Chadema mpo wapi?


M

Mkerio

Member
Joined
Mar 12, 2006
Messages
35
Likes
0
Points
0
M

Mkerio

Member
Joined Mar 12, 2006
35 0 0
Nadhani humu ndani JF kuna viongozi wa chadema. Kampeni zilizopita zimeleta hamasa sana kwa wa TZ. Mimi nakaa Kinyerezi watu wanauliza kadi wapate wapi, ofisi ya chama ipo wapi? Nadhani chama kingefanya recruitment drive kwa kufungua matawi nchi nzima na kuuza kadi kabla moto huu haujaisha nguvu. Ukiacha moto ukipoa itakuwa ngumu. na kwa vile chama kina ruzuku kubwa ni vizuri kuajiri graduates kama makatibu wa majimbo nchi nzima na pia kuweka wenyeviti makini. Mkazo uwekwe kwenye majimbo si mikoa. Naamini kila katibu wa jimbo anaweza kuwa na gari kwa kuchangiwa na wanachama na ruzuku pia. Vijana wakifanya kazi nzuri na kuachana na vitu vidogo vya akina Zitto na Shibuda tutashinda kwa kishindo mwaka 2015. Mimi nipo tayari kulipia ofisi na kumwajiri katibu kata ya Kinyerezi. Chadema Hoyeeeeeeeeeeee! Tukiimarisha matawi tutafanya vizuri uchaguzi wa serikali za mitaa. Hawa watu wa mitaa ni muhimu kwa ajili ya kulinda kura 2015. Inapaswa huku chini tuwe na watu wenye uchungu ili walinde maslahi ya chama. Nilienda Mwanza niliona jinsi vijana walivyoimarisha chama katika matawi. Ukiwaona wanavyokitetea chama unafurahi. Tufanye hivi nchi nzima.
 

Forum statistics

Threads 1,235,767
Members 474,742
Posts 29,234,625