CHADEMA: Kuna wengine watamfuata Dkt. Mashinji

CHADEMA: Kuna wengine watamfuata Dkt. Mashinji

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,626
Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini Tanzania (CHADEMA) kimesema baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Dkt. Vicent Mashinji kujiunga CCM, wapo wanachama wa chama hicho watakaomfuata.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Februari 18, 2020 Mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema, “Dkt. Mashinji tulimjua kuwa alikuwa amepanga safu ya mgombea wake wa uenyekiti (wa CHADEMA) ambaye ni Mwambe (Cecil-alirejea CCM juzi akitokea CHADEMA).”

“Mgombea wake wa urais ambaye ni Sumaye (Frederick- Waziri Mkuu wa Zamani) naye amerudi CCM, sekretariati aliyokuwa ameiandaa nayo itaondoka CHADEMA ni suala la muda tu.”

Sumaye naye alirejea CCM baada ya kujiunga CHADEMA mwaka 2015.

Dkt. Mashinji amejiunga CCM leo katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam ikiwa imepita miezi miwili tangu ufanyike mkutano mkuu wa CHADEMA na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe kutompendekeza tena kuwa katibu mkuu.

Badala yake, Mbowe alimpendekeza mbunge wa Kibamba, John Mnyika kuwa Katibu Mkuu wa Tano wa chama hicho Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania.

Baada ya kukosa nafasi hiyo, Dkt. Mashinji alieleza masikitiko yake kwamba alitamani kuendelea kuwa katibu mkuu ili aweze kumalizia mipango aliyokuwa nayo, ikiwemo maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020.

Mrema akizungumzia kuondoka kwa Dkt. Mashinji amesema, “tunamtakia kila la kheri kwa uamuzi wake huo. Kuondoka kwake hakutakuwa na athari yoyote, kama aliondoka Dkt. Willbrod Slaa aliyekuwa Katibu Mkuu kwa miaka kumi tena wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015 itakuwa yeye aliyekaa ofisini kama miaka miwili na ushehe.”

Mrema amesema si Dkt. Mashinji pekee bali kuna viongozi wengine wa chama hicho nao wataondoka kwa kuwa wana taarifa zao hasa waliokuwa wamejipanga kugombea na kushindwa kwenye uchaguzi wa ndani wa chama hicho uliofanyika Desemba 18 2019 katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

Mwananchi
 
Sawa Sawa Acha Tuone. Kauli Za Waoondoka Baadhi Yao Hawajielewi.

Unasema Siasa Sasa Basi, Mara Sitaki Kuwa Na Chama Mara Oops
Nilikaa Bila Chama Siwatendei Haki Watanzania
 
Hata Dr Slaa ,Zitto, Lawassa, Mkumbo, Waitari,Kaburu,Shibuda na wengine wangi walipotoka Chadema waliondoka na wangapi?

Sisi tusijisifu kwa Siasa za kukodi Siasa ni hoja na vitendo sio hizi zenye ukakasi ambazo zinatuacha sisi tuliokipigania chama kipindi tunaitwa majina yasiyostaha japokuwa Siasa sio uadui.

Hao wengine wanaokuja unauhakika kama Idikadi ni Imani kwao kama hao hawaji kwani waiishi Itikadi ya Chama chao yatabaki kuwa Maneno kama waliotangulia kabla Maneno yao ni hayahaya.

Mashinji tumemjua ktk hii minne kabla sisi Ccm tulikuwa hatumjui tungeneze team kama chama sio kumwona wa jirani ni bora zaidi ndo maana Mbowe anabaki kuwa Mwenyeki bora anayetengeneza team inayoonekana mbele ya jamii ya Kitanzania kwani ni kiunganishi cha Nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mashinji kaenda kujaribu kutafuta mkate wa CCM, mkate wa CDM alinyan'ganywa kula kabla hajashiba, akabaki kusema natamani niendelee kula mkate!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watahama tuu maana CCM wananunua makamanda wetu wazuri tulio wategemea CCM waonezi
 
Mwenyekiti anashindwa kutunza Chama ajiudhuru mtu mzima akivuliwa Nguo huchutama


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom