CHADEMA mmevuna mlichopanda

CHADEMA mmevuna mlichopanda

wewe 2015 lowassa angegombea urais ndani ya CCM kwa sifa mbaya alizokuwa nazo CCM ingepata tabu sana pengine vurugu zingezuka inakuaje mtu mchafu namna ile anashinda urais wakati watanzania wanajua ni mchafu,kilichofanyika pale ni kuokoa CCM na maslahi yao kwani urais upo tu,kama hivi sio miaka mingi lowassa na kundi lake wanaweza ongoza nchi....

Huu ndio upambavu wangu,weka hekima yako wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaah upumbavu wako naona Kama wangu vile,mi nahisi Kama Ni mpango hivi ahamie upinzani maana 2015 Hali haikuwa POA CCM,hivyo akiwa upinzani akigombea kura wagawane na CCM ishinde,japo nafikir CCM Wala lowasa mwenyewe hakutegemea kura zile milioni sita upinzani wangepata!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wewe 2015 lowassa angegombea urais ndani ya CCM kwa sifa mbaya alizokuwa nazo CCM ingepata tabu sana pengine vurugu zingezuka inakuaje mtu mchafu namna ile anashinda urais wakati watanzania wanajua ni mchafu,kilichofanyika pale ni kuokoa CCM na maslahi yao kwani urais upo tu,kama hivi sio miaka mingi lowassa na kundi lake wanaweza ongoza nchi....

Huu ndio upambavu wangu,weka hekima yako wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama nimekuelewa vile.
 
Katika watu wajinga duniani na ulimwenguni Tanzania ipo top 10. Lowassa aliondoka ccm kwenda cdm baadae dr. Slaa akaondoka cdm kwenda ccm indirectly kwa kile alichokiita kutokubaliana na ujio wa lowassa ndani ya cdm na baadae akapewa ubalozi ila hatukuona mapokezi ya huyo dr slaa yalikuaje, leo hii lowassa anarudi ccm kwa mapokezi ya viongozi wakubwa ndani ya serikali huku mkuu wa inchi akiwepo na akifurahia sana. Kuna ya kujiuliza kwa kina sana kwenye hili
 
Katika watu wajinga duniani na ulimwenguni Tanzania ipo top 10. Lowassa aliondoka ccm kwenda cdm baadae dr. Slaa akaondoka cdm kwenda ccm indirectly kwa kile alichokiita kutokubaliana na ujio wa lowassa ndani ya cdm na baadae akapewa ubalozi ila hatukuona mapokezi ya huyo dr slaa yalikuaje, leo hii lowassa anarudi ccm kwa mapokezi ya viongozi wakubwa ndani ya serikali huku mkuu wa inchi akiwepo na akifurahia sana. Kuna ya kujiuliza kwa kina sana kwenye hili
Mkuu,
Naona umeandikwa kwa utulivu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya Julai 2015, nilikuwa miongoni mwa Watanzania waliokuwa wakiiunga mkono Chadema. Sio kama mwanachama bali nilikuwa naafikiana nao katika harakati zao za kisiasa hususan vita dhidi ya ufisadi.

Lakini ghafla wakampokea Lowassa, mwanasiasa ambaye Chadema hao hao walimwandama kwa takriban miaka tisa mfululizo (tangu mwaka 2006 hadi 2015) wakimuita fisadi.

Na wala sikutafakari mara mbili, nikaamua kuacha kuiunga mkono Chadema. Bahati nzuri Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Slaa ambaye pia alikuwa mgombea urais mwaka 2010, nae aliamua kuachana na chama hicho. Niliandika haya kumpongeza

Dear Dkt Slaa,asante kwa kufanya maamuzi magumu kwa kujiuzulu. Tutakuenzi milele ~ Kulikoni Ughaibuni

Na niliwananga Chadema na makala hii

Siasa mchezo mchafu au baadhi ya wanasiasa ndo wachafu? USALITI: Chadema/Ukawa na Lowassa ~ Kulikoni Ughaibuni

