CHADEMA msiwatenge wanaCCM waadilifu - Mbowe

CHADEMA msiwatenge wanaCCM waadilifu - Mbowe

Mbowe kawashikia kweli akili pro-chadema.
 
Mbowe inabidi abadilike sasa aachane na Mikutano ya Hadhara kwani Watanzania wengi sasa wameshaelewa chanzo cha umaskini wao ni nini,Wanajua ufisadi unaoendelea hapa Nchini unaofanywa na MaCCM.Anachotakiwa kufanya sasa ni ku-channel financial resources zaidi katika Maofisi ya Mikoani na Wilayani,Kwenye Tarafa hata Kata na Vijiji,Wazitumie hizo ofisi kubuni miradi ya kimaendeleo wakishirikiana na Wananchi wa maeneo hayo,Wazitumie hizi ofisi katika kunadi Sera na Mawazo ya Chama na namna Chama kilivyojiandaa kuchukua Nchi.Nchi ina changamoto nyingi mno za kijamii,kiuchumi na za kiusalama na inaonekana kabisa CCM wameshindwa kukabiliana na hizi changamoto,Sasa ni juu ya CHADEMA kuanza kuwaambia Watanzania namna walivyojiandaa kukabiliana nazo.Ni vizuri Watanzania wakaanza kuijua CHADEMA kiundani zaidi kupitia hivi vitu watakapokipenda hawatarudi nyuma tena.Pia ni muhimu kwa CHADEMA kuziimarisha ofisi za Mikoani ili kiweze kujenga mtandao mpana wa Kichama utakaosaidia CHADEMA kushinda katika Chaguzi mbalimbali.

wazo hili ni zuri kwa kweli kwa sura kama mbili hivi, au hata zaidi: kwa upande mmoja litaimarisha chama hiko, lakini pia hata chama kikikosa nafasi ya kushika dola mipango iliyobuniwa inaweza kuvuja chama chenye ridhaa kushika dola kitaijua mipango hiyo kinayafanyia kazi mawazo hayo ambayo yatakuwa yameibuliwa huko kwenye mitandao ya vijijini na kwingineko. ni njia ya kuutumikia umma vilevile. kamata salute mkuu!
 
Ikumbukwe kuwa huyuhuyu Mbowe ndiye alisema wahamiaji wasipewe madaraka, leo anasema wasitengwe. Maamuzi ndani ya briefcase ya Mbowe...

Mbowe hajakosea yuko sahihi, ila huyu mkuu ZeMarcopolo ndie kachanganya Kati ya wanaccm na wahamiaji wameingiaje hapa? Au Ana maana ccm ni wahamiaji?
 
Last edited by a moderator:
Kwani kuna bango limewekwa kwenye nyuso za kila mtu anayetaka kujiunga CHADEMA kutokea CCM.

Kuna mechanism gani in place ndani ya CHADEMA kupima na kumfahamu kila anayependa kujiunga na kuwa mwanachama wa CHADEMA.

Kama chama mpaka sasa hakifahamu kina wanachama hai na wafu wangapi, wataweza vetting ya wanaotaka kujiunga na chama kuanzia vijijini mpaka mijini huku kila siku wanagawa kadi kama njugu kwenye mikutano ya hadhara.

Siasa za bongo bana. Why can't you stick to what you do best.

Ninawapongeza wanasiasa wa Tanzania katika uwezo wa political dotting and dabbing around ili kesho ukiwauliza wanakwambia "Nilisha tamka mapema. Nilifahamu hili jambo litatokea" wakati action ni zero.

and what could that be? that 'they' do best? setting the national agenda? or getting beat on demonstrations!
 
Ukishakuwa na mawazo haya tu basi wewe huwezi kuwa mwanasiasa tena kwa nchi hizi za kimasikini.

Siasa ni aghalabu kuleta sustainable solutions kwa wananch!!!
Shida zikiisha mtaji wao utakuwa nini?????!!!!

