CHADEMA Kulikoni Wilaya ya Kilosa???

CHADEMA Kulikoni Wilaya ya Kilosa???

- Toka Jumapili nipo katika ziara ya kikazi ya Wazazi/CCM Taifa katika Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro, tulianza na Gairo, Ifakara, Mahenge na leo ilikuwa zamu ya Kilosa na nipo hapa sasa hivi na kesho nitakuwa Mvomero na Mzumbe University. Kilichonishitua hapa Kilosa ni kuona kwamba hakuna CHADEMA presence kabisa, yaani hata Madiwani wote ni wa CCM, I mean ni vigumu sana kwetu CCM kutawala bila kukumbushwa mapungufu yetu na Chadema sasa wanapokuwa hawapo kabisa mara nyingi inapelekea Viongozi wetu wa CCM kujisahau.

- Halafu inakuja hoja yangu ya msingi, Vipi CHADEMA kumpeleka Slaa DC Washington badala ya kumleta huku Kilosa aje ajaribu kufungua matawi? I mean Tawi la Kilosa si linaweza kuwa muhimu kwa Chadema kuliko tawi la wanachama wanne la DC Washington/USA? Chadema ni muhimu sana mkaangalia priorities zenu kwa sababu hii no moja ya changamoto kubwa inayowatesa sana ya kukimbilia kuanzisha matawi ambayo ni fruitless huko nja na kwa gharama kubwa kuliko kuhangaikia hapa Bongo kwa gharama ndogo na yenye matokeo ya kura kwa chama chenu.

- I mean kesho Mvomero, it was great kufika Mhenge tena jana the place that was once my second home kwa sababu ndipo niliposoma Sekondari, I went there jana na kuwaahidi Shule kwa ujumla kwamba nitawakusanya watu wote maarufu waliowahi kusoma pale kusudi tuwasaidie na changamoto zao, pia niliongea sana na DC na Mkurugenzi wa Wilaya kuhusu kuwapatia gari la Shule, wameniahidi watalifanyia kazi so Mahenge angalau kidogo CHADEMA wapo, jamani ni muhimu sana Chadema mnapokuwepo maana mnasaidia sana kutuamsha CCM tunapolala kidogo!!

- Hapa ni bwenini Nyerere Dom na hiki ni kitanda cha deka nilicholalia Miaka 30 iliyopita nilipokuwa nasoma hapa Kwiro Sekondari, it was great to be here again ninamshukuru sana Mungu kwa kunipa nafasi ya kurudi tena hapa nikiwa mzima.

Le Mutuz

Mimi nafikiri ungeenda kumsaidia mzee Malechela kipindi kile ameangushwa na kibajaji badala ya kujidai wewe ni msemaji wa cdm!!!!!!!!!! PIa nakukumbusha hata mama yako mdogo Anie Kilangoo alichakachua ubunge kule same sasa unauliza cdm haina madiwani kilosa ili iweje na wewe unajua kila unachokifanya na nyinyiemu yenu. Huko Mvomero kwenyewe mlichakachua udiwani maeneo 3 na ubunge pia mlipoka. Ni majimbo mangapi ninyi mlikubali washinde wapinzani????Kila aliposhinda mpinzani kuna watu walijeruiwa vibaya sana na pia mliwafungulia kesi karibu wabunge wote wa cdm walioshinda????sijui ulisomea wapi hata kakumbukumbu kadogo tu hauna, anagalia hata katiba mpya mnavyochakachua. Tena huko mvomero baba yako Malechela anamiliki ardhi kubwa kiujanja ujanja ambayo leo ingesaidia wakulima na wafugaji na matokeo yake watu wanauana kwasababu ya kukosa sehemu za malisho.

WAKAZI WA MVOMERO: AKIJA HUKO HUYU GAMBA MUULIZENI MAENEO ANAYOMILIKI BABA YAKE ALIYAPATAJE NA KWANINI WANANCHI WANAUANA KWA KUKOSA MAENEO YA MALISHO YA MIFUGO??? KAMA HUYU NDIYE MTOTO WA BABU BASI HAPA KALA ASALA.
 
Wewe Wiliamu kweli kichwani hakuna kitu;pole sana!!!!! Ni wapi mlikubali chadema au chama kingine cha upinzani kishinde bila matesi kama siyo jimbo la Vunjo tu!!!!!!! Leo unajidai unataka Dr aende kilosa,mbona arusha mlipiga mabomu na kuua watu tena kwa ajili ya udiwani tu ili japo mpate kata moja!!! Wewe ulipaswa ukamsaidie kumbakumba maana tangu akalishwe chini na Mzee wa matusi ajaonekana tena si kampeni za chaguzi ndogo wala nini!!!Kafanye uenezoi mtere umrudishe kundini babu
 
jamani nauliza hakuna mdhibiti wa hizi kofia za stashahada? maana zinatumika vibaya mpaka wehu kama willie anavaa hii haikubaliki
 
Mnaifanyia kazi chadema penda msipende. Kila wilaya unayotembelea usisahau kufanya tathmini ya uhai wa cdm na kutoa report hapa. Utakuwa umeisaidia sana katika kupunguza gharama za mwanzo.
 