Na baada ya Chadema kulamba matapishi yao na kumkumbatia Lowassa, chama hicho kiligeuka kuwa "chama cha mtu mmoja" kama nilivyotanabaisha katika makala hii

Makala yangu RAIA MWEMA la 05/08/15: "Chama kimoja Vyama Vingi Chama cha Mtu Mmoja" ~ Kulikoni Ughaibuni

Na the latest ni tahadhari niliyotoa baada ya Lowassa kukutana na Magufuli Ikulu mwaka jana

Uchambuzi Wa Kina Lowassa Kukutana Na JPM Na Kumpongeza: Mkakati Au Anarudi CCM?: ~ Kulikoni Ughaibuni

Sidhani kama Chadema wanahitaji kupewa pole kwa sababu kila aliyejaribu kuwatahadharisha kuhusu Lowassa aliishia kutukanwa.

Uamuzi wa Lowassa kurejea CCM si jambo la kushangaza kwa sababu (a) alihama CCM kwa ajili tu ya kusaka urais huko Chadema (b) kwa kugombea urais kupitia Chadema, Lowassa aliweza kukihenyesha chama hicho kilichomuita fisadi huko nyuma, lakini kikalazimika kuzunguka nchi nzima kumsafisha Waziri Mkuu huyo wa zamani.

Kwa kifupi, Chadema mmevuna mlichopanda. Hatma ya chama hiki sasa itategemea sana jinsi kitakavyoweza kuhimili kipigo hiki kikubwa kabisa kwao. As it stands, kuna uwezekano mkubwa kabisa kwa chama hicho kutoambulia japo jimbo moja katika uchaguzi mkuu ujao, sio kwa kushindwa bali sio siri kuwa kuna wabunge kadhaa wa chama hicho wapo njiani kwenda CCM.

Na liwalo na liwe, wabunge wawili wasiotarajiwa kabisa kuwa ipo siku wataikimbia Chadema ni Kubenea na Bulaya wapo njiani kwenda CCM.

Tujikumbushe #FutureTweet hii ya Januari 9 mwaka jana




Sent using Jamii Forums mobile app

Siasa Ni kama Kamari.CDM walikua sahihi 99% kumchukua Lowasa akagombea Uraisi.
Tusidanganyane., Hakuna Uwezekano wa Upinzani kumchukua dola kwa Karatasi.
Lowasa is the best Gambler.

Udhaifu waCDm wa Sasa hautokani na cDM Wala vyama vya Upinzani wala wenyeviti wao. Bali unatokana na Nguvu ya Mwenyekiti wa CCM na Serikali yake.

Mnaangalia cDM. Haujajiuliza Taasisi gani nchini iliyobaki salama na Imara?
Ni Bunge, Ni Mahakama, Ni TLS, Ni Media, ni wasanii, Ni Viongozi wa dini, Ni CCM, ni Vyuo vikuu?

Mkubali Mkatae Lowasa hapaswi kulaumiwa kwa maamuzi yake. Umri wake sio wa kuishi kiuanaharakati Tena.

.
 
Bwana Chahali pamoja na mengi unayoyasema na uliyoyasema, uhakika ni kuwa wewe na genge lenu mmejipa jukumu la kutuamlia hatina ya nchi yetu. Akina Lowassa na wewe lenu moja tofauti na hilo mngetumia nafasi mlizo nazo kuzieleleza siasa za nchi kuikomaza nchi na kusisimua maendeleo.

Mimi ni mwanzilishi wa CCM 1977 kinachoendelea kwenye siasa za CCM ni uozo mtupu. Matokeo yake nchi inaoza wakati mkijifurahisha na siasa za watu ambazo ni unproductive.

Nawaunga mkono CHADEMA kwa maono, mikakati, hoja sahihi na kuvumilia mateso ya CCM na vyombo vya dola. Ya Lowasa ni dalili ya nje tu ya uozo wa nchi. Ila naamini CHADEMA watatoboa wakiwa wameiva kwenye tanuru mnalolichochea.

Mwenyezi Mungu awaangaze.
 
Back
Top Bottom