CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Mi simwelewagi pascal kama mwandishi ila simtafautishi sana na kina Ally Yakuut wa bongo muv
Mkuu Hijja Madava, pole kwa kutokunielewa, mambo ya uelewa ni mambo ya uwezo wa brain kwenye ability, capabilities na brain capacity, kwa kifupi ni mambo ya kiwango cha IQ ya uelewa wa mtu. Huwezi kutumia flash disc ya capacity ya 2GB kuingiza material ya 4 G
P
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, hivyo ni kawaida, ukifanya ukosoaji wowote kuihusu Chadema humu jf, utanyooshewa vidole kuwa wewe ni CCM. Nafanya ukosoaji wangu constructively, truthfully with objectivity, impartiality and balancing, hivyo nawashauri Chadema, wawe tayari kupokea na kuuzingatia ushauri wowote, hata kama ushauri huo unatoka kwa kichaa au kwa shetani, ili kujitafakari na kujitathinini, kama inajidhania imesimama, na uiangalie isianguke. CHADEMA msipuuzie ushauri hata kama ni kutoka kwa shetani!, S ...

Utangulizi
Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa Chadema, na unatolewa na mtazamaji wa muda mrefu wa mchezo wa siasa nchini Tanzania, ambaye ameangalia tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania, uchaguzi wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa 1995, 2000, 2005, 2010, na 2015. Ushauri wenyewe ni kuhusu hii hama hama ya wanachama na viongozi wa Chadema kuhamia CCM. Naishauri Chadema Wajitafakari!, Wasiwabeze Wanaohama Kama Wafanyavyo CCM, Wanaohama Chadema, Wana Hoja za Msingi, Chadema Wanadhani Adui Yao Mkuu Anaowanya Kushindwa Kwenda Ikulu ni CCM, Kiukweli Adui Mkuu wa Chadema Sio CCM, Nitawatajia Adui Mkuu wa Chadema, na Mwisho Nitawapa Ushauri Chadema Wafanye Nini, Waweze Kuingia Ikulu 2025 Magufuli atakapomaliza and only if Magufuli atamaliza 2025!, kwa sababu haya ninayoshauri, kwa uchaguzi wa 2020, saa hizi tayari ni too little too late, na Magufuli ni just too powerful kiasi kwanza hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, uchaguzi wa rais wa 2020 utakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, lakini mshindi tayari ni Magufuli, hivyo wote watakaompinga Magufuli 2020, itakuwa ni kujifurahisha tuu, hivyo Chadema Watake Wasitake, Lazima Wabadilike, Vinginevyo...its the end of the road kwa Chadema, tunarudi kwenye nchi ya Chama Kimoja.

Why Chadema?
Tanzania japo tuna vyama vya siasa zaidi ya 22, lakini vyama vikubwa ni CCM, Chadema na CUF, by now CUF is already a gone case, hivyo tunapozungumzia upinzani Tanzania, tunazungumzia Chadema. Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee ...

Justification ya Kuikosoa Chadema kwa Mtu Ambaye Sii Mwanachama.
Mashabiki na manazi wa Chadema humu jukwaani, ukifanya ukosoaji wa Chadema, au kutoa ushauri wowote kuhusu Chadema, watakubeza unashauri kama nani?. Kwa sababu Chadema ni public party paid by taxpayers money, then the taxpayers have the right to know the conduct of their tax, hivyo Watanzania wote wana right kujua mambo yote ya Chadema, public na private, ni haki yao kwa sababu kinaendeshwa kwa kodi zao!.

Kwanini Uishauri Chadema, Kwa Wao Wenyewe Hawajioni na Kujishauri?.
Ushauri huu nautoa kwa dhana kuwa Viongozi wa Chadema, wanachama wao, wafuasi wao, washabiki wao na manazi wa Chadema humu jf, wote ni pro Chadema, wako ndani ya box la Chadema, hivyo wanaweza wasiwe na uwezo wa kuona nje ya box, soso tulioko nje ya box ambao ni watazamaji, tunaweza kuwa tunaiona Chadema vizuri Zaidi kwa nje, kuliko waliomo ndani ya chama, lakini pia kuna walioko ndani, wanayaona madhaifu na mapungufu ya Chadema from within, lakini kwa vile wamo, wanakosa objectivity ya kujiambia, kujitathinini na kujikosoa, hata hivyo tathmini ya kweli, inapaswa ifanywe na watu wa nje na sio kujitathmini yenyewe.

Chadema Isiwabeze Wanaohama, Ni Haki Yao, Ila Pia Izingatie Hoja Zao, Wana Hoja za Msingi
Kati ya wanachama na viongozi wa Chadema wanaohamia CCM, kuna wengine wanahama kimya kimya bila kusema sababu, kuna wengine wananunuliwa, na kuna wengine na haswa baadhi ya viongozi, wanapohama, wanaandika barua Chadema na kuaga kwa kutoa sababu, ziwe ni sababu za kweli au ni visingizio tuu, lakini kuna kitu wanasema, na wengine hawasemi chochote kuhusu Chadema lakini siku wanapokelewa CCM, Chadema, japo ni kweli wengi kinachowahamisha Chadema ni njaa zao tuu, na wanakwenda CCM kufukuzia fursa, lakini kuna baadhi, wana hoja za msingi sana, hivyo Chadema inatakiwa kutozipuuza hoja zao, isisikilize na kujitathmini kuhusu ukweli wa hoja hizo.

