Chadema kuna ushauri hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kuna ushauri hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngekewa, Mar 14, 2011.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  CHADEMA INAFAA KUKOMAA KISIASA

  KAULI kuwa kumalizika kwa uchaguzi ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi ujao, ingawa si mpya, lakini hivi karibuni imetumika sana katika vyombo vya habari na majukwaa ya kisiasa tena ikipewa maana tofauti na iliyokuwapo hapo awali.

  Kauli hiyo ambayo mara kwa mara imekuwa ikitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa baada ya uchaguzi wao wa ndani ya chama, sasa inatumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhalalisha maandamano na tunaona huenda ndio sababu ya kubadilishwa maana yake.

  Katika maana ya awali, CCM waliitumia kauli hiyo kuponyesha makovu ya baada ya uchaguzi kwa kuwataka walioshindwa kushikana mikono, kupendana na kushirikiana kukiimarisha chama chao ili kishinde Uchaguzi Mkuu na kuongoza Dola.

  Lakini maana ya sasa ya Chadema iliyojitokeza kwa vitendo ni kuhamasisha hisia za kutengana, kuharibu mshikamano na kuzuia Serikali isipate fursa ya kutekeleza majukumu yake ya kuiletea nchi yetu maendeleo.

  Mifano iko dhahiri, kilichotokea mkoani Arusha na hata yaliyofanyika kwa mfululizo katika Kanda ya Ziwa ambako wabunge wa chama hicho, licha ya kuwa na majukumu katika majimbo yao, walifuatana na viongozi wenzao kusambaza propaganda kuwa Serikali haifanyi kitu chochote.

  Tunaona kuwa zilikuwa propaganda zenye nia mbaya kwa kuwa pamoja na kuwa walitumia usafiri wa anga na barabarani, wakapata huduma zote muhimu, hawakusikika wakisifia kazi ya Serikali katika kuboresha mazingira ya upatikanaji wa bidhaa na huduma au uboreshaji wa miundombinu kama viwanja vya ndege, ukiwemo wa Mwanza walioutumia.

  Hawakusikika, wakisifia na kuhamasisha wananchi kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu mingine kama ya barabara walizozitumia; zaidi ya kusema maneno yasiyopendeza kuhusu Serikali kuanzia mwanzo mpaka mwisho kuonesha hakuna jema linalofanyika.

  Hatua hiyo ya Chadema, tumeiona kuwa ni ya uchanga inayoonesha kutokukomaa kisiasa, kwani baadhi ya mambo waliyokuwa wakihamasisha katika jamii, yanatokana na mabadiliko ya siasa na uchumi wa kimataifa au ya hali ya hewa ambayo hakuna Serikali yenye uwezo wa kuyadhibiti.

  Kwa mfano, wanapigia kelele kupanda kwa gharama za maisha ambazo katika uchumi wa Tanzania, husababishwa zaidi na hali ya upatikanaji wa chakula na bei ya mafuta katika soko la kimataifa.

  Pamoja na Chadema kufahamu hilo, hatukusikia wakiwaelimisha wananchi kuwa hata mgogoro wa Libya unaoongeza bei ya mafuta na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha ukame, si Tanzania, Serikali wala Rais Jakaya Kikwete wanaohusika.

  Lakini juzi, tuliwasikia wabunge wawili wa Chadema, Tundu Lissu wa Singida Mashariki na wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, wakitoa kauli za kuisaidia Serikali na kuisifu jambo lililoonesha wanakaribia kukua kisiasa.

  Lissu akiwa jimboni kwake, sio katika Operesheni Sangara, alihamasisha uongozi wa vijiji katika jimbo hilo kufanya tathmini ya haraka ya hali ya upungufu wa chakula katika maeneo yao na kupeleka taarifa mapema wilayani.

  Kwa kauli zao za Operesheni Sangara, Lissu alitarajiwa aseme njaa imesababishwa na Serikali iliyopo madarakani, lakini alitoa kauli ya kiutuuzima, kama kiongozi kusaidia Serikali ipate taarifa mapema ili izuie njaa na huo ndio ukomavu tunaoona umeanza kujitokeza.

  Naye Mbilinyi akiwa jimboni kwake, alisikika akiipongeza Serikali kwa kujenga Uwanja wa Ndege wa Songwe, akisema ameridhishwa na hatua za ujenzi zinazoendelea baada ya kuutembelea na kuwataka wananchi wajipange kunufaika nao ifikapo Agosti mwaka huu ndege zitakapoanza kutua katika uwanja huo.

  Kauli kama hiyo inapingana na kauli nyingine walizosikika wakisema kuwa kazi yao si kuisifu Serikali na kwa hili, tunawapongeza wabunge hao kwa kuanza hatua zinazoonesha wanaelekea kukua kisiasa.

  Tunawashauri Chadema, kutafakari changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii na kuanza kuhamasisha wananchi namna ya kushirikiana na Serikali yao kukabiliana nazo.

  Tunatarajia ukomavu huo ukifikia penyewe, tutaisikia Chadema ikiimba Kilimo Kwanza, kuhamasisha wananchi waongeze uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, si tu ili wajipatie kipato, lakini pia wasaidie kupungua kasi ya kupanda kwa gharama za maisha.

  Tunatarajia Chadema ihamasishe vijana shuleni, kujikita zaidi katika masomo ya sayansi, ili Tanzania ijayo iwe na wanasayansi wa kutosha watakaosaidia kupaisha ndege yake ya kiuchumi na kijamii na sio kukimbia nchi yao baada ya kupotea kwa amani.

  GAZETI LA HABARI LEO
   
 2. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  sasa subiri uone negative comments toka kwa wana cdm,nafikiri hawajui maana ya siasa na opposition party wao ni kupinga tuuu hata yale mema! Hata nyerere aliongea" mnaacha yale mazuri na kuongelea ya kijinga" karibuni wan cdm tusikie pumba zenu na kutoa negative comments kuhusu hii topic
   
 3. F

  FUSO JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Kazi za chama chochote cha upinzani si kuisifia serikali bali ni kuibua uozo na kuuweka bayana kwa wananchi na hicho ndicho kinachofanywa na CHADEMA sasa tatizo lipo wapi?

  CCM walizoea kulala fofofo & Kwenda likizo baada ya kupewa nchi na kuunda serikali lakini this time ni mateso makubwa, kwa sasa kuna baadhi ya mawaziri wanaona kazi ni ngumu, spika naye kiti ni cha moto kiasi anaelemea kuiokoa serikali.

  Suala la mbunge gani afuatane na viongozi wa juu wa chama kwenda mikutanoni hiyo ni hoja dhaifu, kwani akienda mmoja au wakienda wote wewe kinakuuma nini?

  CCM fanyeni kazi mlizoziomba kwa mbembwe, sasa hivi wananchi wameelevuka hadi vijijini, si wale wa 1980 wakati wa Jembe na Nyundo.
   
 4. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Usijihami mkuu hivyo ni vijimambo tu, hiyo ndiyo maana ya opposition na ndiyo maana CDM wanapingana na ccm kwa hoja kwanza CDM haifunga ndoa na CCM, hata sera za CDM na CCM ni tofauti, ndiyo maana wanasema ukiamua kuwa kwenyesiasa lazima uwe na ngozi ngumu uwetayari kukosolewa kwa hoja na usitegemee ni lelemama, ikiwa CCM hawajawahi kuipongeza chadema hata kwa moja kwanini utegemee chadema kuipongeza ccm?
   
 5. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Kwani umesikia CDM ni CCM B? Sikushangaa sana baada ya kuona source ni habari leo.
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  another idiot in town.
   
 7. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wameshindwa kazi? wanataka kuhurumiwa?
   
 8. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hivi ambacho huwa unafanya wewe kina tofauti gani? Wewe hupinga ya wanaCDM nao hupinga ya wanaCCM. Tofauti ni nini ee Kashaga na Ngekewa?
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  crapiest crapp!
   
 10. M

  Mindi JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Mhh...Inaonekana ccm na serikali yake wamepigika vilivyo!! yaani mpaka wanamquote Lissu na Sugu wanaposema kitu kinachoelekea elekea kuipongeza serikali! wanamulika mulika kutafuta sindano iliyodondokea katika rundo la majani makavu. inanikumbusha pale ambapo picha ya Mbowe akipeana mkono na JK ilivyoshadidiwa vilivyo na vyombo vya habari. na hata Mbowe alipotoa mchango wake bungeni kuchangia hotuba ya JK, alizungumza maneno ambayo yalitumiwa sana na wabunge wa ccm na vyombo vya habari, kuonesha kwamba kweli CDM inapongeza serikali. hiki ni kipimo tosha kwamba CDM wamerusha ngumi na imetua panapoumiza haswa! keep it up CHADEMA!!
   
 11. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ni shida kabisa kwani unajua kabisa ulichooandika ni upuuzi na unategemea usifiwe? Kama CDM wakiendelea kuwasifu asubuhi mchan ana jioni mtafanya kazi sasa? si mtaendelea kuiba na kujilimbikizi, mimi nina wasi wasi wewew uko nje kwa peas za mafisadi kwa hiyo unalipa fidia kwa kuandika utumbo humu JF
  Ukome!
   
 12. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni kweli hisia za kutengana na Mafisadi lazima zipandikizwe kwa watanzania, maana dawa yao ndio kuwashtaki kwa wananchi.
   
