CHADEMA mnakosea wapi, mbona mnayumba kimsimamo?

Mbona ccm wanaumia Chadema kwenda kwenye sherehe Mwanza? Tena Chadema na nyie vaeni sare zenu kama wao wanavyovaa mi sare yao ya kijani! Uhuru ni wetu sote!
 
Hii kichwa ni cccm pure hao jamaa wa Chadema hutawaweza wao wanawaza ya kesho wewe uwezo wako wakufikiri unaishia kuwaza ya Jana tu pole sana! ndio mnavyojidanganya kuwa sikukuu ya Uhuru ni ya cccm
Kaka vyama vya siasa ni vya wananchi, lazima tuzungumze kuulegeza upinzani ni rahisi kuliko kuutengeneza ,si kazi ya mchezo
 
Wewe mleta mada unasaidia vipi chama, au upo upande gani??
Ukiwa field utaelewa kinachoendelea.
Wananchi ni wale wale kwa hiyo kuwepo kwenye events za Uhuru ni fursa kisiasa sio disadvantage!!
Uhuru ni wa Watanzania wote bila kujali chama!!
Kuwepo kuna impact kubwa ikiwa fursa ya kuwasilisha uliyokusidia utapewa, hilo ni suala la hisani, nilitegemea kwa kupitia jukwaa hili la uhuru wapinzani wakiitisha press conference kubwa ikiwashirikisha vyombo vikubwa vya kimataifa kuweka wazi adhima ya uhuru wetu lakini mateso ya watanzania ndani ya mkono wa chuma na hali ya kisiasa kwa kipindi hiki
 
Nyie tulieni hivyo hivyo wanasiasa waendelee kuwapelekesha maana nyie si washabiki tu kazi yenu kushabikia hivyo hawana ulazima wa o kujielezea kwenu nyie kazi yenu kushabikia tu.

Watanzania wajinga sana wao wenyewe hawana msimamo wowote zaidi ya kukaa migongoni mwa wanasiasa na kuwategemea.
 
Narudia tena si CCM wala CHADEMA Hakuna chama chenye nia ya kumkomboa mtanzania
Kwa sababu watanzania wenyewe huenda hawajui wanataka nini. Tumelelewa katika mazingira ya kuwa recipients na siyo kuwa active participants in making changes (hatu-set agenda)
 
Siasa za africa mazingaombw mengi
 
Refu limejaa upumbavu tu
 
NI UTOTO KUTOKUSHIRIKI MASUALA MUHIMU YA KITAIFA.

Sherehe za Uhuru ni jambo muhimu la kitaifa. Siyo suala la kichama. Vivyo hivyo shughuli za maendeleo ya Nchi. Unapogomea shughuli muhimu za kitaifa kama hizo unamkomoa nani kama sio utoto?

Hata uchaguzi wa serikali za mitaa ni jambo la Kitaifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…