A Way Forward, Chadema Ifanye Nini.
  1. Kwanza Chadema ijitathmini, is it on the right track?, itambue makosa yake, ikubali makosa, ijirekebishe, isonge mbele. CHADEMA ni sikio la kufa? Iambiwe vipi ili isikie? Masha ana hoja za msingi, zisikilizwe, zizingatiwe, zisipuuzwe!
  2. Ianzishe grassroots recruitment ya wanachama wake waaminifu, isije kujikuta imewakumbatia CCM ndani, Chadema nje hadi ndani ya CC yake, kama ilivyotokea kwa Mwenyekiti wa Bavicha.
  3. Ianzishe headhunting na spotting leadership talents na able people toka kwenye jamii kujiunga Chadema na kujenga kada ya viongozi wake wa kesho, born and breed in Chadema, kwa kuwafanyia grooming, ili kupata wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi.
  4. Ipunguze kushobokea makapi kutoka CCM, wana CCM wanaojitoa CCM na kujinga Chadema, wawe wanachama wa kawaida tuu kama wanachadema wengine na sio kupapatikiwa na kupewa uongozi moja kwa moja.
  5. Chadema I invest on people na mass mobilization, na sio ku invest on vitu na mikutano tuu ya hadhara, kupitia social media na kumiliki media yake yenyewe, kutawafikia watu wengi Zaidi kuliko kutegemea mikutano na maandamano pekee.
  6. Chadema irudishe ukomo wa uongozi, hata kiongozi awe mzuri vipi, anafikia kiwango cha ukomo wake na kuwa kama saturated solution, he can do no more than what he can!, anakuwa hana jipya!, pia Chadema waandae succession plan, by now, wawe na a pool of able people from within kushika nafasi zote za uongozi, na kuendesha serikali, kungekuwa na ukomo, by now watu wangejua Mbowe amefikia ukomo wa uwezo wake, hivyo nani watampokea.
  7. CCM ni chama dola, hivyo Chadema isitumie model ya CCM kuitafuta ikulu, iandae model yake yenyewe ya kupata viongozi wake na wagombea wake, mtindo wa the democrats ya US ni mzuri kuanzia kwenye primaries.
  8. Kuondokana na viongozi ving'ang'anizi na miungu watu, maadamtarget ni kuingia ikulu, umeshindwa kuuingiza Chadema ikulu, unapisha wengine wanaendeleza, sio umeshindwa hala unang'ang'ania!.
  9. Kuwafanyia tathmini wabunge wake na kukubalika kwao, na kuwe hakuna haki miliki ya majimbo, mfano 2020, Mdee anatathminiwa amefanya nini Kawe for 10 years, na jee bado anakubalika?, Wanachadema wote wenye uwezo, wawe huru kumchallenge Mdee, akitokea mwanachama mwingine mwenye sifa Zaidi, uwezo Zaidi na kukubalika Zaidi, Mdee anawekwa pembeni, vinginevyo 2020, kuna majimbo kibao Chadema mtayarudisha CCM!.
  10. Chadema kionyeshe ukomavu na kuwa ni chama mbadala kwa kuachana na cheap politics ya siasa za matukio, na kujikita kwenye real politics ya kushindanisha sera, sio kwa kupinga kila kitu, CCM ikifanya mazuri, mfano elimu bure, Chadema ikubali hili ni zuri, lakini ionyeshe ingekuwa Chadema ingefanya bora zaidi kwa elimu bure hadi chuo kikuu, kwa kuonyesha how CCM inatapanya fedha kwa mambo yasiyo na maana, halafu inanyanyasa Watanzania masikini kwa kuwanyima mikopo. Chadema wajifunze kuibomoa CCM kwa hoja na sio siasa za matukio, mfano mwaka 2020, Magufuli anaingia ulingoni akiwa na elimu bure, ndege za ATCL zinapaa dunia nzima, flyovers, reli ya SGR, na Tanzania ya viwanda. Chadema lazima waje na sera mbadala kuonyesha jinsi ATCL, flyovers na SGR zilivyowatia umasikini Tanzania, kama fedha hizo zingewekezwa kwenye sekta ya kilimo nini kingepatikana, bila kuinua sekta ya kilimo, hiyo Tanzania ni Tanzania ya viwanda gani vinavyotumia malighafi gani?. Ijikite kwenye hoja kama hizi Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
  11. Chadema ipiganie a level playing field kwenye the political ground, kupitia tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, haiwezekani watu wawili wanagombea urais, mgombea mmoja anakuja na vingora, na full government media team, paid by public money for the advantage ya CCM, halafu, mwingine with nothing, halafu utegemee kushinda!.
  12. Chadema ipiganie true free and fair elections with maximum transparency, kama hakuna manouvers zozote zinazofanywa na Tume ya Uchaguzi, kwa nini wazueie party tallying?, wanaogopa nini, kama matokeo yote hadi ya urais yanabandikwa vituoni mbele ya mawakala wa vyama, kuna kosa gabi kama mawakala wote watakuwa na smart phones, ku scan matokeo na kutuma makao makuu kwenye tallycenters za vyama, kama haki itatendeka, then tallying za vyama zitafana na tallying ya NEC, what is it there to hide kuzuia tallying?.
  13. Chadema kutimiza majukumu yake kikamilifu kama Chama cha upinzani kazi yake sio tuu kuikosoa serikali, bali ku I check serikali kuhakikisha inafuata katiba na kutekeleza sharia, taratibu na kanuni, mfano, katika kuzuia mikutano ya kisiasa, rais Magufuli amevunja katiba wazi wazi kabisa mchana kweupe!, chama chochote makini, by now, kingeifungua shauri mahakamani, ili mahakama itoe tafsiri rasmi, kama itathibitisha rais amevunja katiba, anashitakiwa na bunge, na kuondolewa madarakani!. Mfano hata suala dogo tuu kama Daudi Bashite, nilishauri Je, wajua suala vyeti vya Bashite, linaweza kabisa kumng'oa Rais ...
  14. Chadema waipinge CCM kwa kujikita kwenye hoja zenye maslahi kwa taifa, ujinga, umasikini, maradhi, rushwa na ufisadi, kwa kuonyeshea CCM katika kipindi chote cha miaka 50, CCM imeshindwa, na katika rushwa na ufisadi, Chadema iwaeleze wananchi, CCM ndio shina na mlezi wa rushwa zote na mafisadi karibu wote ni CCM!, ili wananchi waelewe kuwa CCM inapigana vita ilivyovilea na kuvijenga.
Ni hayo kwa uchache, nikikumbuka mengine nitayaongeza.

Paskali
Swadakta umenena
 
Viongozi wa Chadema katika mikoa uliyotaja 85% wanatokea mkoa mmoja wa kaskazini. Hata mbunge wa ilemela katika mwaka ulioutaja alitokea mkoa huo huo wa kaskazini!
Inawezekana ikawa kweli. Lkn je waliomchagua yule ya Ilemela, ni kuwa watu wa kaskazini ni wengi kuliko wa mwanza? Kutokana na hilo ndio maana wamechagua wa Mwanza? Je Yule wa kaskazni hana sifa ya kuomba uongozi mahali popote Tanzania? Dhana hizi ndio zinaleta ukabila hata Mwalimu nyerere aliwahi kukumbana nayo Kagera mwaka 1995, na kukemea kwa mitazamo ya kuchaguana kwa ukabila. Tunakoepeleka nchi hii kwa muktadha wa ubaguzi tutajuta. Na niseme tu kuwa Waanzilishi wa hii mitazamo ya kibaguzi ni wale walio madarakani.

