CHADEMA mbona hamueleweki?

..but, what if chama cha upinzani kikishinda uchaguzi kama ilivyotokea Ghana?

..Je CDM sasa wanapaswa kuwapinga rafiki zao walioingia madarakani uchaguzi uliopita ili waporomoke na kuwa chama cha upinzani?!
Kama ni chama rafiki cha muda hakuna tatizo. Jubilee na CHADEMA hawakuwahi kuwa marafiki isipokuwa sasa
 
Tafuta speech ya Mbowe alitoa ufafanuzi kuhusu hili akiwa Tanga.

Pia unamaanisha tukimuunga mkono mpinzani leo, alafu kesho akiingia madarakani tunapaswa kuwa adui yake??

2013 mlimpigia kampeni nani? Je huo urafiki wa kivyama ulikufa lini??
 
Tatizo sugu katika siasa za Africa ni ugumu wa incumbents pamoja na chama tawala kuondolewa madarakani. Hivyo, popote pale barani Africa ambapo watawala watashindwa uchaguzi ni jambo jema kwani linatoa funzo kwa wapiga kura katika maeneo mengine kuwa inawezekana kuchagua wapinzani na maisha yakaendelea. Wapiga kura wengi barani Africa bado hawana confidence hiyo - mara nyingi huchagua kile walichokizoea.

Tabia hiyo imefanya siasa za vyama vingi katika Africa kukosa maana - wapiga kura wanashindwa kutumia nguvu waliyonayo kupitia sanduku la kura kuwaadhibu watawala dhalili kwa kuwa hawana uthubutu wa kuchagua wapinzani. Hivyo, ni ajabu kwa Chadema inayopapambana na chama kongwe madarakani kuunga mkono incumbent huko Kenya.

Kama Raila akishinda, impact yake ni kubwa kwa siasa za Tanzania kwa maana ya kuwafanya wapiga kura kuamini kwamba inawezekana kumtoa Rais aliyeko madarakani kwa kura. Sijajua Chadema wanatumia vigezo gani kumuunga mkono Uhuru na team yake. Kwangu mimi, kumuunga mkono Uhuru na team yake ni sawa na kuunga mkono CCM.

Na jambo jingine ni kwamba hata tukibadili katiba, bado wizi wa kura ni possibility. Kenya wana Katiba mpya, very progressive, lakini bado wasiwasi wa kura kuibiwa ni mkubwa. Mawazo kwamba Tanzania tukibadili Katiba tutapata chaguzi huru na za haki inawezekana si sahihi. Kitu cha msingi ni kuwa na wapiga kura wanaojiamini, wanaojua maslahi yao, na ambao wako tayari kulinda kura zao.
 
Kama ni chama rafiki cha muda hakuna tatizo. Jubilee na CHADEMA hawakuwahi kuwa marafiki isipokuwa sasa

Urafiki ulikuwa kati ya ODM na CDM, hata 2013 walienda kupiga kampeni kule. Ukiwauliza mioyoni mwao wwtakuambia wamemkomoa JPM, maana rafiki yake kashindwa. Kumbe hawajui kuwa kuna JPM na kuna CCM.
 
Chadema kupitia Mwenyekiti wake Mh Mbowe ilishatoa ufafanuzi mrefu sana kuhusiana na Msaliti Raila , kuwakumbatia madikteta kumemponza , amevuna alichopanda .
 
Mchambuzi amekwishajibu kuwa ni official statement kutoka kwa mwenyekiti CHADEMA, na hata Ktibu Mkuu ametuma official note akimtakia Uhuru uchaguzi mwema wa Ushindi
 
Kama ni chama rafiki cha muda hakuna tatizo. Jubilee na CHADEMA hawakuwahi kuwa marafiki isipokuwa sasa

..wewe umekosea kuleta mfano wa Ghana.

..hoja yako ingekuwa na nguvu kidogo kama ungejikita Kenya na mahusiano ya CDM vs Raila + Uhuru.

..CDM wameeleza kwamba Raila aliwatupa mkono ktk uchaguzi uliopita wa Tz.

