CHADEMA msikiuze chama kwa Nyalandu, Lissu anatosha

monde arabe

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
8,487
13,018
Habari za muda huu ndugu wanabodi. Hii ni kwa Wanachadema wote, Watanzania wote,wapenda siasa na wasio wapenda siasa. Tundu Antipas Mughwai Lissu ndiye mtu sahihi kwa muda huu anayeweza kututoa Watanzania Misri na kutupeleka Kanaani.

Kama CHADEMA na Watanzania kwa ujumla tutampitisha mtu mwingine hasa Nyalandu tunaenda kukiua chama kwa sababu Watanzania wote tumewekeza matumaini yetu kwa Lissu kwa kuwa huyu ndiye mtu pekee aliyepitia au kuyaonja mateso na mahangaiko tuliyoyapitia kwa kipind cha miaka 5 ya Magufuli. Tusifanye makosa hata kidogo, Nyalandu ni pandikizi la CCM hatupaswi kumuamini hata kidogo.

2020, twende na Lissu tukikosea hapo tumekwisha (binafsi sitajihangaisha hata kupiga kura endapo Lissu hata gombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya CHADEMA)

Pia,tunapofikiria kuwatafuta Wagombea ndani ya CHADEMA tuwakumbuke watu kama Aquelina, Kamanda Mawazo, Azory Gwanda,Beni Saanane pamoja na watumishi wa umma waliopitia kivuli cha mauti na manyanyaso kwa muda wa miaka 5 bila kuwasahau wakulima wa korosho pamoja na wakulima wa mazao mengine ikiwa ni pamoja na pamba mpunga na mahindi

Lissu anatosha kwa nafasi ya Urais tusifanye makosa huyo ndyo atakuwa sauti yetu!
 
Narudia wakati huu Tz inahitaji mgombea kutoka upinzani mwenye roho ngumu, mwenye maslahi mapana ya Nchi!! TL TU ndiye anatosha, Huwezi muweka Nyalandu ukategemea mazuri.

TAL⏲️
 
Hahaha utasikia 'Tunahitaji mfumo siyo mtu' kisha utasikia 'Anayefaa ni Lisu tu ndiyo wa kutuvusha' au 'Anayefaa ni Mbowe tu'

Mnashindwa kutengeneza mfumo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom