Mimi naishauri CHADEMA kuwa badala ya kumjadili Rais, wangejijadili wao wenyewe. Upepo ninouona kwao sio mzuri. Wana ushabiki, sio ufuasi, hilo ni tatizo kubwa. Wana washangiliaji hawana wapiga kura. Cha kusikitisha zaidi na zaidi ni ule mfano wa mkutano mkuu wa wilaya kuitishwa lakini wajumbe wasiwepo mpaka watafutwe kwa simu, narejea mkutano wa Kinondoni ambayo ina mbunge wa CHADEMA.