CHADEMA, kwanini Dr. Slaa hachukuliwi hatua?

CHADEMA, kwanini Dr. Slaa hachukuliwi hatua?

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,829
WanaJF!

Dhana hii ya kuwajibika na kuwajibishwa imekuwa ikielekezwa upande mmoja tu, nako ni CCM na serikali yake. Tena mara kwa mara mashinikizo yamekuwa yakitokea CHADEMA, kuwa serikali iwawajibishe viongozi wenye kasoro.

Lakini kama ilivyo ada, CHADEMA imesahau kwa makusudi kabisa katika kuwawajibisha viongozi wake hasa wale wenye muelekeo wa kukichafua chama.

Kwa mfululizo wa matukio haya yaliyo muandama Dr Slaa, kama CHADEMA kingekuwa chama makini basi kingemchukulia hatua Dr Slaa za kinidhamu kwa lengo la kulinda hadhi ya chama.

Mfululizo wa matukio yenyewe ni kama ifuatavyo;

1. TUHUMA YA KUKWAPUA MKE WA MTU. Hii tuhuma sio tu kwamba imemchafua Dr Slaa na Josephine, bali imechafua CHADEMA kwa kiasi kikubwa sana mbele ya jamii ya watu wenye heshima na wastaarabu.

2. TUHUMA YA KUMPA JOSEPHINE MAMLAKA NDANI YA CHADEMA. Hii pia imeshusha heshima ya CHADEMA kwani watanzania kwa sasa wanaona CHADEMA ni kama chama cha familia.

Haiwezekani mchumba wa katibu mkuu kupewa fedha za chama kwa ajili ya ziara za mikoani. Josephine ni nani mpaka akakague uhai wa chama mikoani?

3. TUHUMA YA KUJIKOPESHA FEDHA YA CHAMA. Hii tuhuma tangu imetolewa haijawahi kupatiwa maelezo, zaidi ya kupiga piga chenga. Hali iliyo pelekea CHADEMA kuonekana kama sio chama cha siasa bali ni 'saccoss' ya watu wachache.

Kwa tuhuma hizo na nyingine nyingi dhidi ya Dr Slaa kama katibu mkuu wa CHADEMA, ingekuwa ni vyema kama chama kingechukua hatua za kinidhamu dhidi yake, hata kwa kumuondoa kwenye nafasi hiyo ili chama kiweze kurejesha hadhi yake kwenye jamii, ambayo kimsingi kwa sasa hadhi ya CHADEMA imeshuka sana kutokana na matukio haya ya aibu.
 
Mchukulie kwanza hatu yule mbaka wanafunzi, ukimaliza hapo nenda kwa Lowassa kwa kuzaa na yule mkosa ubunge wa Arusha mjini, ukimaliza uende kwa Mwigulu kwa kuzini wakati ana mke wake, halafu husisahau kupitia kwa Sitta maana alinyanyasa yule mke wake wa ndoa mpaka mauti yanamfikia, halafu husisahau yule aliyetoka kufiwa na kajukuu kake mitaani kwetu. pia pitia kwa "theki yuu vere machi, muulize wale watoto babao ni nani pia muulize na mama yake na Nape atwambie nani baba wa Nape.. list ni ndefu ukishamaliza hao njoo kwa Dk Slaa.
 
Ni kwa kuwa wana imani na CCM.

Wanapenda CCM iendelee kutawala milele, ndio maana hawaondoi udhaifu.

Ni jambo la kushangilia kwa wana CCM!!
 
Ukijua udhaifu wa adui yako, utumie kama habari za kiintelijensia kukurahisishia ushindi. Kwa nini umshauri adui yako aondoe udhaifu wake?

Kada wa CCM aliongelea OPERATION CHAOS, naona ndio mnaendelea nayo!
Soma hapa ambavyo 'Boss' wako William Malecelaalivyoandika kwenye facebook yake...Angalia sana hapo kwenye blue.

@ LE MUTUZ STRAIGHT TALK!!:
Leo kuna habari njema sana kwetu CCM, kwamba Mwenyekiti wa Chadema ameamua kujitoa kugombea Urais 2015, so I told you OUR OPERATION CHAOS is working kwani our never ending online attacks zimemfanya ajipime, ok now one more to go, next on line ni Dr. Slaa, naye ni lazima ajitoe kugombea ili our best interest Zitto ndiye awe mgombea wao 2015!

