CHADEMA mjitafakari kwa hili

mserekale

Member
Jul 4, 2019
79
103
Haingii akili ninyi kama Chama Kikuu cha Upinzani kwa zaidi ya miaka kumi kukosa TV ya kurusha mikutano yenu mubashara!

Nashindwa kuelewa idara yenu ya uenezi inafanya kazi gani? Kama imekufa pia mtuambie tujue moja!

Leo mtu akitaka kujua Tundu Lissu aliongea nini baada ya kuchukua fomu ya kuomba uteuzi au akiwa kule kijijini kwao Singinda ni ngumu mno kupata hizo speech.

Karibia media zote zimewasusa na mnafanyiwa hujuma za kila aina kama kukatiwa sauti na kufutiwa speech zenu nyie mpo mpo tu. Mmejipanga kuchukua nchi kweli nyie?

CHADEMA online media inafanya kazi gani? Nilitegemea ingekuwa msitari wa mbele kufanya live streaming ya mikutano yenu lakini wapi?

Mnajua ni watanzania wangapi wanawafatilia kupitia mitandao ya kijamiii?

Mjitafakari!
 
Haingii akili ninyi kama chama kikuu cha upinzani kwa zaidi ya miaka kumi kukosa TV ya kurusha mikutano yenu mubashara!

Nashindwa kuelewa idara yenu ya uenezi inafanya kazi gani? Kama imekufa pia mtuambie tujue moja!...
Walianza kufungia magazeti ili usije ukasoma habiri kinzani hata hiyo TV ingelifungiwa tu, rudisha nyuma kumbukumbu zako kilichotokea kwenye bunge live
 
Suala la kutokuwepo kwa 'coverage' katika matukio ya kisiasa ya vyama vya upinzani si kosa la Chadema hata kidogo; ni kosa la idara ya habari na mfumo mbovu uliopo wa upashanaji habari nchini, unaosababishwa na tabia ya chama tawala ya kuvitisha vyombo vya habari (press intimidation).

Utaratibu unaousema wa Chadema kuwa na "TV yao" ni utaratibu ulio butu - mufilisi! Hakuna nchi yoyote duniani iliyo na utaratibu huo, bali vyombo huru vya habari ndivyo hupaswa kutimiza wajibu wao kwa kuripoti taarifa za pande zote "without fear or favour".

Hebu tuambie, umeshawahi kusikia kwa mfano eti chama cha Democrats cha US, au chama cha Labour cha Uingereza kina "TV yake" ya kurusha taarifa zake chenyewe? Tusipende kuvitupia lawama vyama vyetu vya upinzani kwa kila tatizo linaloibuka, hata kama tatizo hilo linasababishwa na udhaifu wa kimfumo!
 
Pamoja na hujuma katika media dhidi ya Chadema, Sababu Ni moja tu, kwamba mamlaka zinahofia teknolojia na utandawazi.

Kuwa zitaawamsha wajinga ambao hutumika Kama mtaji wao. Ila Cha kufurahisha HUWEZI zuia nyakati na Teknolojia. "THE TRUE JUDGE IS TIME"
 
mserekale,

Ingekuwepo ingefungiwa tu na huu utawala wa dikteta John Magufuli
Lakini Muhimu kitengo cha Uenezi kiwe na Plan B inasikitisha sana hata CHADEMA media haichukui matukio live.

Fanyeni kila linalowezekana kurecord matukio yote yarusheni you tube whatsapp groups na facebook sisi tutayasambaza.

Kama tumenyimwa haki ya kusikika na vyombo vya habari huu siyo wakati wa kulia lia ni wakati wa kupambana.

Dunia ya leo main stream media hazitazamwi sana kama social networks hivyo tutumie social media to the fullest
 
Haingii akili ninyi kama chama kikuu cha upinzani kwa zaidi ya miaka kumi kukosa TV ya kurusha mikutano yenu mubashara!

Nashindwa kuelewa idara yenu ya uenezi inafanya kazi gani? Kama imekufa pia mtuambie tujue moja!...
huyu mbona angezitungia sheria ili zifungwe fasta kama alivyofanya kwa magazeti
 
Hiyo TV ingepewa leseni na nani wakati vyombo vya habari vilivyopo linatishiwa endapo vitarusha habari za CDM.

Umejiuliza kwa nini ITV ama hata Azam au wengine hawakutaka hata kusogea Ukumbi wa mkutano wa CDM?
 
Haingii akili ninyi kama Chama Kikuu cha Upinzani kwa zaidi ya miaka kumi kukosa TV ya kurusha mikutano yenu mubashara!

Nashindwa kuelewa idara yenu ya uenezi inafanya kazi gani? Kama imekufa pia mtuambie tujue moja!

Leo mtu akitaka kujua Tundu Lissu aliongea nini baada ya kuchukua fomu ya kuomba uteuzi au akiwa kule kijijini kwao Singinda ni ngumu mno kupata hizo speech.

Karibia media zote zimewasusa na mnafanyiwa hujuma za kila aina kama kukatiwa sauti na kufutiwa speech zenu nyie mpo mpo tu. Mmejipanga kuchukua nchi kweli nyie?

CHADEMA online media inafanya kazi gani? Nilitegemea ingekuwa msitari wa mbele kufanya live streaming ya mikutano yenu lakini wapi?

Mnajua ni watanzania wangapi wanawafatilia kupitia mitandao ya kijamiii?

Mjitafakari!

Utawala huu wangeshafungiwa. Maana wanaogopa hata kivuli tu cha wapinzani
 
Back
Top Bottom