Aliposhida JK awamu ya kwanza kwa kishindo,nani aliamini kutakua na upinzani tena?sote tuliamini upinzani ulikua umezikwa na hata ilisemekana JK kaja kuua upinzani,nakumbuka kauli hiyo ilisemwa na Lipumba,akionyesha kukata tamaa kabisa,hata sisi wapenzi wa chadema tulikata tamaa.Nini sasa kimetokea mwaka huu,waliokua wamekata tamaa wamefanikiwa mara tano zaidi ya uchaguzi ulopita,walodhaniwa wamekuja kuua upinzani wameshuka toka 81% mpaka 61%.Unadhubutu vipi leo kusema Chadema inakufa? Kama bunge lililopita chadema walikua na wabunge wa kuchaguliwa 5,la sasa wakuchguliwa 23 ni mara 5 zaidi achilia mbali uchakachuaji ulofanywa,then kimahesabu ya probability,uchaguzi ujao wana uwezo wa kufanikiwa mara 5 zaidi ya wa sasa,hivyo kuwa na wabunge wa kuchaguliwa 115 baada ya kuchakachua,achilia mbali viti maalum.Kwa hiyo mkuu cheza na takwimu si kuropoka.