- NILIWAAMBIENI HAWA HAWANA MGOMBEA URAIS 2015, SO SASA WALE WOTE TUNAOSHIRIKIANA KUWADHOOFISHA KWA KUTUMIA MITANDAO TUZIDISHE MASHAMBULIZI KAMA ILIVYO SASA, NINALO BOMU MOJA LA KIONGOZI WAO MMOJA MAARUFU KUTAKA KUMBAKA DEMU MMOJA MAJUU NA KESI IPO MAHAKAMANI NA DOCUMENTS ZIPO, INA MAANA HUYU AKIPEWA KUGOMBEA CHADEMA AKAPATA URAIS HATARUHUSIWA KWENDA HIYO NCHI, SASA TUTAKUWAJE NA RAIS AMBAYE NI LIMITED KWENYE INTERNATINIONAL COMMUNITY? SAAFI SANA MHESHIMIWA MBOWE KWA KUJIPIMA NA KUACHIA NGAZI SASA MSHAURI NA MWENZAKO SLAA AJIPIME!!

KIDUMU CCM!

KIDUMU CHAMA TAWALA!!

HA! HA! HA! HA!

- LE MUTUZ!!
 
ni utumwa na ujinga kila siku kupost mada zinazohusu chadema
wewe uko CCM post mada zinazohusu chama chako
yako mengi humo,ufisadi,uuwaji,ugaidi,wizi,rushwa,ukiukwaji wa haki za binadamu,
kuhonga makanisani na misikitini, madawa ya kulevya, mikataba mibovu inayotuathiri sote,uuzwaji wa rasilimali zetu,
ugawaji hovyo wa vitalu, nk, hayo huyaoni eehhh?
ya chadema waachie chadema na ya CCM tuwaachie wenyewe.
wewe sio msemaji wao ndio maana kila chama kina msemaji wao.
its shame kwa kijana kama wewe kila siku kutumika badala ya kuitumika nchi yako
 
Kuwa na MKE ndio TATIZO? MBONA CCM inaoVIONGOZI kibao wenye hulka hizo na hawajajiuzulu?

Mfano ni Kiongozi wetu shupavu Mzee Rashid Kawawa alikuwa na wanawake sehemu Mbalimbali nchini lakini alikuwa anaimudu kazi yake ndani ya chama au serikalini vizuri sana

Mfano mwingine ni John Malecela alikutana na MBUNGE kijana Anna Kilango akatumia Uwezo wake na wako pamoja hiyo hauitki KUKWAPUA?

Mfano Mwingine Naibu Waziri Malima alipokuwa Guest Kisarawe... alikuwa na Mwanadada ambaye sio Mkewe unaona hiyo ni sawa?

Kama peza za CHADEMA zinakuuma --- kwanini za wana CCM walizobeba kupeleka USWISI hauziulizii? ni zaidi ya za SLAA
na zingeweza kukujengea GHOROFA la BARAFU...
 
Imefika wakati Chadema kujisafisha mbele ya jamii kuchukuwa maamuzi mazito.

Mimi nilifikiri 'night shift' inawahusu madaktari na wauguzi kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa hospitalini, kumbe magamba nanyi mnafanya 'night shift' kwa ajili ya kukiokoa chama chenu cha magamba kwa kurusha makombora kuelekea kwa CDM. Poleni kwa kazi nzito. Mungu awarehemu.
 
From Kada wa CCM:

@ LE MUTUZ STRAIGHT TALK!!:

Leo kuna habari njema sana kwetu CCM, kwamba Mwenyekiti wa Chadema ameamua kujitoa kugombea Urais 2015, so I told you OUR OPERATION CHAOS is working kwani our never ending online attacks zimemfanya ajipime, ok now one more to go, next on line ni Dr. Slaa, naye ni lazima ajitoe kugombea ili our best interest Zitto ndiye awe mgombea wao 2015!

KIDUMU CCM!

KIDUMU CHAMA TAWALA!!

HA! HA! HA! HA!

- LE MUTUZ!!

