CHADEMA mmetumika vya kutosha!

Umejaribu kutafiti CHADEMA kilikuwa na hali gani alipokichukua hadi leo na kuwa adui namba moja wa CCM? Na je unajua ni nguvu ya kiasi gani CCM inatumia kujaribu kukidhoofisha?
Utafiti hauwezi kumpa mbowe credibility yeyote, ukumbuke dunia iko safari (inabadirika) hivyo wananchi wenyewe wanaelewa kwa kiasi dhana ya upinzani hasa ikichangiwa na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano hivyo taarifa zinasambaa sana.

Mabadiriko huwa yanakuja yenyewe bila ata kuchagizwa na mtu, uwepo fursa kama tehama ni chachu kwa wapinzani kuitumia na kuongeza nguvu kwao ila kimkakati wameshindwa tena sana.

Pia uhitaji wa madiriko hasa kwa miaka kama 10 hivi nyuma ukichunguza vyema utaona na kugundua kuwa siyo kwamba upinzani uliimarika ila ilikuwa kwamba CCM iliyumba sasa imesimama na kutengemaa ndiyo maana upinzani unadhoofu na kufa. Hatujawahi kuwa na upinzani imara ila ilitokea tukawa na CCM dhaifu sasa imerudisha imara wake wapinzani chali.

Nakwambia si kwa chuki Mh. Mbowe hawezi kuivusha CHADEMA alipofikia ni kuporomoka tuu. Haoni ata fursa ya kutumia vijana wazuri waliopo nchini ukabila na uroho wa madaraka unaiua chadema na upinzani nchini.
 


Huu upuuzi ulioongea hapa ningeuona wa maana kama mngekuwa mnashinda box la kura kuhalali. Ccm haiko madarakani kama chama chenye afadhali kuliko vilivyopo, bali ni matumizi yake ya nguvu ya dola. Huo ubora wa ccm hauonekani wala haupo zaidi ya mabavu ya vyombo vya dola.
 


Labda utueleze ukabila na uroho wa madaraka wa Mbowe umeanza lini. January 2016 alipoambiwa yeye na wenzie marufuku lufanya shughuli za siasa? Au pale jiwe lenu liliposema wa kaskazini watasubiri sana?
CCM kwa sasa duwa yenu kubwa ni kuona Mbowe anatoka kwenye uongozi mkiamini kabisa mkiweza hilo mtapandikiza watu wenu halafu iwe de ja vu kama mlivyofanya kwa NCCR, TLP na CUF.
 
Rafiki yangu usije ukadhani yote yanayosemwa na wapinzani wanao hamia CCM ni uongo Mbowe kamsaliti Chacha Wange/marehemu leo, Dr. Slaa kwa tamaa zake, kitila, zitto, Kafurila, Mwita, na wengine wengi kisa tuu kuhoji uhalali wake.

Siasa siyo vijembe na kebhehi majukwaani rafiki yangu, zipo njia kibao za kufanya siasa tangu 2015 chadema kama chama kikuu cha upinzani kimefanya mariadhiano gani na chama chochote cha upinzani??

Subiri mwaka 2020 wanavyokanyagana kudanganya wananchi eti wanataka kuungana stupidities..! Hivi unaweza kuniambia chadema wanamradi gani mkubwa wa chama kutumia ruzuku na pesa michango ya wanachama na wafadhili mpk washindwe kujenga ofisi ya maana poor Mbowe poor chadema.
 
Kwahiyo nanyinyi mmemchoka mbowe ila shida ni CCM tu. Sawa tumekuelewa ingawa umetumia nguvu nyingi sana kujieleza.
 
Mkuu chunga matumizi ya sarufi R na L nitarudi kujadili maudhui ya bandiko lako
 
Kwa kupora ushindi, kweli it deserve.
 
Wewe big mind kwanza nikuombe usitumie kimombo hata siku moja kwani hukijui!
Pili pamoja na hama hama hii, chadema bado ni wengi sana. Wanachama million 6 na chadema wa mioyo na ambao ndio wa kweli kabisa ambao hata sio wanachama wako zaidi ya millioni sita tena.
Hasa wakati huu wa JPM watu wengi wana hasira naye kwa maovu na uonevu anaowafanyia vyama vingine hasa chadema na CUF.
Poleni sana ndugu Chadema na CUF. Jiwe hata kusikia sauti ya viongizi wa dini hakusikia. Na Polepole ajue ataitwa the Hague mwache ajitoe ufahamu akihangaika utoa hongo za ccm kwa kutumia trillion za wananchi. Where is 1.5tr???
 
Ccm imewafunga vyama mbadala mikono na miguu, bado wanaiba kura, na wanawahonga wanachama, wanawafungulia kesi nyingi za uwongo na kuwanawafunga!!
Halafu eti wanamwaga uvccm hapa kuimba wimbo wa Mbowe hafai! Mbowe hafai!
Kama vile yote yanayofanywa na Polepole na wenzake wote pamoja na policcm, ccmtra na ccmNEC hazitoshi!

,shame on you! Mungu yuko anawaona! Ni aibu kubwa kwa polepole ambaye alikuwa mwenye kutetea haki sasa hivi amekuwa bwana wainda maslahi yake ya tumbo siyo nchi yake.

Live Mbowe alone!
 
Magamba wanataka Mh. Mbowe asepe ili iwe rahisi kupitisha yao. Maana miaka nenda rudi wameshindwa kupandikiza mgogoro wa kuimaliza CDM kwa gia yeyote; ikiyobakia ni haya manunuzi yanayoendelea.
 
Wengi wenu mnadhani kuwa upinzani, ni kuwa vibaraka wa serikali na kuwania ruzuku tu pamoja na marupurupu ya udiwani ama bunge. Hayo ndiyo yamejaa kwenye akili zenu. Not a very good mindset.
 
Magamba wanataka Mh. Mbowe asepe ili iwe rahisi kupitisha yao. Maana miaka nenda rudi wameshindwa kupandikiza mgogoro wa kuimaliza CDM kwa gia yeyote; ikiyobakia ni haya manunuzi yanayoendelea.
Afadhali basi wangesubiri hayo manunuzi yao yavunje chama ndipo waje na hiyo hoja yao. Lakini wanaonyesha kukurupuka, jazba na muku.🙂
 
Duniani kote siasa ni mchezo wa kimaslahi zaidi. Nikune mgongo wanguna mimi nitakukuna mgongo wako.

Ni lazima wakati mzee Mamvi anaingia CDM kuna ambao walifaidika kipesa. Unaweza ukafaidika mfukoni lakini kimaadili unakuwa umeshaonyesha udhaifu mkubwa sana. Yuda alipewa fedha na waliomuua Yesu lakini dhambi ya usaliti ilimfanya akajinyonga.
 
Unajua Chiriku ni aina ya ndege ambaye hutumia maneno yale yale aliyokaririshwa na Bwana wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…