Hata wakati wa harakati za kudai vyama vingi walitishia wananchi kuwa vyama vingi vitaleta vita, wananchi wa vijijni kwa kutokuwa na elimu ya kutosha wametishwa. CUF nayo ilisilibwa kuwa chama cha udini, na sasa wanasem CD ni cha ukanda na waanzilishi ni walio madarakani. Sasa imeingia ndani ya chama na serikali na watu wanaamini hivyo kuwa teuzi za kikabila mara kidini. Na kama kweli kuna viongozi wapo wanaofanya hivyo na kufanya teuzi kwa misingi hiyo, hawalitakii mema taifa letu.
 
Hakuna CHADEMA ilipo kosea labda kama hoja yako imekaa kinafiki nafiki wakati ukweli unaujua , CCM Inatumia rushwa wazi wazi tena kwa kukiri kabisa na haichukuliwi hatua , wanatumia jeshi la polisi kukandamiza upinzan kwa nguvu zote na kuvuruga uchaguzi wa uhuru na haki

wanatumia vijana wa kihuni kushambulia wapinzani na kuwajeruhi na kuwaua pamoja na kuwateka mbele polisi Ref: arumeru na hakuna hatua yeyote imechukuliwa ,wanatumia sijui watu gani**** kuteka na kupotezea watu kusiko julikana na wengine kuvizia upizani na kufyatulia risasi hadharani Ref: tundu lissu, nassari leo hapo bado takukuru hawafanyii uchunguzi swala lolote linalo husu upinzani zaid zaid takukuru itawatishia upinzani Ref: tukio la nassari na ushahid wa rushwa, bado mahakama itapiga dana dana mashauri yanayo husu chadema ,,wakati huo tume ya uchaguzi inaendeleza usanii wake wa kukandamiza upinzani bado bunge nalo halijaja na kauli mbiu ya '' wewe wabane bungeni mimi nitawashughulikia huku nje'' hahahhaaa

halafu eti mjinga mmoja sijui kichaa anatoka huko aliko toka kuuliza chadema imekosea wapi?!? Wewe lazima utakuwa mwendawazimu. Hilo swali ungeuliza kama vyama vyote biwe na uhuru sawa pasipo mbeleko ya jeshi la polisi ,tume ya uchaguzi, bunge na mahakama
Dah.....
75859ccad6e8b9de2d788ce89c9b05de.jpg
 
Sasa assume wewe ndio upinzani tanzania unadhan nje na vyombo vya habari ungelalamikia wapi? Maan polisi hawako upande wako ,mahakama tia maji tia maji tume haiko upande wako nankote ukipeleka taatifa au ukilalamika huko hawatoi msaada wowote mfa. Nassari alitoa taarifa juu ya tukio la rushwa na video clip akawasilisha na muhusika akakiri tena mbele ya media na hakuna kilicho fanyika bado utaendelea kupeleka malalamiko yako hukko? Swala la lissu jee lipo kwenyw vyombo husika nini kinaendelea hadi sasa, walio tekwa ! Taatifa zipo sehwemu husika nini kimefanyika, wanao vamia mikutano ya upinzan tena na silaha za moto na wengine na sare kabisa je jeshi na vyombo husika vimetoa msaada gani

, bungeni nako wakisema waoingee madhila yao mara wametolewa nje au kunyimwa nafasi za kuchagia bungen na wameenda mbali zaid kuwafungia kuhudhuria vikao bungeni sasa wafanye nini, mtaani nako wanawindwa tuu Mara watekwe mara wakatwe mapanga ,mara wauawe ref, mawazo na kilicho taka kumtokea lissu ? Hebu fanya kama wewe ndio ungekuwa upinzani ungefanyaje kwa mfano? Unajua kuna wakati tukiacha siasa tukaongea ukweli kabisa upinzani wana nyanyasika sana hasa kwa siasa na nchi za afrika na hii ni kutokana na nchi hizo kuto kuwa na utaayari wa kuipokea democracy kwa mikono miwili.

Ni sawa na mtoto yatima baba anamtesa ,mama anamtesa kina dada wamnamtesa anaona bora kueleza kero zake kwa majiran na jamaa wa karibu ili kupunguza maumivu ya moyo maana wote wenye uwezo wa kumsaidia hawana mda nae malalamiko yake yote yatiwa kapuni

Na nilazima wawe na malalamiko maana ile democrasia halisi inayo takiwa kuwepo haipo kabisa yani
ushauri mzuri mkuu Kkimondoa chadema ihamie kenya kwenye demokrasia na tume huru!
 
Paskali mi nakubaliana nawe kwa hoja nyingi ila chache nitakataa, nianze na za kukataa,
1. Kama chama hakijatengeneza succession plan ni kazi ngumu kutengeneza mazingira ya kuachiana uongozi, yes nakubaliana nawe kwamba mfano hata kama mbowe ni mzuri wa fikra kuliko malaika lazima aondoke aje mwingine, lakini katika mazingira ya sasa hivi simuoni mtu imara na thabiti wa kumkabidhi Chama. Kabwe alikuwa anataka uenyekiti mfano siku chache badae unaona anapokea hongo toka chama kingine kuizamisha chadema, uongozi kwenye nchi ya wenye njaa kama hii lazima uwe makini na nani unampa nini.
2. Swala la chadema kupigania mambo ya msingi kwa taifa nadhani wamefanya labda kama sio kwa level zinazotakiwa lakini wamefanya.
3. Kujipambanua kama chama mbadala badala ya kukosoa kila kinachofanywa, nadhani hilo nalo linafanyika vizuri kwa kuanisha ni wapi chadema wangefanyaje tofauti na wenzao wa upande wa pili na ndo maana kama utafuatili siasa Za serialized ya tano kwa sasa asilimia kubwa inatekelezwa ilani ya chadema lakini pengine kwa staili tofauti Sana.
4. Kuingia ikulu bila kupigania tume ya uchaguzi na katiba mpya ni kazi ngumu nakubaliana sana lakini kama sio mapambano ya hayo mambo tusingekuwa na msamiati unaoitwa ukawa hivyo ni wazi katika eneo hilo pengine chadema wana alama tena nyingi.
Hata hivyo kwa mazingira ya sasa huwezi kudai katiba wala tume huru ya uchaguzi labda kama unataka unrestishwe in peace.
Mambo ninayokubaliana ni mengi sana ila nitaandika machache tu
1. Chadema kujitathimini mwenendo wake na aina ya siasa zinazofanywa na chama hicho na kwa wakati huu
a) Siasa za kiharakati sio aina ya siasa kwa mtizamo wangu za kuendekezwa na chama kinachojiandaa kushika doll.
b) Kuwaamini viongozi wa juu na maamuzi yao yakawa kama ni maamuzi ya chama kizima huu ni udikteta ambao unaambatana na kufanya maamuzi makubwa nje ya Katiba.
2.Kuiga karibia kila kitu kutoka ccm ikiwemo namna ya upatikanaji wa wagombea wao, hili tatizo kubwa Sana labda pale ambapo ni utaratibu umewekwa na katiba ya nchi.
Kwa leo naomba kuwasilisha haya tu.
Mimi sio mwanachama wa Chama chochote cha siasi ila natamani kuona upinzani wenye nguvu kwa nia ama ya kukomboa taifa au kukiamsha usingizini chama tawala kututumikia watanzania
Itoshe kusema Wajipambanue kisayansi ni kweli tunahitaji upinzani kwa zama hizi lakini siyo upinzani wa Kiharakati ambapo kila mtu anakuwa msemaji wa Chama (Publicity Secretary of a Party) Wabadilike wachukue hatua Kujitolea kuwe na mipaka yake
 
