CHADEMA-Maendeleo, CCM-Amani

Dume la Mende

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
423
Reaction score
66
Wakati CCM wanajaribu kudumisha amani, Chadema wana mtazamo tofauto kwamba amani bila maendeleo ni bure. Je, maendeleo bila amani itakuwa vipi? Basi nashauri vyama hivi na wadau wao, wajaribu ku-synchronize the two, yaani hivi vitu viwili, amani na maendeleo, vinategemeana.
 

Kwa Tanzania, Amani = Upumbavu/Ujuha/Ujinga/Umasikini/Ufisadi/Mtaji wa CCM/
 
Hata maandiko matakatifu yanasema wazi kwamba, ni heri kulala juu ya paa na amani, kuliko ndani ya nyumba na ugomvi au vita.
 

Hapo kwenye ekundu: chadema hawasemi amani bila maendeleo ni bure bali wanasema "amani bila haki ni bure". Na kutoka hapo tunaweza kumalizia kwamba "amani bila haki hakuwezi kuwa na maendeleo". Haki ni msingi wa maendeleo na amani ya kweli. Kukikosekana haki hakuwezi kuwa na maendeleo wala amani ya kweli.
 
kukosa amani si lazima kumaanisha watu wanakurupushana kwa mapanga mkuu. kukosekana kwa amani ni dhana pana sana ambayo watu wanaitizama kwa wepesi.
Yes,, please elucidate so we know dhana hiyo.
 
Chimbuko la CCM ni "Mapinduzi", na hata kwa jina inajieleza kabisa kuwa mantiki na falsafa yake ni "Mapinduzi"..... wakati kwa CHADEMA ni "Demokrasia na Maendeleo"....! Nayo kwa jina hujieleza.....! Zaidi ni kwamba, mapinduzi wanayoita CCM hayajawahi kufafanuliwa kama ni mapinduzi ya namna gani hmaanishwa na CCM.... matokeo yake nchi ikapinduliwa miguu juu, kichwa chini...! Kwa hiyo kama CCM wanavyosema "Amani" ni kiini macho tu....! Hebu fikiria; Ukiwa baba, kila siku ukifika nyumbani, watoto na mama yao pamoja na wafanyakazi wako, huku wakiwa wameshinda njaa kutwa nzima, wanapata makwenzi walau mojamoja..... lakini kwa kuwa hakuna mwenye ubabe wa kukurudishia, wala kukuchukia hatua, wanabaki kuumia bila jinsi....! Sasa nikuulize, katika ile nyumba yako kutakuwa na amani? Au ni utulivu tu umetawala....? Hiyo ni picha halisi ya CCM kwa sababu wakiwa watawala wa nchi, lakini wananchi wakiteseka bila huduma yoyote, njaa, nk.... hutumia ubabe kuwazuia wananchi hao kufikisha hisia zao panapohusika.....! Sasa amani iko wapi? Lakini vilevile, kwa maneno mengine, "Demokrasia" huleta amani hasa pale "Maendeleo" yanapowezekana kwa kila mmoja....!
 

Amani unayoizungumzia ni ipi?
Madini asilimia 3%
Foleni massa matatu kwenda kazini
Mlo mmoja kwa siku
Amani ya kikaburu
Amani ya mabomu ya mbagala na Gongs
Amani ya wengine kulipwa millioni 12 na wewe elfu 20
Amani gani?:glasses-nerdy:
 
CCM hawahubiri amani ila wanavuruga amani kwa matendo yao..
 
Acha kupotosha watu...
 
hivi maana halisi ya amani unaifahamu!?, Hapa Tanzania amani hakuna bali kuna utulivu amani haiwezi kuwepo sehemu ambapo hakuna haki, kunaubabe, kuna dhuluma, kuna watu wanaofikiria kwamba bila wao hakuna mtawala mwingine, watu wengine wapo kwenye Neema wakati wengine wamechoka kwa ugumu wa maisha huwezi kunishawishi nikakubali kwamba hapa kuna amani.

Amani wanayohubiri ccm ni kwamba wao waendelee kutawala, kuiba fedha za umma, kugawana madini yetu, kurithishana utawala vizazi na vizazi, waendelee kuwaona watanzania mabwege, wazidi kuwanyima watanzania elimu ya kujitambua. na pia watanzania wazidi kukosa huduma bora za kijamii, hii ndiyo amani wanayotaka tudumu nayo hawa ccm.

Chadema kinaamini kwamba Haki ni msingi wa maendeleo na maendeleo ndiyo yanaleta amani, bila haki hakuna amani, na ndicho kilichopo hata huko kwa waarabu hakuna haki na ndio maana hawana amani.

Hakuna Chama kilianzishwa ili kitawale daima so Haki, maendeleo na amani bila ccm vinawezekana watanzania tuchukue hatua.
 
Kwa serikali ya CCM upumbavu mbele,amani ya fikra finyu,kubadilisha uongo kuwa ukweli,ulimbukeni mwingi wa viongozi wa CCM,kuwadanganya watanzania na kuwadhurumu mali zao na kuwafanya kuwa maskin,Chadema fikra mbele na kuwaletea maendeleo watanzania.
 
CHADEMA - Mwananchi amka usingizini, CCM-Tulia uliwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…