CHADEMA tulipe uzito hili

CHADEMA tulipe uzito hili

NGOWILE

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
454
Reaction score
258
Ndugu zangu wanajamvi kwanza niwasalimu.

Ni siku nyingi cjajitokeza hapa jamvini katika kujadili maswala mbalimbali yanayolihusu Taifa letu.Hii ni kutokana na hali yangu ya kiafya kutokuwa nzuri kutokana na ajali niliyoipata mwezi january na kwa sasa ninamshukuru Mungu kwani ninaendelea vizuri.

Leo nitajaribu kukizungumzia chama changu cha democrasia na maendeleo CHADEMA.Kikubwa kilichononifanya nijitokeze ni kutaka kuwashauri viongozi waandamizi wa chama changu kuhusiana na namna ya kuendelea kukikuza chama chetu kutoka hapa tulipo na kuendelea mbele na kuweza kushika dola katika siku za usoni.

Ni ukweli usiopingika kuwa chadema ndicho chama kikuu cha upinzani hapa nchini mwetu kwa hivi sasa.Kwa maanahii ninapata ujasiri mkubwa wa kusema kuwa ndicho chama pekee mbadala wa chama tawala chama cha mapinduzi CCM.Kwa maana hiyo CHADEMA ndilo tumaini pekee kwa watanzania baada ya kukichoka chama cha mapinduzi.Kwa nafasi hii ambayo CHADEMA imefikia ni vyema viongozi wake kufahamu kuwa watanzania hasa wale waliokichoka chama cha mapinduzi na waumini wa mabadiliko wanakitazama chama hiki kwa jicho makini na kwa ukaribu sana ili kujihakikishia kuwa watafanya mabadiliko yatakayokuwa na tija kwa faida yao na watoto wao.Hivyo ni vyema viongozi na watendaji wa chama hichi kuikwepa mitego ambayo inaweza kuuharibu muonekano wa chama hichi mbele ya umma wa watanzani na hasa mitego ile inayoandaliwa na kuratibiwa na viongozi wa chama cha mapinduzi.

Ni wazi kuwa sehemu kubwa ya wanayokiunga mkono chama hiki ni vijana na hii ni kutokana na kukata tamaa ya kimaisha na kukosa matumaini ya maisha yao.Kwa kulifahamu hili ni lazima chama kiache kujiridhisha na idadi kubwa ya vijana wanaijitokeza katika mikutano ya hadhara ya chama hiki kuenda mbali zaidi kuhakikisha kuwa vijana hawa wanajiandikisha katika daftari la mpiga kura na vile vile wapewe elimu ili wafahamu umuhimu wa kupiga kupika na thamani ya kura zao.

Pamoja na hayo ni dhahiri kuwa taasisi inayokuwa haikosi migogoro na kupishana mawazo.Na hali hii ni vyema sasa viongozi waandamizi kukemea malumbano ya baadhi ya wanachama na viongozi katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii badala yake migogoro ijadiliwe na kutatuliwa ndani ya chama kwa vikao halali na kwa kufuata katiba ya chama pamoja na zile za mabaraza ya chama.

Ni lazima sasa chama kuanzisha timu ya vijana wanaoelewa na kuifahamu vyema falsafa ya chama,katiba ya chama pamoja na malengo ya chama na wawezeshwe kwenda kila kona ya nchi hii kuhubiri nia na madhumuni ya chama pamoja na kuwajengea uwezo viongozi wa ngazi za chini za chama.Sina maana kwamba sithamini jitihahada za viongozi waandamizi wa chama katika kukijenga chama,lengo ni kuongeza nguvu kazi yenye uelewa wa kutosha watakaoweza kufika maeneo mengi na kwa wakati mfupi.

Ni vyema sasa viongozi wa chama wakafahamu kuwa vyombo vya habari si rafiki tena kwa siasa za chadema kutokana na woga ama kumilikiwa na makada wa chama cha mapinduzi.Hivyo ni wakati muafaka wa chama kuanzisha vyombo vyake vya habari na hasahasa redio.Tupo tayari kuchangia uanzishaji wa redio hiyo.Ikiwezekana kila kanda iwe na redio yake ili kuwafikia watanzania wengi.

Kwa leo naomba niishie hapa.

By.Nicholaus Ngowi (mtoto wa seremala)
mobile.0713014400
 
Back
Top Bottom