Nape Nnauye
MP Mtama
- Dec 26, 2012
- 99
- 408
Mhe. Mbowe akiwa Mbeya alikiri wazi kuwa CHADEMA kwa miaka yote tangu kuanzishwa kwake kimekuwa ni chama cha HARAKATI... Lakini nilifurahi kusikia akiwaomba wenzake kuwa sasa ni wakati wa kukibadili Chama chao kutoka chama cha harakati na kuwa sasa chama cha SIASA.
Sasa ni karibu miezi mitano tangu atangaze na kuwasilisha ombi hili kwa wenzake lakini kwa masikitiko makubwa wenzake mmempuuza mwenyekiti wenu, badala ya kukibadilisha chama sasa mnakifanya cha harakati zaidi mpaka sasa mnapanga na kutekeleza kudhuru watu hasa wasiowaunga mkono.
Kumpuuza Mbowe kwenye wito wake huo ni kifo chenu na hivyo kuathirika kwa demokrasia nchini. Uwepo wenu umeleta joto zuri kwenye siasa na demokrasia nchini ukiachilia mbali vibweka vya baadhi ya viongozi wenu. Lakini nadhani sio tatizo la chama bali la viongozi wachache waliofanya CHADEMA kichaka cha kufichia rangi zao halisi.
MTAKAO CHANGIA PUNGUZENI MAPOVU NA MATUSI MJENGE HOJA.