Wanahama kwa hofu ya kuuwa na ccm hakuna kingine
Lkn lawama nyingi sana ziwaendee waandishi wa habari wamekuwa wachumia tumbo wenye kujipendekeza wameukimbia ukweli na kuukumbatia uongo wamekuwa sehemu ya mazambi ya kuuwawa na kutekwa kwa wapinzani ikiwa kazi yao ni kusema kweli leo wamekuwa waoga wameufyata wamegeuka kuwa watumwa wa zambi na ndo maana hata kristo aliwaonya juu ya matendo yao ya kuunga mkono uongo lkn hakika laana na mateso haya yatawafuaata kule waliko na majibu yake ni hapahapa kabla ya mauti yao,leo mnajificha lkn kesho ni yenu mmbarikiwe sana enyi kina pasko mayara
 
1. Siamini kama wanachama wakiamua kuhama chama cha siasa na kujiunga na chama kingine ni lazima kwenye chama wanachohama kunakuwa kumefanyika makosa. Actually, wakati mwingine wanaohama wanaweza pia wakawa na sababu zao na wanaweza kusema sababu ni x, y na z, lakini je ni kweli ndizo sababu "hasa" zilizowafanya wahame au kuna pia sababu zingine ambazo hazitajwa hadharani - mfano kuahidiwa greener pastures kwenye chama kingine au kupata protection ya kutosha? Nakumbuka kuna mwanaCCM mmoja aliyehamia Chadema na wakati akiwa Chadema alikuwa akiikosoa serikali na kwa kutumia uzoefu wake serikalini, alikuwa akisema anajua mambo mengi. Alipoamua kurudi CCM, moja ya mambo aliyoyataja ni kuikosoa serikali kwamba si sahihi (jinsi nilivyomwelewa).

2. Kwa upande wangu, kwenye ushindani kila mtu anatumia mbinu mbalimbali na kwa bahati mbaya vyama vya upinzani kwa sasa vina mtihani mgumu kwa upande wa kujinadi na kupata wanachama wapya na hili si kosa la vyama hivi hata kidogo (maana liko nje ya matakwa yao). Na hili pia lina matokeo hasi kwa vyama vya upinzani. Hivyo, kwa baadhi ya mambo yanayotokea hatuwezi kusema vyama vya upinzani vimekosea. Inabidi pia tuone sehemu ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwa afya ya vyama vya upinzani na tuseme kwamba hali hii inaathiri ustawi wa vyama hivi ingawa kinachofanyika si kwa matakwa yao.

3. Na tusipokuwa na vyama vya siasa vyenye ushindani ili kuikosoa serikali na kuifanya iwajibike vizuri zaidi kwa wananchi, ina maana waathirika ni sisi wenyewe. Hivyo, mtu anayefurahia kufa kwa vyama vya upinzani ni sawa na anayekata tawi alilokalia.

4. Mwanachama akihama chama chake na kujiunga na chama kingine siyo kapi na asionekane kapi (labda iwe dhahiri kwamba hana au amekosa sifa za kuwa mwanachama wa chama cha siasa). Lakini kama sababu ni kutofautiana na chama chake na kufukuzana, kwangu mimi kwa mwanachama kama huyu si kapi hata kama chama chake cha awali kitamwona kama ni kapi. Kwangu mimi, kapi ni mtu asiye na sifa za kuwa mwanasiasa (hafai). Nasema hivi, kwa sababu hata sisi hapa tulipo tumetoka sehemu mbalimbali na kwa sababu tumetoka sehemu hizo hakutufanyi tukose sifa za kuwa tulipo leo hii unless kama tumepoteza sifa za kuwa kwenye ajira (kama hilo linawezekana).

5. Ukomavu wa kisiasa ni mchakato - inachukua muda kwa sababu kuna sababu nyingi zinachangia kufikia huu ukomavu. Mimi niseme tu kwamba vyama vya upinzani vimefanya kazi kubwa na visikate tamaa pamoja na kwamba vinakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na kukosekana kwa a 'level political ground'.
Kihistoria ni kazi kikiondoa chama kilicho madarakani kwa mda mrefu kama ilivyokuwa kazi ngumu kumuondoa mkoloni ilikuwa toka enzi ya mkwawa mpaka nyerere.hivyo safari ya kuiondoa ccm ni ngumu kama ilivyo kuondoa utawala wa simba na yanga kwenye mpira ikumbukwe watu wanakimbilia kwenye fursa.
 
... nyingi sana ziwaendee waandishi wa habari wamekuwa wenye ukweli na wamekuwa sehemu ya kazi yao ni kusema kweli leo na ndo maana hata kristo aliona juu ya matendo yao ya kuunga mkono haya kule waliko na majibu yake hapahapa, mmbarikiwe sana enyi kina pasko mayara
Amen.
P.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, hivyo ni kawaida, ukifanya ukosoaji wowote kuihusu Chadema humu jf, utanyooshewa vidole kuwa wewe ni CCM. Nafanya ukosoaji wangu constructively, truthfully with objectivity, impartiality and balancing, hivyo nawashauri Chadema, wawe tayari kupokea na kuuzingatia ushauri wowote, hata kama ushauri huo unatoka kwa kichaa au kwa shetani, ili kujitafakari na kujitathinini, kama inajidhania imesimama, na uiangalie isianguke. CHADEMA msipuuzie ushauri hata kama ni kutoka kwa shetani!, S ...

