KAMUGUNGA
JF-Expert Member
- Mar 25, 2013
- 238
- 269
Kuna mtu anaweza kuhoji kwamba kwanini hili niliweke hapa na sio kulipeleka moja kwa moja ofisini, kwangu naona ni muhimu kuliweka hapa ili Makamanda wote wapate kulijua na kulifanyia kazi wakati chama kikiandaa miongozo kuhusu hili.
Ni wajibu wa kila mwanachama wa chama chochote kiwe cha mpira, siasa, saccoss nk kulipia ada kwa uendeshaji wa Chama husika na kuimalisha ustawi na uenezi wa chama hicho.
Kwa wale Makamanda wa Chadema wenye kadi; Kipengere cha pili(2) cha wajibu wa mwanachama na kinasomeka hivi; "Kuchangia ghalama za uendeshaji chama kwa njia ya ada ya uanachama ya kila mwaka na kwa michango mingineyo inayoamriwa na vikao vya chama".
Hili halipingiki kabisa kwamba kila mwanachadema anawajibu wa kuchangia uendeshaji wa chama. Lakini ni lazima tukumbuke kabisa kwamba upatikanaji wa rasilimali vifaa ndani ya chama imekuwa changamoto hivyo mara nyingi na kwa watu waliowengi walikuwa wanahangaika na kadi ambazo zina kiingilio na ada ya mwaka mmoja tu na hata wasambaza vifaa hawakuwahi huko nyuma kuhimiza wanachama kulipia ada kwa vile hata wangelipia bado STIKA zenyewe zimekuwa shida kupatikana kwenye ofisi nyingi za chama.
Kwanini sasa nimeamua kuandika hili.
1. Chadema mwaka huu itapata wagombea wake wa Udiwani na Ubunge kupitia mchakato wa kura za maoni. Na maneno yaliyoenda kwa wapiga kura za maoni ni kwamba ili waweze kupiga kura lazima wawe wamelipia ada zao mpaka 2015. Zoezi hili limekuwa gumu kwa watanzania hawa wapenda chadema ambao ni viongozi hasa huko vijijini.
2. Zoezi lageuka kuwa rushwa na kete kwa wagombea. Tumekuwa tukishuhudia CCM ikipata wagombea wabovu lakini ni kwasababu mfumo wao wa kura za maoni unaruhusu tajiri aingie kwa wapiga kura na kadi mpya 5000+ ambazo akizigawa kwa wananchi basi anakuwa tayari ana mtaji wa kutosha. Sasa hata kwetu Chadema yameanza kutokea, baada ya wajanja kujua kuwa ulipaji ada ni lazima ili kiongozi apige kura; wajanja wameenda kwenye ofisi mbalimbali za Chama hasa kanda wakabeba stika za ada sasa wanatembea nazo kwenye maeneo ama wanayogombea wao ama wapenzi wao na kuzigawa stika hizo kwa masharti kwamba lazima watu wao wapewe kura maana kisingizio ni kwamba wagombea hao ndo wamezinunua na ndo kuonyesha kuwajali viongozi hao wapiga kura za maoni.
3. Kukosekana kwa muongozo kutoka kwenye ofisi za Chama. Nimejaribu kuliuliza hili kwa viongozi wa Kanda lakini majibu niliyopata siwezi kwa utu uzima wangu kuyaandika hapa.
4. Dalili za kurudia mfumo wa CCM kupata wagombea ubunge na Udiwani. Kama kila mtu lazima alipie ada na kwakuwa stika za ada zimekuwa adimu kwenye ofisi za chama na kwa kuwa kuna watu walipata kadi zao 2009/2010 nk ambao kwa mahesabu ya kawaida wanadaiwa mpaka shs6000; sioni viongozi wetu huko vijijini wakilipia ada hizi bali kutakuwepo na mwanya mkubwa sana kwa wagombea kulipia ada hizi kwa masharti ya kupewa kura na mwisho wa siku mwenye kisu kikali hata kama hafai ndiye atayepita.
5. Viongozi wa majimbo wanatumia hili kama rungu la kuwachapa watu wasiopenda wagombea waliowabeba migongoni mwao. Kuna mahali kiongozi wa jimbo alitoa kauli za vitisho kwamba yeye ndo mwenye stika za ada na anatoa kwa watu wanaompenda na watakaompigia kura mtu wake. Hii ni hatari.
Naamini Chama Changu Chadema ni makini sana na kupitia hili na jukwaa hili watachukua hatua haraka.
Ni mimi mpenda Chadema kufa na kupona.