CHADEMA mna mpango gani na majimbo haya ya Kigoma?

CHADEMA mna mpango gani na majimbo haya ya Kigoma?

Kwa asilimia kubwa naweza kukuamini mleta 'uzi' jinsi ulinyoweza kwa umakini kuileta na kuitetea hoja ya yako. Nadha HQ wakisikivu watalifanyia kazi hili

mkuu Makete mbali na kwamba me ni mzaliwa huko,pia nimebahatika kuzunguka miji na vijiji vingi mno wakati tulipokuwa tumeenda mkoani humo kufanya tathimini ya hali ya umaskini na ukimwi kwa kuzingatia uwepo wa wakimbizi,tumeifanya kazi kwa zaidi ya miezi 6,na mbali ya kuwa nafanya kazi hyo ya NGO'S iliyoniajili damu ya ukamanda ilikuwa inanisukuma kufanya research kuhusiana na vyama vya siasa na karibia vijiji vyote CCM ilikuwa inasubiri namba kutoka kwa CDM,Tatzo wananchi wamewachoka viongozi wao wa wilaya na mkoa,wanawataka viongozi kutoka makao makuu na wabunge,tena nisaidieni kunipatia namba ya profesa Safari,Baregu,Mabele malando na Mnyika tafazali.,
 
naomba kiongozi wa Chama wanye sifa za kutokea kwa majina halisi hapa kama dk Slaa,Zitto,Mnyika,Makene na dk Kitila wajitokeze kutoa majibu nami nitawaPM niwape namba zangu kwani tupo zaidi ya vijana 60 tuliomaliza vyuo vikuu tunahtaji tuwapatie mpango kazi wetu plz.
 
Tusimung'unye maneno. NCCR ilishinda huko kwa ushirikiano wa Zitto na Zoka wa TISS. Na tuzo kwa kazi nzuri ni ubunge wa Mbatia. Mwangalieni Zitto kwa macho sita. He is a snake.
 
Kwa sasa mkoa wa kigoma ndiyo kisima cha mageuzi hapa nchini maana magamba hapa ndio chama cha upinzani maana kati ya majimbo nane yalipo hapa mkoani magamba walisinda majimbo matatu tu na yenyewe baada ya nguvu kubwa vinginevyo ccm ilikuwa imeshatupiliwa mbali na wanakigoma. CHADEMA wakezeni vya kutosha katika mkoa huu maana kwa mujibu wa katibu mkuu wa CDM Dr. Slaa mkoa wa Kigoma ndio unaongoza kwa kuwa na madiwani wengi wa CHADEMA nchini,hivyo huu mkoa ndiyo hazina kuu ya chama. Ongezeni nguvu haswa hapa.
 
viongozi wa chadema msikilizeni mwanachadema mwenzenu nendeni mkoa wa kigoma mkoa ulioonyesha mfano wa kupenda mageuzi munataka wananchi watoe machozi ya damu ndio muende nilienda kasulu mjini kikazi,hata mimi nilisikia vijana wananiambia wanapenda sana kumuona mnyika kwenye kihoteli nilichofikia nadhani wakati umefika sasa viongozi kuzungukia maeneo ambayo wananchi wanawahitaji

pamoja na kwamba viongozi watakuja huko kwenye harakati zao za kukijenga chama lakini nikujuze tu kwamba wanakigoma mnatakiwa kubadilika.hamweleweki!!!!tuanze na kaburu.alifanya kazi kubwa sana ya kuijenga cdm.lakini baadae akaonekana anawasiliana na tiss.na baadaye akatimkia umagambani,akaiacha cdm solemba alikuwapo mtu anaitwa nsazugwanko,huyu alitimkia umagambani.akaja kafulila.akaingia kwenye siasa za makundi nae akatimkia nccr.huko nako kukatokea ugomvi mkubwa na viongozi wenzake akatimuliwa uanachama.wabunge wengi wa kigoma walitokea cdm.zitto nae ameripotiwa na gazeti moja kuwasiliana na tiss na ra!!wanacdm hawajaamini mpaka leo.haeleweki kama yuko umagambani au cdm.huu ni mtihani mkubwa sana kwa wanacdm wote na sio kwa viongozi tu.nawaombeni wanakigoma muwaweke kiti moto wabunge wenu.wanaharibu sifa ya mkoa wa kigoma.
 
pamoja na kwamba viongozi watakuja huko kwenye harakati zao za kukijenga chama lakini nikujuze tu kwamba wanakigoma mnatakiwa kubadilika.hamweleweki!!!!tuanze na kaburu.alifanya kazi kubwa sana ya kuijenga cdm.lakini baadae akaonekana anawasiliana na tiss.na baadaye akatimkia umagambani,akaiacha cdm solemba alikuwapo mtu anaitwa nsazugwanko,huyu alitimkia umagambani.akaja kafulila.akaingia kwenye siasa za makundi nae akatimkia nccr.huko nako kukatokea ugomvi mkubwa na viongozi wenzake akatimuliwa uanachama.wabunge wengi wa kigoma walitokea cdm.zitto nae ameripotiwa na gazeti moja kuwasiliana na tiss na ra!!wanacdm hawajaamini mpaka leo.haeleweki kama yuko umagambani au cdm.huu ni mtihani mkubwa sana kwa wanacdm wote na sio kwa viongozi tu.nawaombeni wanakigoma muwaweke kiti moto wabunge wenu.wanaharibu sifa ya mkoa wa kigoma.


