CHADEMA, kwanini mnacheza ngoma ya CCM Igunga? Achaneni na DC!

Chadema inawezekana mmewingia mtego wa CCM walioundaa kwa kumtumia DC wao kwa kuacha kitchen tables issue za maji, umeme,sukari
kupanda kwa gharama za maisha, elimu na ajira
na kuanza kujadili issue za DC ambazo hazimsaidii mwana igunga kwa lolote lile. CCM inapata wakati mgumu sana kuzungumzia issue hizo hapo juu hasa kumwambia mtanzania maskini pale kijijini Igunga ambaye hajui atakula nini leo yeye na familia kuwa CCM imemletea maendeleo wakati hana uhakika wa kula leo hii. CCM wanataka muache issues hizo mkimbilie issue za DC ambazo hamzimsaidii mwana igunga kupata elimu bora, kupata umeme wala chakula cha kula na watoto wake.

Nini cha kufanya kuanzia sasa.

achaneni na swala la DC liacheni chini ya timu ya wanasheria wenu na muongeze nguvu kwenye kampeni ktk issues nilizozitaja hapo juu ambapo CCM haina majawabu yake swala la DC mtakuwa na muda mwingi tu wakulijadili mara baada ya kampeni kwisha otherwise mtakuwa mnacheza mdundiko wa CCM.

Umenena vema!!! Na hii ni aibu sana kwa Magamba kumtumia huyu mama na Heshima zake!! Kwa kweli hizi njaa na tamaa za vyeo vinaimaliza Tanzania!!
 
Back
Top Bottom