Utangulizi
Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa Chadema, na unatolewa na mtazamaji wa muda mrefu wa mchezo wa siasa nchini Tanzania, ambaye ameangalia tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania, uchaguzi wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa 1995, 2000, 2005, 2010, na 2015. Ushauri wenyewe ni kuhusu hii hama hama ya wanachama na viongozi wa Chadema kuhamia CCM. Naishauri Chadema Wajitafakari!, Wasiwabeze Wanaohama Kama Wafanyavyo CCM, Wanaohama Chadema, Wana Hoja za Msingi, Chadema Wanadhani Adui Yao Mkuu Anaowanya Kushindwa Kwenda Ikulu ni CCM, Kiukweli Adui Mkuu wa Chadema Sio CCM, Nitawatajia Adui Mkuu wa Chadema, na Mwisho Nitawapa Ushauri Chadema Wafanye Nini, Waweze Kuingia Ikulu 2025 Magufuli atakapomaliza and only if Magufuli atamaliza 2025!, kwa sababu haya ninayoshauri, kwa uchaguzi wa 2020, saa hizi tayari ni too little too late, na Magufuli ni just too powerful kiasi kwanza hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, uchaguzi wa rais wa 2020 utakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, lakini mshindi tayari ni Magufuli, hivyo wote watakaompinga Magufuli 2020, itakuwa ni kujifurahisha tuu, hivyo Chadema Watake Wasitake, Lazima Wabadilike, Vinginevyo...its the end of the road kwa Chadema, tunarudi kwenye nchi ya Chama Kimoja.

Why Chadema?
Tanzania japo tuna vyama vya siasa zaidi ya 22, lakini vyama vikubwa ni CCM, Chadema na CUF, by now CUF is already a gone case, hivyo tunapozungumzia upinzani Tanzania, tunazungumzia Chadema. Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee ...

Justification ya Kuikosoa Chadema kwa Mtu Ambaye Sii Mwanachama.
Mashabiki na manazi wa Chadema humu jukwaani, ukifanya ukosoaji wa Chadema, au kutoa ushauri wowote kuhusu Chadema, watakubeza unashauri kama nani?. Kwa sababu Chadema ni public party paid by taxpayers money, then the taxpayers have the right to know the conduct of their tax, hivyo Watanzania wote wana right kujua mambo yote ya Chadema, public na private, ni haki yao kwa sababu kinaendeshwa kwa kodi zao!.

Kwanini Uishauri Chadema, Kwa Wao Wenyewe Hawajioni na Kujishauri?.
Ushauri huu nautoa kwa dhana kuwa Viongozi wa Chadema, wanachama wao, wafuasi wao, washabiki wao na manazi wa Chadema humu jf, wote ni pro Chadema, wako ndani ya box la Chadema, hivyo wanaweza wasiwe na uwezo wa kuona nje ya box, soso tulioko nje ya box ambao ni watazamaji, tunaweza kuwa tunaiona Chadema vizuri Zaidi kwa nje, kuliko waliomo ndani ya chama, lakini pia kuna walioko ndani, wanayaona madhaifu na mapungufu ya Chadema from within, lakini kwa vile wamo, wanakosa objectivity ya kujiambia, kujitathinini na kujikosoa, hata hivyo tathmini ya kweli, inapaswa ifanywe na watu wa nje na sio kujitathmini yenyewe.

Chadema Isiwabeze Wanaohama, Ni Haki Yao, Ila Pia Izingatie Hoja Zao, Wana Hoja za Msingi
Kati ya wanachama na viongozi wa Chadema wanaohamia CCM, kuna wengine wanahama kimya kimya bila kusema sababu, kuna wengine wananunuliwa, na kuna wengine na haswa baadhi ya viongozi, wanapohama, wanaandika barua Chadema na kuaga kwa kutoa sababu, ziwe ni sababu za kweli au ni visingizio tuu, lakini kuna kitu wanasema, na wengine hawasemi chochote kuhusu Chadema lakini siku wanapokelewa CCM, Chadema, japo ni kweli wengi kinachowahamisha Chadema ni njaa zao tuu, na wanakwenda CCM kufukuzia fursa, lakini kuna baadhi, wana hoja za msingi sana, hivyo Chadema inatakiwa kutozipuuza hoja zao, isisikilize na kujitathmini kuhusu ukweli wa hoja hizo.