 13. Unyanga

  Unyanga JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  una uwezo wa kukosoa kwa hoja na wala sio kutumia lugha yenye maneno makali(offensive words) na watu bado wakakuelewa unakusudia nini! Ndugu zangu wa cdm tumekuwa tukitumia maneno makali sana kuanzia sisi wenyewe humu kwenye jf mpaka viongozi wetu majukwaani bila kusimamia hoja, tukifika kwenye jamii ya watu wanaojua kujenga hoja tunaaibika. Rejea mjadala wa katiba mpya pale udsm tundu lissu alipokuwa anakosolewa na prof.shivji,prof alitumia lugha laini na ya busara sana kwa mwanafunzi wake lissu ili amuelewe, matokeo yake akaja na hoja dhaifu siku nyingine pale pale udsm na hapa ni ktk topic ya dowans pale council chamber na kutaka kuwashambulia wasomi na hoja zake dhaifu na ushahidi wa uongo wa dr walter roodney, alichoambulia ni kukosolewa kwa hali ya juu na kupata aibu mule ukumbini, na wakosoaji walikuwa ni dr kibogoya(cordinator wa postgraduate udsm na mwenyekiti wa udasa) pamoja na prof shivj(mwenyekiti wa mwl nyerere proffeserial chair in pan africanism). Amkeni mbishane kwa hoja imara na maneno mazuri na sio kukashifu na kutukana. MTU MZIMA HUWA AKIRI MDOMONI ILA MOYONI HUWA AMEELEWA; NI MATUMAINI YANGU WANA CDM MTAKUWA MMENIELEWA kama na linakuwa gumu iko haja ya kuwapeleka kwa babu loliondo.
   
 14. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #14
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  mimi nadhani hata spika wa bunge alisema hili kuwa kazi ya chama pinzani ni kutafuta makosa na kuikosoa serikali pale inapokosea na lengo kuu ni kila chama kinataka kushika dola
  kwa hiyo ukilegea na ukawa na sera zilezile za zamani ukizani kuwa watu wamelala utaondoka kweli
  kuna mema yamefanywa lakini bado hatukutakiwa tuwe hapa tulipo kwani tuna rasimali nyingi kuliko nchi yeyote hapa duniani lakini bado tu masikini
  ni bora enzi za mwalimu aliweza hata kuilisha china kwa chakula kutoksa tanzania lakini sasa hivi hata kile cha kwetu ni tatizo

  so kama kuna cha kusifia watasifia kama walivyo fanya ktk kusifia hotuba ya raisi wakati wa kufungua bunge na kama kuna mabaya watasema na hiyo ndio siasa ilivyo

  ni bora ukajisifia kuliko kusubiri kusifiwa mkuuuu
   
 15. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Source yenyewe HabariJANA, that y lina pumba za mwaka JANA, YES kila kitu kimesababishwa na serikali, mpaka tuwaondoe tuwafunze namna ya kuongoza nchi, unaogea utumbo mama mzima, Njaa Tz nani kasema? Mito, mabwawa, maziwa kbao "kama yako" ocean, mabonde kbao, Mungu akupe nin tena? Ukame wa muda gani kuna nchi hazijawah kupata mvua miaka sasa, Marekani wametunza mafuta ya kutumia zaidi ya miaka 40, nyie hata wiki hakuna, ccm bana sometyms mafuta yapanda meli zimejaa bandarin! Nyukilia, gesi, makaa, upepo, tunayo mnatuzingua na genereta"dowz" mvua o ukame, wacha tuwafundishe kuongoza nchi... pm**f aliewatuma mwambien hvyo Mpaka kieleweke ppplzzzzzz!
   
 16. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Sikuwahi kuona umesifia Chadema hata siku moja, wewe ndiye hasa utoaye negative comments, yaani hata chadema wafanye nini utawapinga tu.

  Mimi nafikiri wabunge wa CCM wangeanza kwanza kuona ukweli na wakaweka maslahi ya taifa mbele kuliko ya Chama, tatizo la hawa wazee wa CCM ni chama kwanza taifa baadae. wanafikiri watakuwa wanawakilisha CCM milele wakamuulize John Samweli Malecera. sasa Yupo Kimya!!!!.

  Kujenga Miundo Mbinu ni Wajibu wa Serikali yoyote na sioni cha kuisifia, Watatue Kero zilizopo, Umeme,Mfumuko wa Bei, Ufisadi wa Pesa za Serikali, inaelekea wewe hujui Ufisadi uko wapi, angalia wahasibu wote wa Halmashauri jiulize mishahara yao ikoje na ulinganishe na Mali walizonazo ndio utapata majibu!!?, Utalia ukiambiwa 70% ya Budget ya Halmashauri Huliwa na Hawa watendaji.
   
 17. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari leo!kumbe walikuwepo kwenye mkutano wa Sugu,mbona hawajaandika mengine aliyoyasema,wamechukua moja tu,kwel kuna waandish vilaza
   
 18. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kashaga + ngekewa=lipumba
   
 19. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  naona haka kamsemo kamewauma sana,jamani tunajenga nchi moja kwanini tugombanie fito? wana CDM siasa sio chuki hakuna haja ya kutukanana tunapotoa hoja zetu! tutoe hoja zinazojenga na so kubomoa
   
 20. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  yani nilivyoona heading nikajua habari ya maana, kumbe imetoka habari leo mtetezi wa Mafisadi.ulitarajia comments gani toka kwao kama sio kupunguza presha ya chadema ya kusfisha nchi, keep going CDM nyie ni wanaharakati wa kweli TZ
   
Loading...