Chadema mlitaka nchi isitawalike, leo mnaomba maridhiano

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
Chadema mlitaka nchi isitawalike leo hii mnaomba maridhiano!? Mmekuwa Malaika au Shetani yule yule kabadili staili!?,miaka minne mmetumia nguvu zenu zote kupinga maendeleo ya Tanzania,leo mnaomba maridhiano,mnapaswa kujitafakari sana kabla ya kufanya maridhiano hayo.

Chadema mnaoshiriki ndani na nje ya nchi kulihujumu taifa dhidi ya vita vya uchumi ikiwemo kushirikiana na mabeberu kukamata ndege ili kudhohofisha jitihada za nchi kujikomboa kiuchumi, eti leo ndiyo wanataka wakakae jukwaa moja na Mzalendo namba moja wa nchi, mtetezi wa taifa, mtetezi wa wanyonge. Hapana.

Chadema kupitia Tundu Lissu walizunguka dunia nzima kuishitaki serikali,wakaitukana Serikali kwenye Hard Talk,BBC wakaenda Jumuiya ya Ulaya na Marekani kuombea nchi mabaya ikiwemo kunyimwa misaada ya maendeleo kutoka nchi wahisani, mikopo pamoja na kuitangaza nchi vibaya kuhusu kukiuka haki za binadamu na utawala bora, eti leo ndiyo wanataka kukaa jukwaa moja na Rais Magufuli wanayemwita dikteta. Hapana.

Chadema waliodiriki hata kumzushia Rais wa nchi kifo kutokana na uadui walioujenga kwake, na hawajamwomba radhi kwa kitendo hicho, eti leo ndiyo wanataka wakakae jukwaa moja na Rais? Hapana.

Chadema walisusia sherehe za kuapishwa kwa Rais Magufuli tarehe 05th Nov,2015 pale Uwanja wa Uhuru na kueleza kwamba, hawamtambui kama Rais aliyechaguliwa kidemokrasia kwa kushinda kupitia uchaguzi, leo ndiyo wanasema wako tayari kuhudhuria sherehe za Uhuru, kwa maana wawe karibu au waketi jukwaa moja na Rais wasiyemtambua? Hili halikubaliki.

Chadema ambao wanapinga kila kitu yakiwemo maendeleo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano kwa miaka minne mfululizo kama vile miradi mikubwa ya kiuchumi, ununuzi wa ndege, elimu bure, maji, afya, umeme vijijini, mikopo vyuo vikuu, barabara, fly over, mazao ya wakulima, eti leo ndiyo wanataka kuwa karibu na Rais Magufuli?

Kwa maoni yangu ili tamko la Chadema kushiriki sherehe za uhuru liweze kueleweka kwa Watanzania kwamba lina nia njema, viongozi wa Chadema wangeanza kutekeleza masharti yafuatayo:-

Kwanza, Chadema watambue Rais Magufuli ni Rais halali aliyechaguliwa kidemokrasia na si vinginevyo.

Pili, Chadema watambue na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM hususani katika suala la kufufua uchumi wa nchi, kuwaletea wananchi maendeleo.

Chadema mshiriki kwa vitendo vita dhidi ya rushwa, ufisadi pamoja na kushiriki vita vya uchumi kwa kutoshirikiana na mabeberu wa nje.

Chadema waache kumtukana Rais ikiwa ni pamoja na kumwomba msamaha, kuwaomba msamaha watanzania kutokana na uovu waliofanya kwa nchi hii.

Chadema watamke hadharani kwamba, kuanzia sasa watafanya siasa za ushindani kwa njia ya kistaarabu, kwa kuheshimiana, kwa kushindanisha sera na hoja badala ya matusi na kwamba kiongozi wao au mwanachama wao atakayekwenda kinyume, Chama kitamchukulia hatua za kinidhamu mara moja.

The last kick of a dying horse,Chadema wanajua kua mwisho wao wa kuwa chama kikuu cha upinzani upo karibu, hivyo wanaomba poo kunusuru ruzuku,Kwa hakika Chadema wanastahili kuadhibiwa na Wananchi 2020 ikiwezekana Wananchi wawakatae Wabunge wote watakaogombea kupitia Chadema.

Nimalizie kwa kusema kazi inayofanywa na Rais John Magufuli imemaliza mechi dakika ya kumi badala ya dakika tisini,ni sawa na kusema kazi iliyofanywa na Rais Magufuli imewapiga Chadema kwa KO round ya tatu.

Niwatakie heri ya Sikukuu ya Uhuru.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854
 
Bora umeweka na namba ya simu kabisa, mmeshagundua jamaa ni kama Idi amin Dada ukimsifia tu hata kama hujui kusoma na kuandika anakupa uwaziri.
 
Kwanini una roho ya ubinafsi wewe mrundi!!! Watu wanataka maridhiano ili wajenge nchi we unamwaga petroli au unaona kitumbua chako kinapokonywa ?? Kwani maridhiano yanakukera nini??? Hii nchi ni yako??? Mbona mko hivi wtz yani kuna watu mshajiona wenye haki na keki ya nchi hii kuliko wengine!!!! Pumbavu mkuu
 
Asante sana mkuu huyu jamaa naona ni Mrundi kweli au Mnyarwanda hataki nchi yetu tuishi kwa uhuru na mshikamano
Kwanini una roho ya ubinafsi wewe mrundi!!! Watu wanataka maridhiano ili wajenge nchi we unamwaga petroli au unaona kitumbua chako kinapokonywa ?? Kwani maridhiano yanakukera nini??? Hii nchi ni yako??? Mbona mko hivi wtz yani kuna watu mshajiona wenye haki na keki ya nchi hii kuliko wengine!!!! Pumbavu mkuu
 
Kuna watu sijui ni wana ccm!!? Lkn mwana ccm halisi hawezi kuwa jinga kiasi hiki!! Yani hawataki kuona wapinzani wakishiriki jambo lolote hapa nchini kazi ni kuchochea moto uwake ili wapinzani wasishirikishwe katika ujenzi wa taifa letu,,ccm watafuteni hao virusi muwaonye wanawasha moto ili nani akauzime? Magufuli Leo kajitahidi kuepuka hotuba zake za chuki kitu ambacho kinampandisha chat kisiasa na kuondoa marumbano
 
Mleta uzi huu sijui kapotelea wapi
Mwisho wa uzi zake,alikuwa anakuwekea cv + # ya sim 😄

Ova
 
Mleta uzi huu sijui kapotelea wapi
Mwisho wa uzi zake,alikuwa anakuwekea cv + # ya sim 😄

Ova
Nafasi yahuyu kichaa imechukuliwa na Pumbavu Lucas mwashambwa ..aka Mwasambwanda...cheki huyu Kada original sio feki kama wewe, alikuwa anaweka na namba ya Simu ila Mwisho wasiku alichoka ila wewe siku moja tuu umechoka nakuacha kuweka namba...nyooko wewe
 
Back
Top Bottom