Willy,

Umesomeka vyema kabisa na kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na hoja yako. Welldone kwa kuwa mkweli.
 
Mimi nafikiri ungeenda kumsaidia mzee Malechela kipindi kile ameangushwa na kibajaji badala ya kujidai wewe ni msemaji wa cdm!!!!!!!!!! PIa nakukumbusha hata mama yako mdogo Anie Kilangoo alichakachua ubunge kule same sasa unauliza cdm haina madiwani kilosa ili iweje na wewe unajua kila unachokifanya na nyinyiemu yenu. Huko Mvomero kwenyewe mlichakachua udiwani maeneo 3 na ubunge pia mlipoka. Ni majimbo mangapi ninyi mlikubali washinde wapinzani????Kila aliposhinda mpinzani kuna watu walijeruiwa vibaya sana na pia mliwafungulia kesi karibu wabunge wote wa cdm walioshinda????sijui ulisomea wapi hata kakumbukumbu kadogo tu hauna, anagalia hata katiba mpya mnavyochakachua. Tena huko mvomero baba yako Malechela anamiliki ardhi kubwa kiujanja ujanja ambayo leo ingesaidia wakulima na wafugaji na matokeo yake watu wanauana kwasababu ya kukosa sehemu za malisho.

WAKAZI WA MVOMERO: AKIJA HUKO HUYU GAMBA MUULIZENI MAENEO ANAYOMILIKI BABA YAKE ALIYAPATAJE NA KWANINI WANANCHI WANAUANA KWA KUKOSA MAENEO YA MALISHO YA MIFUGO??? KAMA HUYU NDIYE MTOTO WA BABU BASI HAPA KALA ASALA.

Sijui nikuweke kwenye kundi gani kiumbe wewe?. Mbona haya unayoyaandika hapa ni tofauti na mada iliyopo?.
Ni hekima kama ungefungulia ama ungeanzisha topic hizo badala ya kuchanganya?.
Kwanini unawahusisha wazazi?, naona una mapungufu makubwa katika kufikiria. Unahitaji matibabu bila shaka una mtindio wa ubongo.
 
- Jamani swali nililouliza mbona ni dogo sana kwamba kwa nini Chadema hawapo hapa Kilosa? Sasa kama kweli hapa Kilosa tu hampo je mtaweza vipi kushika Dola kama mnavyodai bila kuwepo sehemu muhimu kama hizi? Mbona ni swali dogo sana I mean Mheshimiwa Mwigulu anatokea Chama Tawala so akienda USA ni kuendeleza tu mwendo wa kasi zaidi, ila Slaa kwenda DC Washington na huku Kilosa tu hampo kabisa inaleta maswali mengi sana kuliko majibu, au mnasemaje?

Le Mutuz

Kilosa ni miongoni mwa wilaya zenye hali duni sana kiuchumi,na ni miongon mwa wilaya zenye HATI MBAYA YA CAG kwa sababu ya UBADHILIFU wa HALMASHAURI YA WILAYA,pia ipo nyuma kielimu kwa sasa tofauti na zamani,ukiangalia maisha ya wana kilosa kwa ujumla hayaridhishi,hakuna fursa,hakuna kiwanda(kulikua na kiwanda cha kutengeneza mazulia-carpet) na cha kukamua mafuta ya pamba,pia kwa swala la kilimo ni kwamba wana kilosa hawapewi pembejeo za kilimo,
Sasa bwana W. J. Malecela sidhan kama wana kilosa wanahitaji mambo ya siasa,ila wanahitaj kuletewa maendeleo kwa kushirikishwa au kuwezeshwa,wewe umefika kilosa na naamin umeiona hali ya kilosa,tangu wakumbwe na mafuriko serikali imewapa bati 2 na mfuko mmoja wa siment,je watajenga??
Changamoto nyingine ni kwamba Mbunge wa kilosa bwana Mkulo(MNYASA) AMEWASUSA Wana kilosa ETI kwa kuwa amegombana na katibu/mwenyekiti wa CCM wilaya,,,anataka hadi amuombe radhi,
sasa na nyie wana-CCM kama mnataka hadi mkazaniwe ndo mlete maendeleo huo pia ni ujuha
NIMEZALIWA KILOSA,NIMEKULIA KILOSA,NA SEHEM YA ELIM YANGU YA AWALI NILIIPATIA KILOSA,NAIFAHAM KILOSA
 
Last edited by a moderator:
-

- Hapa ni bwenini Nyerere Dom na hiki ni kitanda cha deka nilicholalia Miaka 30 iliyopita nilipokuwa nasoma hapa Kwiro Sekondari, it was great to be here again ninamshukuru sana Mungu kwa kunipa nafasi ya kurudi tena hapa nikiwa mzima.

Le Mutuz

Shikamoo mzee! umenipita miaka 40!
 
Tuna kushukuru mtoto wa Jumanne msaliti, ngoja tuongee na wakubwa wa kanda, pale yupo mama shujaa Mh. Kiwanga Suzan.
 
Tuna kushukuru mtoto wa Jumanne msaliti, ngoja tuongee na wakubwa wa kanda, pale yupo mama shujaa Mh. Kiwanga Suzan.
 
Back
Top Bottom