A Way Forward, Chadema Ifanye Nini.
  1. Kwanza Chadema ijitathmini, is it on the right track?, itambue makosa yake, ikubali makosa, ijirekebishe, isonge mbele. CHADEMA ni sikio la kufa? Iambiwe vipi ili isikie? Masha ana hoja za msingi, zisikilizwe, zizingatiwe, zisipuuzwe!
  2. Ianzishe grassroots recruitment ya wanachama wake waaminifu, isije kujikuta imewakumbatia CCM ndani, Chadema nje hadi ndani ya CC yake, kama ilivyotokea kwa Mwenyekiti wa Bavicha.
  3. Ianzishe headhunting na spotting leadership talents na able people toka kwenye jamii kujiunga Chadema na kujenga kada ya viongozi wake wa kesho, born and breed in Chadema, kwa kuwafanyia grooming, ili kupata wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi.
  4. Ipunguze kushobokea makapi kutoka CCM, wana CCM wanaojitoa CCM na kujinga Chadema, wawe wanachama wa kawaida tuu kama wanachadema wengine na sio kupapatikiwa na kupewa uongozi moja kwa moja.
  5. Chadema I invest on people na mass mobilization, na sio ku invest on vitu na mikutano tuu ya hadhara, kupitia social media na kumiliki media yake yenyewe, kutawafikia watu wengi Zaidi kuliko kutegemea mikutano na maandamano pekee.
  6. Chadema irudishe ukomo wa uongozi, hata kiongozi awe mzuri vipi, anafikia kiwango cha ukomo wake na kuwa kama saturated solution, he can do no more than what he can!, anakuwa hana jipya!, pia Chadema waandae succession plan, by now, wawe na a pool of able people from within kushika nafasi zote za uongozi, na kuendesha serikali, kungekuwa na ukomo, by now watu wangejua Mbowe amefikia ukomo wa uwezo wake, hivyo nani watampokea.
  7. CCM ni chama dola, hivyo Chadema isitumie model ya CCM kuitafuta ikulu, iandae model yake yenyewe ya kupata viongozi wake na wagombea wake, mtindo wa the democrats ya US ni mzuri kuanzia kwenye primaries.
  8. Kuondokana na viongozi ving'ang'anizi na miungu watu, maadamtarget ni kuingia ikulu, umeshindwa kuuingiza Chadema ikulu, unapisha wengine wanaendeleza, sio umeshindwa hala unang'ang'ania!.
  9. Kuwafanyia tathmini wabunge wake na kukubalika kwao, na kuwe hakuna haki miliki ya majimbo, mfano 2020, Mdee anatathminiwa amefanya nini Kawe for 10 years, na jee bado anakubalika?, Wanachadema wote wenye uwezo, wawe huru kumchallenge Mdee, akitokea mwanachama mwingine mwenye sifa Zaidi, uwezo Zaidi na kukubalika Zaidi, Mdee anawekwa pembeni, vinginevyo 2020, kuna majimbo kibao Chadema mtayarudisha CCM!.
  10. Chadema kionyeshe ukomavu na kuwa ni chama mbadala kwa kuachana na cheap politics ya siasa za matukio, na kujikita kwenye real politics ya kushindanisha sera, sio kwa kupinga kila kitu, CCM ikifanya mazuri, mfano elimu bure, Chadema ikubali hili ni zuri, lakini ionyeshe ingekuwa Chadema ingefanya bora zaidi kwa elimu bure hadi chuo kikuu, kwa kuonyesha how CCM inatapanya fedha kwa mambo yasiyo na maana, halafu inanyanyasa Watanzania masikini kwa kuwanyima mikopo. Chadema wajifunze kuibomoa CCM kwa hoja na sio siasa za matukio, mfano mwaka 2020, Magufuli anaingia ulingoni akiwa na elimu bure, ndege za ATCL zinapaa dunia nzima, flyovers, reli ya SGR, na Tanzania ya viwanda. Chadema lazima waje na sera mbadala kuonyesha jinsi ATCL, flyovers na SGR zilivyowatia umasikini Tanzania, kama fedha hizo zingewekezwa kwenye sekta ya kilimo nini kingepatikana, bila kuinua sekta ya kilimo, hiyo Tanzania ni Tanzania ya viwanda gani vinavyotumia malighafi gani?. Ijikite kwenye hoja kama hizi Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
  11. Chadema ipiganie a level playing field kwenye the political ground, kupitia tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, haiwezekani watu wawili wanagombea urais, mgombea mmoja anakuja na vingora, na full government media team, paid by public money for the advantage ya CCM, halafu, mwingine with nothing, halafu utegemee kushinda!.
  12. Chadema ipiganie true free and fair elections with maximum transparency, kama hakuna manouvers zozote zinazofanywa na Tume ya Uchaguzi, kwa nini wazueie party tallying?, wanaogopa nini, kama matokeo yote hadi ya urais yanabandikwa vituoni mbele ya mawakala wa vyama, kuna kosa gabi kama mawakala wote watakuwa na smart phones, ku scan matokeo na kutuma makao makuu kwenye tallycenters za vyama, kama haki itatendeka, then tallying za vyama zitafana na tallying ya NEC, what is it there to hide kuzuia tallying?.
  13. Chadema kutimiza majukumu yake kikamilifu kama Chama cha upinzani kazi yake sio tuu kuikosoa serikali, bali ku I check serikali kuhakikisha inafuata katiba na kutekeleza sharia, taratibu na kanuni, mfano, katika kuzuia mikutano ya kisiasa, rais Magufuli amevunja katiba wazi wazi kabisa mchana kweupe!, chama chochote makini, by now, kingeifungua shauri mahakamani, ili mahakama itoe tafsiri rasmi, kama itathibitisha rais amevunja katiba, anashitakiwa na bunge, na kuondolewa madarakani!. Mfano hata suala dogo tuu kama Daudi Bashite, nilishauri Je, wajua suala vyeti vya Bashite, linaweza kabisa kumng'oa Rais ...
  14. Chadema waipinge CCM kwa kujikita kwenye hoja zenye maslahi kwa taifa, ujinga, umasikini, maradhi, rushwa na ufisadi, kwa kuonyeshea CCM katika kipindi chote cha miaka 50, CCM imeshindwa, na katika rushwa na ufisadi, Chadema iwaeleze wananchi, CCM ndio shina na mlezi wa rushwa zote na mafisadi karibu wote ni CCM!, ili wananchi waelewe kuwa CCM inapigana vita ilivyovilea na kuvijenga.
Ni hayo kwa uchache, nikikumbuka mengine nitayaongeza.

Paskali
MAYALLA bwana na hoja zako ni za kipuuzi kweli!. Sasa kuhama kwa mtu si ni kitu cha kawaida sana kwenye siasa....watu wangapi wametoka ccm wamejiunga na upizani. Uwe unaleta issue za msinngi humu ndani, ukiendelea hoja nyepesi na zakijinga namna hiyo utakosa hata watu wa kupitia page yako. Just be independent!
 
Uzi huu nimrukubali kabisa na naona it is a way forward kwetu sisi cdm kuona namna ya kumkabili adui huyu wa haki. Hakuna taabu tena kuona kuwa ccm umeshindwa kuongoza nchi. Hili huambiwi bali unaliona mwenyewe. Kwa kutumia dola kupata ushindi hiyo ni kukataliwa kabisa. Kwa hiyo cdm ina chance kubwa kuja na new strategy ya kuiondoa ccm maana wameshagundua kuwa njia tulionayo ni Democratic na tumeona kuwa kama ilivyo kwa nchi za kiafrica democrasia is a dream. Kwa namna hiyo basi mayalla nakuunga mkono sasa kama tumenyimwa rally sio kunung'unika na kulalama chi kwa chini. Tueendeni na utaratibu mwingine. Twende mlango kwa mlango, dirisha kwa dirisha geti kwa get I tuwaelimishe wa Tanzania. Cdm media sasa ndiyo wakati wake. Miaka mitatu still enough to crap what we are losing.
 
MAYALLA bwana na hoja zako ni za kipuuzi kweli!. Sasa kuhama kwa mtu si ni kitu cha kawaida sana kwenye siasa....watu wangapi wametoka ccm wamejiunga na upizani. Uwe unaleta issue za msinngi humu ndani, ukiendelea hoja nyepesi na zakijinga namna hiyo utakosa hata watu wa kupitia page yako. Just be independent!

Mpendwa usigrash mawazo ya mtu. Yawe mabaya au mazuri. Uziwe sungura mjanja sisitaki mbovu zile. Chuja na utupe makapi mazuri fanyia kazi. Kama wewe yawekana sijui nafasi yako kwenye chama. Lkn kama ni kiongozi basi Mayalla karusha niwe limekupata, kama ni mwanachama vile vile. Asante
 
Kaka Pascal Mayalla, nakubaliana na hoja yako. Lakini, ugonjwa mkubwa uliobaki na kuwasumbua CHADEMA ni kuwepo kwa Lowassa na kundi lake. Kundi la Lowassa likiondoka kwa kuhamia chama kingine au kuanzisha chama chao, CHADEMA itarejea kwenye njia yake. Hakika, uwepo wa Lowassa na kundi lake ni jambo gumu sana kwa CHADEMA kwakuwa inakuwa na muda mwingi wa kujibu tuhuma kuliko kujijenga.

