CHADEMA kumsafisha Lowassa!

CHADEMA kumsafisha Lowassa!

Chadema itashirikiana na mtu yeyote aliyetayari kuiangusha ccm hata kama ni shetani chadema tutampa sapoti ilimradi tuteketeze maccm.

Tuliwaambia kuwa CHADEMA ni WAHAINI mkakataa. Kwa kauli hii inathibitisha kuwa mna ushirikiano na KAGAME.
 
Kuna habari zimeanza kuzagaa kuwa CHADEMA wanapaswa kumsafisha Lowassa kupitia chama chao ili aweze kugombea urais kwa tiketi ya UKAWA kupitia CHADEMA.

My take: CHADEMA tegemeeni chama kuondoka mikononi mwenu mana Lowassa anakuja na timu yake na hela yake hapo ni njia ya kutimiza malengo yake yeye na mtandao wake. So tegemeeni CHADEMA kutumika kama condom kama Shibuda alivyo kitumia
haiwezekani kuna watu wamekijenga chama muda mrefu mpaka mabomu wamepigwa Leo kuelekea uchaguzi eti watu wanahamia hayo mambo mtatuboa wapenzi Wa CHADEMA.
Kama kumtumia shetani kumuondoa shetani kunafaida basi lowasa atumike ili mradi shetani sisiemu aondoke.
 
Kwa hiyo unataka Lowassa akija Chadema afukuzwe? Chadema haichukii mtu bali matendo maovu
 
Chadema itashirikiana na mtu yeyote aliyetayari kuiangusha ccm hata kama ni shetani chadema tutampa sapoti ilimradi tuteketeze maccm.

Hayo ni maneno ya mtaani vijiweni kwa waliokosa kazi wala yasikupe shida, just relax!!

kuna watoto wamekipigania chama hapa Leo unambiwa kaa pembeni agombee mwingne kisa kuelekea u chaguzi mkuu ili tushinde sasa kumbe makelele tunayopga tunajidanganya tuuu hata makinda akija tutaimba pipoooooz wakati ccm wana tuua kina lowasa walikuwepo na wengne walitoa hela kutugawa wapinzani Leo ndio icon ya ushindi kwel pesa inanunua vhochote.
karibuni kina Chenge na mafisad wengne Wa Ccm huku chadema

Usidanganye watu wewe hata NYERERE hakuwahi kupigana vita ya kudai uhuru lakini alikaribishwa na wazee waliopambana na wakoloni na akapewa heshima kubwa ya kuwa rais wa kwanza.

Mandela aliwasamehe makaburu pamoja na udhalimu wao.

Kupigwa mabomu hakujaanza leo tangu enzi za mwalimu mtu akikaidi anapigwa tu.

UKAWA muwe makini na makundi ya watu wanaowapotosha ili mukose mamilioni ya kura za wafuasi wa Lowasa .
Lowasa ni tishio kwa uhai wa CCM . Anakubalika kila upande wa Tanzania.

Hakuna Uadui kwenye siasa. Lowasa atawaunganisha watanzania wa vyama na makundi yote ,atakua ni rais wa watu sio KITENGO .

Tukiendekeza chuki za kisiasa tutabomoa nchi.
CUF ndio wapinzani waliouawa zaidi lakini walisamehe na kukaa pamoja na wauaji wao.
Huu ni mfano bora wa kuigwa katika kujenga umoja wa watanzania. Tunataka siasa za shamrashamra na upendo na hamasa na mbwembwe nyingi kama anavyofanya Lowasa sio chuki na matusi. Tunataka kufurahia demokrasia sio kugawanywa kwa chuki.
Wapiga kura wataamua nani wa kumhukumu kwenye sanduku la kura.

UKAWA tumieni hii fursa ya makosa ya CCM kumtoa mchezaji mahiri na mfunga magoli Edo iwe ni zamu yenu kupumua sasa kwa kuunganisha nguvu na kuingia ikulu .Kama ni mabomu sasa iwe ni zamu ya CCM kupigwa watakapokuwa chama cha upinzani.

Hata baada ya vita ya Kagera sio kila askari aliyepigana alipandishwa cheo.Vigezo viliendelea kuwa ni vile vile vya mwenye sifa zaidi.

Ni rahisi JK kumkabidhi Lowasa nchi chini ya UKAWA kuliko mgombea mwingine toka chama cha upinzani kutokana na uzoefu wake ndani ya serikali na imani kubwa waliyonayo watanzania kwake.
 
Duniani hakuna kosa lisilosameheka, Lowassa ni binadamu kama binadamu wengine ikiwa kweli alipotoka au alipotoshwa basi hana budi kusamehewa.
 
Zaidi ni ngumu Lowasa kuhama CCM kwani upo uwezekano amewekewa ulinzi mkali ktk nyanja zote kutokana na kufahamu siri nyingi za chama chake.
Akijaribu kuhama tu..........
 
Zaidi ni ngumu Lowasa kuhama CCM kwani upo uwezekano amewekewa ulinzi mkali ktk nyanja zote kutokana na kufahamu siri nyingi za chama chake.
Akijaribu kuhama tu..........
wewe humjui mmasai
 
mamlaka pekee yenye uwezo wa kumsafisha mtu ni mahakama c vinginevyo
 
wewe humjui mmasai

Mmasai mbele ya Serikali?
Tambua sasa macho ya serikali yapo kwa Lowasa kwa sasa na si pengine.

Wanajua siri zao zote zawezatolewa wakifanya mchezo. Hata usalama wa Taifa pia utakuwa na jukumu hilo.

Tuzidi angalia picha.
 
Hofu yangu ni pale Lowasa akiukosa huo urais kupitia CDM.......

Tutaishia kusema kulikuwa na NCCR, CUF na CDM........

Time will tell
 
wewe humjui mmasai

if you are going to kick authority on teeth you might as well use two feet kumbuka mwenyekiti wa ccm ndio amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama yeye ndie mahakama zipo chini yake yy ndie kauli yake ni sheria sasa kama leo mmasai anayo vyote nilivyovtaja hapo juu ajabu ku kick authority
 
Ukawa angalien kuweka mgombea makin ili tushinde lowasa anafaa manake mkimueka lipumpa chadema watamaind mkimueka slaa ukawa utavunjika mueken Lowasa ashatabiriwa na TB joshua atakua rais
 
Kuna habari zimeanza kuzagaa kuwa CHADEMA wanapaswa kumsafisha Lowassa kupitia chama chao ili aweze kugombea urais kwa tiketi ya UKAWA kupitia CHADEMA.

My take: CHADEMA tegemeeni chama kuondoka mikononi mwenu mana Lowassa anakuja na timu yake na hela yake hapo ni njia ya kutimiza malengo yake yeye na mtandao wake. So tegemeeni CHADEMA kutumika kama condom kama Shibuda alivyo kitumia
haiwezekani kuna watu wamekijenga chama muda mrefu mpaka mabomu wamepigwa Leo kuelekea uchaguzi eti watu wanahamia hayo mambo mtatuboa wapenzi Wa CHADEMA.
You are absolutely correct sir,waache wajaribu alafu CDM ibaki historia.
 
Back
Top Bottom