Huu ni mkakati rasmi wa chama cha mapinduzi, na wameajiriwa wengi kwa fedha za walipa kodi kufanya hii operation chaos! Sasa hivi Hamy-D ndiye captain wa kikosi cha operation chaos!

Angalia kamusi ya kiingereza neno Cliche. This has become a cliche!
 
ni utumwa na ujinga kila siku kupost mada zinazohusu chadema
wewe uko CCM post mada zinazohusu chama chako
yako mengi humo,ufisadi,uuwaji,ugaidi,wizi,rushwa,ukiukwaji wa haki za binadamu,
kuhonga makanisani na misikitini, madawa ya kulevya, mikataba mibovu inayotuathiri sote,uuzwaji wa rasilimali zetu,
ugawaji hovyo wa vitalu, nk, hayo huyaoni eehhh?
ya chadema waachie chadema na ya CCM tuwaachie wenyewe.
wewe sio msemaji wao ndio maana kila chama kina msemaji wao.
its shame kwa kijana kama wewe kila siku kutumika badala ya kuitumika nchi yako

Mkuu, wewe una kompyuta na keyboard yako ipo sawa, kwanini usianzishe thread kuhusu mada ulizozitaja?

Mimi nachofahamu wahusika wote wenye hizo tuhuma walijiuzuru, sasa niweke thread ya nini?

Huyu Dr Slaa ambae mpaka sasa ni katibu mkuu wa CDM ingawa tuhuma kibao zina mkabili ndio yapaswa kuhoji!
 
Umemsahau na kiongozi mwingine mwenye tuhuma za kuuza pembe za ndovu.
 
Mkuu, wewe una kompyuta na keyboard yako hipo sawa, kwanini usianzishe thread kuhusu mada ulizozitaja?

Mimi nachofahamu wahusika wote wenye hizo tuhuma walijiuzuru, sasa niweke thread ya nini?

Huyu Dr Slaa ambae mpaka sasa ni katibu mkuu wa CDM ingawa tuhuma kibao zina mkabili ndio yapaswa kuhoji!
Kinana ana tuhuma pia. Ameshajiuzulu?
 
Wewe bila ya kupost ishu za CHADEMA na dr Slaa siku hujaingiza?ufisadi wa viongozi wako kina kinana JK na lowasa kuanzia BOT madini hadi maliasili hauwausu?kweli Lumumba MAPINDA ni wengi
 
Kinana ana tuhuma pia. Ameshajiuzulu?

Mwaka 2009 ndio hilo sakata liliibuliwa. Kesi ikaenda mahakamani na mahakama haikuona uhusika wake.

Na ukumbuke Msigwa anasema hayo bila kuwa na ushahidi wowote zaidi ya kutaka umaarufu wa lazima.

Jambo la faraja ni kwamba watanzania wamemshtukia Msigwa kuwa ni muongo na anapaswa kupuuzwa.

Kwa muktadha huu; CCM haiwezi kuchafuka kwa pumba anazo eneza Msigwa.
 
Mungu is always correct. Ndio slaa kwenye chadema
 
Mungu is always correct. Ndio slaa kwenye chadema
Kwani ile operation chaos aliyotwambia kada wa CCM William Malecela (Le Mutuz) imekamilika? Au ndio hii inaendelea?

@ LE MUTUZ STRAIGHT TALK!!:

Leo kuna habari njema sana kwetu CCM, kwamba Mwenyekiti wa Chadema ameamua kujitoa kugombea Urais 2015, so I told you OUR OPERATION CHAOS is working kwani our never ending online attacks zimemfanya ajipime, ok now one more to go, next on line ni Dr. Slaa, naye ni lazima ajitoe kugombea ili our best interest Zitto ndiye awe mgombea wao 2015!

- NILIWAAMBIENI HAWA HAWANA MGOMBEA URAIS 2015, SO SASA WALE WOTE TUNAOSHIRIKIANA KUWADHOOFISHA KWA KUTUMIA MITANDAO TUZIDISHE MASHAMBULIZI KAMA ILIVYO SASA

KIDUMU CCM!

KIDUMU CHAMA TAWALA!!

HA! HA! HA! HA!

- LE MUTUZ!!

Back
Top Bottom