Wakuu ifike mahala tukubaliane kwa kauli moja na tuache kulaumiana na kuhukumu mkoa mzma kwa makosa ya watu wachache,hiyo ni stereo type mbaya,kimsingi watu wa kigoma huwa hatunuliki kwa madaraka wala talanta,wanaonunulika kwa bei yoyote ujue huyo hakuwa mmoja wetu,natambua,nanyi mjue watu wa Kigoma tunamisimamo isiyoyumba na ni wabishi sana,nafikiri hayo waliyoyapata uliowataja toka kigoma ni matokeo ya ubishi ambao ni asili yetu na misimamo isiyoyumba.
 
Mkuu Mpau kama ulikuwa hujui,chukua hii ,dogo Mkosamali alisafirisha hadi daresalama kwa gari ya Kafulila na kulipiwa kila kitu ili aende makao makuu kumwona mwenyekiti mbowe na amwulize jimbo la muhambwe limetengewa shilingi ngapi?hii inafuatia na ushawishi wa Zitto,Mma Buyogela a.k.a mama Balu na kafulila walikaa nae kwa zaidi ya masaa 3 katika Upendo Guest house kumshawishi huku Kafulila akimsisitizia Mkosamali kwamba makao makuu hawajalipa kupaumbele jimbo la Muhambwe na majimbo mengine mkoani humo iktajwa kuwa mwaka wa 2000 na 2005 CDM makao makuu walitoa fedha za kutosha bt zikaliwa na wajanja wachache na CDM ikapoteza jimbo,na kuonana na mwenyekiti Mbowe ilishindikana ndipo bwana Kafulila akamkutanisha na Johni Mnyika wakati huo akiwa ofisa habari wa chama makao mkuu na Mnyika akamwakikishia kwamba ni kweli kwa Jimbo la muhambwe chama hakijalipa kipaumbele jimbo hilo bt hawezi kukosa milioni 1 na nusu,huyohuyo Kafulila akampeleka dogo kwa mwenyekiti wa NCCR Mageuzi bwana Mbatia na mbatia akamwakikishia kumpatia milioni 5 kwa ajili ya kampeni kama atahamia NCCR ,na dogo Mkosamali akasaini deal na kuhamia huko yeye na mshauri wake mkuu ambaye kwa wakati huo alikuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CDM kutokea mkoa wa Kigoma ndugu Balela na wakaenda redio Kwizela kutangaza kujitoa CDM na kuhamia NCCR,kumbukumbu zangu zinaniambia dogo alishiliki kwenye kampeni za marudio ya ubunge Busanda akitokea chuo cha SAUT,Tatzo kubwa la dogo Mkosamali ni njaa ya pesa na madarka bt bora alivyohama mapema coz alikuwa anatumiwa na Zitto na kwa sasa ni janga jimboni mwake hakubaliki tena na amebakia kugombana na mkuu wa wilaya hiyo na mwenyekiti aliefukuzwa huku akishinda kwa waganga Burundi,data ninazo

:angry:
ya kweli hayo mkuu......
 
ya kweli hayo mkuu......


very true my friend anadai kwa sasa yupo kwenye mapambano na kwa sasa pia kila mtu anamwona adui,bifu lake lilianza na mwenyekiti wa halmashauri aliyeng'olewa
 
Kweli kamanda umenena, CDM ni chama changu lakini naungana na wewe kwamba makao makuu wanaelekeza nguvu sana sehemu sehemu zilizokwisha kombolewa nakusahau kuwa kaskazini haiwezi kuifanya DCM ichukue dola 2015. Mfano mdogo ni mkoa wa kagera. Kuna wilaya ya BKB vijijini ambayo haina mtu yeyote wa kuisemea tangu uchaguzi mkuu umalizike hakuna mkutano hata mmoja ulishawahi kupigwa kule. lakini tunasikia mara mbowe atikisa arusha, Dr. slaa kunguruma kaskazini na maeneo mengine lkn si mikoa mingine. wananchi wanalalamika sana. Muleba inaelekea kikombolewa kwa juhudi za watu wachache si kwa mkono wa uongozi wa CDM taifa. Nadhani ni wakati muafaka wa wahaharakati na wapenda maendeleo ya nchi yetu kuwalazimisha viongozi wa kitaifa kututendea haki kwa kugawa rasilimali za chama kwa usawa. Kamanda nakukubali
 
Nyie waha fanyeni kazi mtatoka huyo slaa na wenzie hawaji na fuko la hela... Mnawalilia makao makuu kwan wamekuwa mingu wenu?
 
Waungwana..tunaowahitaji viongozi wa kitaifa ni wengi,kanda ya kusini Mtwara ,Lindi na Ruvuma ni moja ya maeneo ambayo hayajafikiwa,tukumbuke pia viongozi wa kitaifa wanamajukumu mengi sana,mkakati unaokubalika ni waibuke wanaharakati kutoka maeneo husika tukiwasubiri viongozi wa kitaifa tutachelewa....sisi ndo tunaoyajua matatizo yetu tujitoe kuyasemea...
 
Back
Top Bottom