CHADEMA: Mnajimaliza kutokea ndani

CHADEMA: Mnajimaliza kutokea ndani

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,512
Reaction score
40,197
Huko nyuma niliweka ushauri wangu hapa jukwaani kuhusu huu ulafi wa CHADEMA kupokea wananchama kutoka CCM na vyama vingine na kuwapa madaraka. Wengi walioingia kwa mbwembwe chamani siyo waumini wa kweli wa demokrasia. Tatizo linaloikabili CHADEMA leo ni USALITI kwa rangi zake zote.

Imesalitiwa kutoka ndani na inashambuliwa kutoka nje. Wenye macho tuliyaona haya na kuwashauri kwamba kabla ya kuwapa watu uongozi ni vyema ikawachuja kwanza kufahamu uadilifu na uwezo wao. Kuna kundi kubwa ndani ya viongozi wa CHADEMA ambao wanasubiri kipenga kilie waoneshe rangi zao kamili. Msidhani hao wenyeviti wa mikoa na makatibu wanaorudisha kadi ni jambo la ajali tu. Kila kitu kimepangwa na kitatekelezeka kwa wakati uliotarajiwa. Hawa wasaliti wamejibidiisha kusaka na kupata details zote muhimu za chama na kikosi kazi kimeshajipanga pa kuanzia na kumalizia.

Kufikia mwaka 2015 CHADEMA itakuwa na majeraha makubwa mengi na inawezekana (endapo hawatajipanga sasa) wakasambaratishwa kabisa na kuwa kama vyama vingine viliyopita. Yote haya yanafanywa na CCM kwa usaidizi wa 100% kutoka vyombo vya serikali.

Pigo la awali la CHADEMA ni kuongezeka kwa wanaojiita wapenzi wa chama hiki mitandaoni ambao kazi yao kubwa ni kutukana hoja zozote zinazokwenda kinyume na chama. Ninamaanisha kuwa wakosoaji wamewekewa mkakati wa kunyimwa haki ya kukikosoa CHADEMA kwa lolote lile. na hilo linaratibiwa kwa umakini na ufanisi mkubwa.

#JustSaying
 
Sawa tumekuelewa kama kawaida!lingine tafadhali....
 
chama cha dini na magumashi. CHADEMA waache wavune walichopanda
 
Sawa tumekuelewa kama kawaida!lingine tafadhali....
Asilimia kubwa ya mitihani mnayopitia mmeonesha kutofanya vizuri.

CCM inakufa pia CHADEMA inakwenda nayo bila shaka
 
Msiwasingizie CCM, matatizo yenu yanatokana na ninyi wenyewe, madudu mliyokuwa mnayafunika kwakudhan hayatatoka yamefumuliwa ndo mnahaha kumtafuta mchawi,mwaka wenu huu!
 
mkuu Msanii CHADEMA ndo inazidi kupasua anga, ni kama mfalme daudi alivyopaishwa na Mungu mwenyewe dhidi ya mfalme Sauli...
shaka ondoa..........lazima kutenganisha ngano na makapi. #JustSaying
 
Nimeona asilimia 30 kuwa kweli katika hayo uliyoyaandika
 
Sehemu kubwa ya viongozi wa CHADEMA ndiyo wanaotekeleza jukumu la kuua hiki chama.

Wakati kinaendelea kusifiwa na kushabikiwa na wananchi wengi inawezekana shamrashamra hizo ndo zikawa zinakisindikiza kuelekea shimoni. Narejea kauli yangu kwamba CCM inakufa na inahakikisha inaharibu vyama vyote vyenye uelekeo wa kuwakwamua wananchi kutoka ktk lindi la hali ngumu ya maisha.

Ikumbukwe tokea awali kwamba washabiki wengi siyo wapiga kura
 
Back
Top Bottom