Kiongozi, CHADEMA wanapukutika kwa sababu nyingi - ung'ang'anizi wa madaraka na uongozi (Fikiria hazina yake iliyoondoka kwa sababu ya kukosa matumaini ya uongozi); jambo lingine ni kukosa material people wenye uwezo wa kufanya analysis (Kiuchumi, Kijamii, na Kisiasa - wao hawaoni iwapo zama zinabadilika - wanataka waingie Ikulu kwa style za kampeni za 1995). Mayalla kafafanua vizuri sana
 
Nimekuelewa vizur sana ni muda wa kurudi nyuma kujipanga kwa sasa hata wanaohama huwezi kushikilia hoja ya manunuzi kiasi flani pumzi imekata kitendo cha kuchukua makap ya ccm na kuyapa uongozi.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, hivyo ni kawaida humu jf, mtu ukifanya ukosoaji wowote kuihusu Chadema humu jf, utanyooshewa vidole kuwa wewe ni CCM. Nafanya ukosoaji wangu constructively, truthfully with objectivity, impartiality and balancing, bila kuwajali hawa manazi wa humu watasema nini, as long as ninachoshauri ni kitu cha kweli, hivyo nawashauri Chadema, wawe tayari kupokea na kuuzingatia ushauri wowote, hata kama ushauri huo unatoka kwa kichaa au kwa shetani, ili wautumie ushauri huo kujitafakari na kujitathinini, wakiuna una maana, wautumie, wakiuona haina maana, waupuuze, ni busara kwa kwa kila anaejidhania amesimama, na aangalie isianguke. CHADEMA msipuuzie ushauri hata kama ni kutoka kwa shetani!, S ...

Utangulizi
Hili ni bandiko la ushauri wa bure kwa Chadema, na unatolewa na mtazamaji wa muda mrefu wa mchezo wa siasa nchini Tanzania, ambaye ameangalia chaguzi mbalimbali za nchini na nje ya nchi, tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania, (Kwahani -994), uchaguzi mkuu wa 1995, 2000, 2005, 2010, na 2015. Ushauri wenyewe ni kuhusu hii hama hama ya wanachama na viongozi wa Chadema kuhamia CCM. Naishauri Chadema wasiwabeze hawa wanaohama kama wafanyavyo CCM, bali Chadema wajitafakari, kwa sababu baadi ya hawa wanaohama Chadema, wana hoja za msingi.

Siku zote Chadema wanaendesha siasa kwa dhana potofu, wanadhani adui yao mkuu anaowafanya kushindwa kwenda Ikulu ni CCM, kiukweli adui mkuu wa Chadema sio CCM, nitawatajia adui mkuu wa Chadema, na mwisho nitawapa ushauri Chadema wafanye nini, waweze kuingia Ikulu 2025 wakati Magufuli atakapomaliza muda wake. tena only if. Magufuli atamaliza 2025!, kwa sababu kwa uchaguzi wa 2020, saa hizi tayari ni too little too late, na Magufuli ni just too powerful kiasi kwamba hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, uchaguzi wa rais wa 2020 kwa mawazo yangu nauhesabu utakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, kwa sababu mshindi tayari ameishajulikana ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo wote watakaompinga Magufuli 2020, itakuwa ni kujifurahisha tuu, hivyo Chadema watake wasitake, ni lazima wabadilike, vinginevyo...its the end of the road kwa Chadema, tunarudi kwenye nchi ya chama Kimoja.

Why Chadema?
Tanzania japo tuna vyama vya siasa zaidi ya 22, lakini vyama vikubwa ni CCM, Chadema na CUF, by now CUF is already a gone case, hivyo tunapozungumzia upinzani Tanzania, tunazungumzia Chadema. Kifo cha CUF hichoo... chaja! Upinzani kubaki CHADEMA pekee ...

Justification ya Kuikosoa Chadema kwa Mtu Ambaye Sii Mwanachama.
Mashabiki na manazi wa Chadema humu jukwaani, ukifanya ukosoaji wa Chadema, au kutoa ushauri wowote kuhusu Chadema, watakubeza unashauri kama nani?. Kwa sababu Chadema ni public party paid by taxpayers money, then the taxpayers have the right to know the conduct of their tax, hivyo Watanzania wote wana right kujua mambo yote ya Chadema, public na private, ni haki yao kwa sababu kinaendeshwa kwa kodi zao!.

Kwanini Uishauri Chadema, Kwa Wao Wenyewe Hawajioni na Kujishauri?.
Ushauri huu nautoa kwa dhana kuwa Viongozi wa Chadema, wanachama wao, wafuasi wao, washabiki wao na manazi wa Chadema humu jf, wote ni pro Chadema, wako ndani ya box la Chadema, hivyo wanaweza wasiwe na uwezo wa kuona nje ya box, soso tulioko nje ya box ambao ni watazamaji, tunaweza kuwa tunaiona Chadema vizuri Zaidi kwa nje, kuliko waliomo ndani ya chama, lakini pia kuna walioko ndani, wanayaona madhaifu na mapungufu ya Chadema from within, lakini kwa vile wamo, wanakosa objectivity ya kujiambia, kujitathinini na kujikosoa, hata hivyo tathmini ya kweli, inapaswa ifanywe na watu wa nje na sio kujitathmini yenyewe.

Chadema Isiwabeze Wanaohama, Ni Haki Yao, Ila Pia Izingatie Hoja Zao, Wana Hoja za Msingi
Kati ya wanachama na viongozi wa Chadema wanaohamia CCM, kuna wengine wanahama kimya kimya bila kusema sababu, kuna wengine wananunuliwa, na kuna wengine na haswa baadhi ya viongozi, wanapohama, wanaandika barua Chadema na kuaga kwa kutoa sababu, ziwe ni sababu za kweli au ni visingizio tuu, lakini kuna kitu wanasema, na wengine hawasemi chochote kuhusu Chadema lakini siku wanapokelewa CCM, Chadema, japo ni kweli wengi kinachowahamisha Chadema ni njaa zao tuu, na wanakwenda CCM kufukuzia fursa, lakini kuna baadhi, wana hoja za msingi sana, hivyo Chadema inatakiwa kutozipuuza hoja zao, isisikilize na kujitathmini kuhusu ukweli wa hoja hizo.

A Way Forward, Chadema Ifanye Nini.

