamka atagombea urais na JK sidhani kama CDM watafuata njia hiyo.

Nadhani CDM siyo chama cha visasi kama CCM na hili ndilo linawafanya wawepo hapo walipo leo hii. Mafumbo ya Shibuda hayawezi kuamsha hisia za watu wanaofanya maamuzi kisayansi, ila yataamsha hisia za watu wanapenda majungu na fitina ambao ni utamaduni uliojengeka zaidi CCM kwa baadhi ya watu wanaoona bila siasa hawan njia mbadala ya kujipatia riziki na hivyo kujikuta wanaendekeza majungu na makundi.
 
hakuna kitu kama hicho'atapiga kelele mpaka 2015'shibuda ni kama mke mwenye mume mwelewa'kazi kwake

Acha unafiki wewe, bora ya Shibuda anasema wazi na anachukuwa posho! Kuliko hao unaowaona mashujaa wako wanasema hawataki posho halafu upande wa pili wanachukuwa posho sijui nani mnafiki hapo?
 
Kwa matamshi yake kuwa wanaopinga Posho ni madomokaya na hiyo ikiwa ndiyo sera ya CDM, Sasa CDM wanaweza kumfukuza shibuda. Yupo nje ya bunge anapinga sera za chama chake, wanaweza kumwajibisha kama chama kwa utovu wa nidhamu kama kanuni za chama zina kipengele hicho. Hapa kinga ya bunge ilivyoainishwa kwenye katiba kifungu cha 100 hakimlindi hata kidogo. Yupo nje ya bunge na anakashifu sera za chama chake. kama kuna provision ya hivyo katika katiba/ kanuni za nidhamu za cdm. This is an opportunity to flush him out of cdm
Kama wewe ni mwana CDM jaribu kuja na hoja za kujenga chama na si kubomoa, tufikirie ni kwa jinsi gani tutamfanya awe mwanachama mzuri kuliko kusubiri loop hole ili afukuzwe wewe unaiita golden chance, basi kama wangekuwa wanafuata ushauri huu au mitego ya aina hii ya kuwindana kasemea ndani au nje ya bunge wengi sana wangeshafukuzwa.
 
Angalau chama kiseme chochote kuhusiana na kauli hii ya shibuda! Amewadhalilisha wanachama wa chama chake na watz wote tunaozipinga hizi posho.

Kuhusu kumwadhibu, sina la kusema maana sijui kanuni, taratibu na sheria za chama chake, ila nashauri wamuache tu maana he seems to be domokaya than those who he thinks are!
 
MWANALUGALI said:
CHADEMA lazima kidhihirishe ukomavu wa kuvumiliana!!!! Lazima kimvumilie Huyo Kibuda wao mpaka mwaka 2015! Ninachokijua ni kuwa amewaharibia wanaCCM wenzake ambao wangetaka kukimbilia CHADEMA baada ya kushindana na sera za Magamba wakati wa uchaguzi!!!!. Muacheni akae,aliropoke atakacho ila nyinyi andaeni Kamanda wa kushika jimbo hilo uchaguzi ajao halafu muone atakimbilia wapi! Shibuda anafanya hayo yote ili afukuzwe arudi CCM na kupokelewa kwa mikono miwili, lakini mwaka 2015 baada ya kura za maoni, CCM hawatampokea maana watakuwa wameisha mtengeneza mgombea mwingine!

Huyu adhabu yake siyo kumfukuza kwenye chama, bali ni kumtenga kwa kila jambo ndani ya chama hata vikao vya wabunge wa CHADEMA asiruhusiwe kuhudhuria! anatakiwa kuteswa kisaikolojia mpaka atakapoamua yeye mwenyewe kubwaga manyanga.
Smart thinking and piece of advice!
 
hawa na uwezo wa kumfanya chochote shibuda kwa sababu ndani ya cdm kuna maovu zaidi ya hilo la shibuda na sio mara ya kwanza shibuda kuwapinga cdm, na hata hivyo mbona wapo wabunge kama mh.selasini na akonai walishalalamika kwenye vikao vya bunge kuwa posho iongezwe lakini hawakufanywa chochote??
 
Shibuda anapendwa na wabunge wenzake wa cdm si mafano. Ki ukweli posho ni tamu na cdm hawawezi kuiachia ccm tu wachukue posho hizo litakuwa piku la kisiasa
 
There is a lot of logic in your statement. Nilikuwa sijui hilo ndio maana nikapost hiyo thread. kama ruzuku zinakwenda kwa number of wabunge then, you need to think twice before flushing him. Ingawa kwa maoni yangu ningekubali kupoteza hiyo ruzuku yake kulinda maamuzi ya chama.

CHUACHAKARA, wewe kweli ni Great Thinker, maana hoja yako ya awali uliijenga vizuri sana kimantiki, kisheria na kimtazamo, lakini TOWNSEND alivyotoa hoja yake, umeitazama nakuona una ina logic na ukakubaliana naye, kisha ukatoa maoni yako. Mimi nimeona wewe ni tofauti na wachangiaji wengi humu, hawaangalia kabisa hoja za upande wa pili zaidi ya kushikilia misimamo yao. Hongera sana nimejifunza kitu kikubwa kwako.
 
Back
Top Bottom