Hiki cha kuleta maendeleo endelevu hawafanyi hata tuimbe mpaka jua lisichomoke!!!!!

umeshindwa kudai maendeleo kwa anayekusanya kodi yako leo unawaza kudai kwa chadema? wafungue miradi kwa pesa kutoka wapi? hizo mil 200 za ruzuku zinatosha kulipa watendaji wa chama? walipe gharama za mikesi kibao ya kubambikiwa na maccm na walipe gharama za ofisi then ibaki fedha kwa ajili ya ofis za kanda,mikoa na wilaya? unajua tz ina wilaya ngapi? nina wasi wasi na ufaulu wako ktk somo la mathematics! kama ni kuchangia chama,acha kuongelea michango ya wengine tuambie wewe binafsi umechangia m4c kias gani? Nawashauri wenye mawazo km yako wabuni miradi huko huko mawilayani kwa nguvu zao na si kusubiri pesa kutoka makao makuu.wanachadema wa ukweli nadhani watakuwa wamenipata!
 
Akili ya mbowe bana chama anatembea nacho kwenye mikoba yake mwenyewe popote alipo anatoa maamuzi hata bila ya vikao kufanyika haya ndiyo madhara ya chama kuwa cha ukoo.

Asiyejua kuwa mko mitandaoni hasa JF kusubiri kupinga, kupotosha na kuponda kila hoja ya Mbowe na Slaa ni nani! Mnajifanya wajinga sana lakini, bila kujua
 
umeshindwa kudai maendeleo kwa anayekusanya kodi yako leo unawaza kudai kwa chadema? wafungue miradi kwa pesa kutoka wapi? hizo mil 200 za ruzuku zinatosha kulipa watendaji wa chama? walipe gharama za mikesi kibao ya kubambikiwa na maccm na walipe gharama za ofisi then ibaki fedha kwa ajili ya ofis za kanda,mikoa na wilaya? unajua tz ina wilaya ngapi? nina wasi wasi na ufaulu wako ktk somo la mathematics! kama ni kuchangia chama,acha kuongelea michango ya wengine tuambie wewe binafsi umechangia m4c kias gani? Nawashauri wenye mawazo km yako wabuni miradi huko huko mawilayani kwa nguvu zao na si kusubiri pesa kutoka makao makuu.wanachadema wa ukweli nadhani watakuwa wamenipata!

Wazo katoa mwana CHADEMA mwenzako ambaye upeo wake unatoka nje ya wigo uliopo wewe!!!!!

Mathematics sio kigezo cha kuwa na mawazo mazuri na kama ni kigezo then niletee matokeo ya hesabu ya viongozi wakuu ndani ya chama chako,jenga hoja ukiwa na fall back position mkuu usikurupuke tuu!!!!

Mimi sio muumini wa vyama vyenu hivi vya siasa ndio maana nimesema kwa nchi za kimasikini haya hayawezekani iwe chama A wala B na nimesema mtaji wao ni shida za walio wengi na hawawezi kutatua sustainably!!!!!! Fungua kichwa hicho acha kuwa bi-polar!!!!

Fedha za miradi hamna ila za kutalii na kufungua matawi na kuzungumza na diaspora ulaya na marekani achilia mbali kukodi chopa zipo tena kwa vyama vyote vikubwa??!!!!!!! Halafu unasema nimechangia ngapi are you serious????!!!!

Maendeleo ya kweli ni fani ya kujitegemea inayohitaji a true and sustainable state cum political will ambayo haipo kwa vyama vingi sana!!!!! Hizi maneno za mkimchagua nani ataleta maendeleo acheni bana.,zipo approach za kuleta maendeleo ambazo zinaweza kuanzishwa wakati unasubiri kuanza kukusanya kodi..,nazo pia hazijulikani???!!!

Wapenda maendeleo ya ukweli na endelevu nadhani mmenipata!!!!
 
Are you sure this is not too accademic? and less practical?
 
Back
Top Bottom