  1. Kwanza Chadema ijitathmini, is it on the right track?, itambue makosa yake, ikubali makosa, ijirekebishe, isonge mbele. CHADEMA ni sikio la kufa? Iambiwe vipi ili isikie? Masha ana hoja za msingi, zisikilizwe, zizingatiwe, zisipuuzwe!
  2. Ianzishe grassroots recruitment ya wanachama wake waaminifu, isije kujikuta imewakumbatia CCM ndani, Chadema nje hadi ndani ya CC yake, kama ilivyotokea kwa Mwenyekiti wa Bavicha.
  3. Ianzishe headhunting na spotting leadership talents na able people toka kwenye jamii kujiunga Chadema na kujenga kada ya viongozi wake wa kesho, born and breed in Chadema, kwa kuwafanyia grooming, ili kupata wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi.
  4. Ipunguze kushobokea makapi kutoka CCM, wana CCM wanaojitoa CCM na kujinga Chadema, wawe wanachama wa kawaida tuu kama wanachadema wengine na sio kupapatikiwa na kupewa uongozi moja kwa moja.
  5. Chadema I invest on people na mass mobilization, na sio ku invest on vitu na mikutano tuu ya hadhara, kupitia social media na kumiliki media yake yenyewe, kutawafikia watu wengi Zaidi kuliko kutegemea mikutano na maandamano pekee.
  6. Chadema irudishe ukomo wa uongozi, hata kiongozi awe mzuri vipi, anafikia kiwango cha ukomo wake na kuwa kama saturated solution, he can do no more than what he can!, anakuwa hana jipya!, pia Chadema waandae succession plan, by now, wawe na a pool of able people from within kushika nafasi zote za uongozi, na kuendesha serikali, kungekuwa na ukomo, by now watu wangejua Mbowe amefikia ukomo wa uwezo wake, hivyo nani watampokea.
  7. CCM ni chama dola, hivyo Chadema isitumie model ya CCM kuitafuta ikulu, iandae model yake yenyewe ya kupata viongozi wake na wagombea wake, mtindo wa the democrats ya US ni mzuri kuanzia kwenye primaries.
  8. Kuondokana na viongozi ving'ang'anizi na miungu watu, maadamtarget ni kuingia ikulu, umeshindwa kuuingiza Chadema ikulu, unapisha wengine wanaendeleza, sio umeshindwa hala unang'ang'ania!.
  9. Kuwafanyia tathmini wabunge wake na kukubalika kwao, na kuwe hakuna haki miliki ya majimbo, mfano 2020, Mdee anatathminiwa amefanya nini Kawe for 10 years, na jee bado anakubalika?, Wanachadema wote wenye uwezo, wawe huru kumchallenge Mdee, akitokea mwanachama mwingine mwenye sifa Zaidi, uwezo Zaidi na kukubalika Zaidi, Mdee anawekwa pembeni, vinginevyo 2020, kuna majimbo kibao Chadema mtayarudisha CCM!.
  10. Chadema kionyeshe ukomavu na kuwa ni chama mbadala kwa kuachana na cheap politics ya siasa za matukio, na kujikita kwenye real politics ya kushindanisha sera, sio kwa kupinga kila kitu, CCM ikifanya mazuri, mfano elimu bure, Chadema ikubali hili ni zuri, lakini ionyeshe ingekuwa Chadema ingefanya bora zaidi kwa elimu bure hadi chuo kikuu, kwa kuonyesha how CCM inatapanya fedha kwa mambo yasiyo na maana, halafu inanyanyasa Watanzania masikini kwa kuwanyima mikopo. Chadema wajifunze kuibomoa CCM kwa hoja na sio siasa za matukio, mfano mwaka 2020, Magufuli anaingia ulingoni akiwa na elimu bure, ndege za ATCL zinapaa dunia nzima, flyovers, reli ya SGR, na Tanzania ya viwanda. Chadema lazima waje na sera mbadala kuonyesha jinsi ATCL, flyovers na SGR zilivyowatia umasikini Tanzania, kama fedha hizo zingewekezwa kwenye sekta ya kilimo nini kingepatikana, bila kuinua sekta ya kilimo, hiyo Tanzania ni Tanzania ya viwanda gani vinavyotumia malighafi gani?. Ijikite kwenye hoja kama hizi Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas ...
  11. Chadema ipiganie a level playing field kwenye the political ground, kupitia tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, haiwezekani watu wawili wanagombea urais, mgombea mmoja anakuja na vingora, na full government media team, paid by public money for the advantage ya CCM, halafu, mwingine with nothing, halafu utegemee kushinda!.
  12. Chadema ipiganie true free and fair elections with maximum transparency, kama hakuna manouvers zozote zinazofanywa na Tume ya Uchaguzi, kwa nini wazueie party tallying?, wanaogopa nini, kama matokeo yote hadi ya urais yanabandikwa vituoni mbele ya mawakala wa vyama, kuna kosa gabi kama mawakala wote watakuwa na smart phones, ku scan matokeo na kutuma makao makuu kwenye tallycenters za vyama, kama haki itatendeka, then tallying za vyama zitafana na tallying ya NEC, what is it there to hide kuzuia tallying?.
  13. Chadema kutimiza majukumu yake kikamilifu kama Chama cha upinzani kazi yake sio tuu kuikosoa serikali, bali ku I check serikali kuhakikisha inafuata katiba na kutekeleza sharia, taratibu na kanuni, mfano, katika kuzuia mikutano ya kisiasa, rais Magufuli amevunja katiba wazi wazi kabisa mchana kweupe!, chama chochote makini, by now, kingeifungua shauri mahakamani, ili mahakama itoe tafsiri rasmi, kama itathibitisha rais amevunja katiba, anashitakiwa na bunge, na kuondolewa madarakani!. Mfano hata suala dogo tuu kama Daudi Bashite, nilishauri Je, wajua suala vyeti vya Bashite, linaweza kabisa kumng'oa Rais ...
  14. Chadema waipinge CCM kwa kujikita kwenye hoja zenye maslahi kwa taifa, ujinga, umasikini, maradhi, rushwa na ufisadi, kwa kuonyeshea CCM katika kipindi chote cha miaka 50, CCM imeshindwa, na katika rushwa na ufisadi, Chadema iwaeleze wananchi, CCM ndio shina na mlezi wa rushwa zote na mafisadi karibu wote ni CCM!, ili wananchi waelewe kuwa CCM inapigana vita ilivyovilea na kuvijenga.
Ni hayo kwa uchache, nikikumbuka mengine nitayaongeza.

Paskali
Katibu Mkuu awe Meya wa Ubungo Jacob,Mashinji anapwaya sana hazijui mbinu chafu za ccm na jinsi ya kupambana nazo.Jacob anawezea Pascal Mayalla
 
Back
Top Bottom