Shinto
JF-Expert Member
- Dec 6, 2010
- 1,781
- 98
Mikoa ya kusini sasa ipo kwenye vita kali kupigania rasilimali yao ya gas isihamishwe kuja Dar es salaam kama raw material badala yake all processing na viwanda vinavyotumia gas kwa kiwango kikubwa viende vikajengwe huko.Nadhani hii ni karata nzuri kwa wananchi wa mikoa ya kusini, kwani kuwepo kwa viwanda kutachochea ajira na miundo mbinu kuimarika.Ni wazi CCM wameanzisha mgogoro na hii voting bloc, kwa nini CDM haitaki ku-step in?Je ile sera maarufu ya majimbo ilikoma?Nina uhakika CDM ikishikia bango juu ya swala hili kama ilivyofanya kwa sakata la Mwangosi na Ulimboka, itanufaika vya kutosha kisiasa, pia itaondoa dhana iliyojengeka kusini kuwa CDM ni chama cha watu wa kaskazini!.