..Raila alivunja urafiki wake na CDM kwasababu aliunga mkono CCM na Magufuli.

..Msimamo huo wa Raila ndiyo umepelekea CDM kubadili kambi na kumsupport Uhuru Kenyatta.

..Pamoja na hayo, siyo kweli kwamba marafiki wote wa CDM ni vyama vya upinzani.
 
..but, what if chama cha upinzani kikishinda uchaguzi kama ilivyotokea Ghana?

..Je CDM sasa wanapaswa kuwapinga rafiki zao walioingia madarakani uchaguzi uliopita ili waporomoke na kuwa chama cha upinzani?!
Maswali haya yamejitosheleza...
 
Mimi Sio Chadema, ila vyama vya siasa huwa na mirongo inayofuta, kuna vya mrongo wa kulia (Conservative) Mrongo wa Kati(Liberal) na Mrongo wa Kushoto (Socialists)

Vyama huwa vinasapotiana kutokana na mirongo yao. Mfano: Jeremy corbyn(Socialist) ni mpinzani Ungereza lakini ana support chama kinachotawala Venezuela.

Swali lako halina taja kwamba ukiwa mpinzani lazima usupport wapinzani. Siasa haziendi hivyo ndugu.
 
Mkuu hawa walishapoteza NETWORK muda mrefu. Ni suala la kuwasamehe tu.
Sasa wameamua kuua DHANA ya upinzani wao wenyewe.

Kuna methali inasema kuwa "NDEGE WAFANANAO HURUKA PAMOJA". Kwa mantiki hiyo tulitarajia CDM kuunga mkono wapinzani wenzao kwa sababu wanafanana kwa namna mbalimbali.

Kwa namna nyingine ni kwamba, CDM sasa wamekubali rasimi kukiunga mkono CCM.(Wamekubali INDIRECTLY)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila wakili msomi nadhani japokuwa unasema huna chama lakini una mahaba na CDM, mi naona wanaeleweka sana kuwa waligeuzia gia angani, mengine yote remains to be history, ili uwaelewe vizuri ni lazima nawe uwe tayari ku engage gia pindi mwenyekiti anapofanya hivyo.
Na bado kuna mengi tu yanakuja.
 
Kinachoiua CHADEMA ni falsafa ya kuendesha chama. Wengine ndo tunasema kila siku.

Huwezi ukawa na chama ambacho matamko na fikra za mwanachama ndo sera ya chama. Haya anayofanya Lissu na Wema ni moja ya kasoro kubwa ya chadema kwa sasa.

Nakumbuka EL ndo ameonyesha mapenzi na Uhuru na si CHADEMA. Lakini mwisho chadema wamefuata kwa mkumbo.

Fikra kama hizo si za kuikombozi.

Tusubiri watu wengine wenye fikra tofauti na Mbowe hapo tutafika.

Kwa ufupi Mbowe amezidiwa akili hata na Wema. Hamna namna ya kuendelea na chama kwa mtindo huo.
 
Petro E Mselewa leo uliiazimisha Akili yako kwa mtu! Swali ulilouliza au kujifanya huelewi naona Unajipotosha wewe binafsi! Labda ukapumzike upate usingizi,ukiamka kichwa kitakuwa mahali pake pa siku zote! Hilo swali liulize kwa CCM pia, kwa nini wanaunga mkono Chama Cha Upinzani huko Kenya badala ya Chama Tawala? Je issue hapa ni kuwa Chama Tawala na Chama Pinzani ndiyo shida? Mimi naamini issue hapa ni kila mtu na RAFIKI YAKE! ADUI WA RAFIKI YAKO NI ADUI YAKO PIA and the Vice versa is true!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lets say leo tunamuunga mkono Besigye wa Uganda alafu akashinda akaingia Ikulu,
Kipindi cha kwanza kimeisha wanarudi tena kwenye uchaguzi, Je, hatupaswi tena kumuunga mkono Besigye kwasababu yuko madarakani??
Kama ni chama rafiki tangu mwanzo hakuna shida.
 
Magu alimpigia raila odinga kampen kwan nayenyew haijakushangaza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…