CHADEMA: Msimtupe kamanda Ngowi

CHADEMA: Msimtupe kamanda Ngowi

SHURU

New Member
Joined
Feb 14, 2013
Posts
4
Reaction score
13
Wiki iliyopita niliweka hapa jamvini hali ya mpambanaji Nicholaus Ngowi maarufu kama mtoto wa seremala ambaye alipata ajali jijini mMwanza akiwa kwenye shughuli za ujenzi wa CHADEMA KWA KUJITOLEA.u

kamanda Ngowi anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa mguu kwani umeharibika sana. Naendelea kukikumbusha CHADEMA kumsaidiamtu huyu yawezekana yupo kimya ila hali yake ni mbaya.namba zake ni 0713014400 na 0765507166
 
Yap kama alipata ajali kwenye shughuli za chama ana haki ya kugharamikiwa na chama japo yawezekana ni gharama sana ila utu kwanza pesa baadae.....
 
Mkuu maadam umeamua kumsaidia kwa nini usipeleke taarifa kwa tawi la CDM karibu na huko,
maana si viongozi wote CDM wanaingia JF"chukua hatua"
 
tuwekee picha yake mkuu, na namba zake za simu tuongee naye, ili tujue jinsi ya kumchangia!
 
Kamanda wa anga yupo mwanza kwa siku 3, jaribu kumtafuta anaweza toa msaada.... nenda ofisi ya mbunge nyamagana/ chama pia.
 
Mpe pole sana Ngowi mwambie avumilie Chadema wanakaribia kuingia ikulu.Atatibiwa Kama Mnyika anavyosubiri ili aendelee na shule
 
Aisee weka number zake kama waweza nimtafute hata nikamwone kamanda huyu!
 
namba si hizo hapo chini kwenye uzi,sasa mnataka namba gani zaidi ya hizo hapo?
 
Wiki iliyopita niliweka hapa jamvini hali ya mpambanaji Nicholaus Ngowi maarufu kama mtoto wa seremala ambaye alipata ajali jijini mMwanza akiwa kwenye shughuli za ujenzi wa CHADEMA KWA KUJITOLEA.u

kamanda Ngowi anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa mguu kwani umeharibika sana. Naendelea kukikumbusha CHADEMA kumsaidiamtu huyu yawezekana yupo kimya ila hali yake ni mbaya.namba zake ni 0713014400 na 0765507166

ACHA MAJUNGU WEWE SOMA MAELEZO YA NGOWI

Ajali iliyonipata sio mwisho wa kuipigania CHADEMA na Taifa
Ni ukweli kwamba nilipata ajali jijini Mwanza tar 20january ikiwa ni siku moja baada ya kufanya mkutano mkubwa sana katika kata ya kitangiri ambayo ipo chini ya diwani wa mahakama bwana Matata.Mkutano tuliufanya pamoja na kamanda Alphonce Mawazo lengo likiwa ni kuendelea kukijenga chama.Kufanya mkutano huo ilikuwa ni sehemu tu kwani lengo langu kufanya safari toka Dodoma ilikuwa ni kuungana na kamanda pamoja na wapiganaji wengine kuelekea Muleba na baadae Magu kwa ajili ya kampeni kwani kulikuwa na uchaguzi mdogo wa vijiji,vitongoji na mitaa. Nikiwa bado Mwanza nilipata ajali ambapo niliumia mguu wa kushoto kwani ulichanika vibaya na kuvunjika baadhi ya maeneo ikiwemo sehemu ya kukanyagia na vidole.Nilitibiwa siku ile na kulazwa hospitali ya bugando kwani nilitapika damu sana na nilikuwa na maumivu makali sana.Kibaya zaidi nilifungwa vibaya kitu ambacho kilisababisha mzunguko wa damu kwenye mguu kukosekana hivyo kupelekea sehemu ya nyama ya mguu kuoza ambapo nilifanyiwa upasuaji ili kuiondoa jumamosi ya wiki iliyopita katika hospitali ya mwananchi ambapo nililazwa kwa siku 17 kwani huduma ilikuwa hairidhishi katika hospitali ya Bugando.Baada ya upasuaji nilihamishiwa hospitali ya KCMC ambapo ninaendelea kutibiwa mpaka hivi sasa.Ninafaham kuwa shughuli ya kujenga chama sio shughuli ya viongozi wa chama bali ni jukumu la kila mwanachama kuhakikisha itikadi na falsafa ya chama zinamfikia kila mtanzania. Upendo wangu kwa nchi yangu ndio msukumo unaonifanya nifanye harakati za ukombozi maeneo tofauti ya nchi yetu ili kuhakikisha watanzania wanaondokana na utawala dhalimu ambao unamnyonya mtanzania.Kiukweli Kamanda Alphonce Mawazo alitaka sana kuwa nami hospitalini lakini nikamwambia Aende kwani Muleba na Magu wanahitaji ukombozi.Sina uhakika kama chama kina taarifa juu ya kilichotokea lakini ninawashukuru wote ambao wanaendelea kunipa ushirikiano na faraja katika kipindii hiki kigumu kwangu.Ninafaham fika kuwa ukweli haujawahi kushindwa na uwongo, wala dhulma haikuwahi kushinda haki na Mungu hakuwahi kushindwa na shetani. huu ni ushahidi tosha kuwa katika vita tunayopigana dhidi ya dhulma tutashida siku si nyingi hivyo ni jukumu la kili mpenda haki kuendeleza mapambano bila kuchoka ushindi upo karibu.CHADEMA sio kituo cha kutoa misaada bali ni chama cha siasa hivyo wale wanaolibeba swala langu kisiasa nawaomba waache. Ninaomba tuendeleee kuombeana ili nipone mapema na kurudi kwenye mapambano.by Nicholaus Ngowi (mtoto wa seremala) 0713014400 na 0765507166 ​




 

Similar Discussions

Back
Top Bottom